Msaada: Dume zima nina aibu mbele ya wanawake

Msaada: Dume zima nina aibu mbele ya wanawake

Kadi Poa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Posts
2,015
Reaction score
1,005
Jamani mimi nina aibu ile ya kuzaliwa (introverts) mbele ya mkusanyiko mkubwa wa watu kama vile harusini, kwenye sherehe na hata misibani.

Imeniwia vigumu sana linapokuja suala la kuwa na mahusiano na marafiki wapya hata suala zima la mapenzi na wanawake.

Hapa nilipo sijawahi kuwa na wanawake wapenzi wanaofika hata 20, sasa nimekaribia kufika umri wa kutaka kuoa ila ninajiuliza sijui nioe mwanamke wa tabia ya namna gani anayeweza kufanana na mimi.

Sijui nioe muongeji sana ili niweke balance ama awe full aibu kama mumewe hapa wakija wageni wakose wakuwachangamkia.

Naombeni msaada wa mawazo yani nimekwama njia panda.
MWENJEJI WA KIGOMA ILA SIO MRUNDI AMA MCONGO MAN
 
"hapa nilipo sijawahi kuwa na wanawake wapenzi wanaofika hata 20". Haha kwani uliambiwa unatakiwa kufikisha idadi gani, ili uwe normal?
mkuu naomba unisaidie kwa hili
nimekaribia kufika umri wa kutaka kuoa ila ninajiuliza sijui nioe mwanamke wa tabia ya namna gani anajeweza kufanana na mimi
 
Mwenye tabia ambazo wewe utaendana nazo na kuridhia.
juu ya sifa zote hizo ni vipi kama atakuwa ni mkimya kama mimi, nyumba si itakuwa ina bore sana hususani wakija wageni ndani
 
Una umri gani tuanzie kwanza hapo unajiita dume kumbe bado mvulana
 
mkuu naomba unisaidie kwa hili
nimekaribia kufika umri wa kutaka kuoa ila ninajiuliza sijui nioe mwanamke wa tabia ya namna gani anajeweza kufanana na mimi

Mwenyewe sijaoa, so siko kwenye nafasi nzuri ya kukushauri. Ila nadhani ndoa ni calling. We endelea na maisha yako, ukifika muda muafaka utajua tu.
 
Duh pole sana ila usikate tamaa nakushauri utafute mwanamke wa kati sio mkimya na sio muongeaji sana ila ukichukua muongeaji sana na akajua udhaifu wako basi atakuonea sana
 
Duh pole sana ila usikate tamaa nakushauri utafute mwanamke wa kati sio mkimya na sio muongeaji sana ila ukichukua muongeaji sana na akajua udhaifu wako basi atakuonea sana
wabeja sana
 
Back
Top Bottom