Hahaaaaa Karibu Mbezi Mkuu
Mimi niliumwa na tandu nadhani May mwaka huu mwezi mmoja tu tokea nihamie.
Maumivu yake acha kabisaaaaaa
Nilipanic hatari maana nilikuwa nikisikia sumu yake ni kali kuliko nyoka basi nikakiona kifo hiki hapa.
Bahati nzuri alikuwepo mtu karibu hivyo alivyoniuma tu yeye akamuona akamuwahi kumuua.
Sasa wakati anamuua mimi huku pressure juu like “Unataka nife? Yani badala uniwahishe hosp unahangaika kumuua?” Hapo najisikilizia ndio nakufa nini jamani? Hahaaaaa
Kwa hofu nilikimbilia ndani nikatafuta kitunguu swaumu kilipo nikakiponda harakaharaka nikasugua kwa nguvu juu ya jeraha maana palianza kuvimba (mimi hutumia kitunguu swaumu kama tiba nikiumwa na wadudu kama nyuki,nyigu n.k)
Nilifanya vile mara 3 kwa siku ile japo palikuwa panauma sana,baada ya hapo nikameza dawa za maumivu basi.
Maumivu yaliendelea hadi baada ya wiki yakapotea ila eneo aliloniuma ngozi ilibabuka.
Cha kufanya fanya fumigation ya nguvu hapo,zingatia na usafi pia.
Ila ondoa shaka,tandu haui.