Msaada: Dawa kwa mtu aliyeng'atwa na tandu

Msaada: Dawa kwa mtu aliyeng'atwa na tandu

Nijuavyo mm kuna walie tandu wakubwa weusi wanakuaga sana maporini na hata nge wapo wale wakubwa weusi pia nao wanakua kwenye mapori hao ndio balaa sana ila hao wa majumbani ni wakawaida wanaweza wakakuuma na usipate shida au ukapata shida kulingana na mwili wako..ila ushauri wangu jiulize kwann wanaingia ndan alafu dhibiti maana ukitafuta tiba bila kudhibiti uingiaji wao ni ni hatari.na ukiona mazingira yana hao wadudu ujue kuna wadudu wengine wapo around wa jamii hiyo.kama nge na nyoka kwahiyo kama wanatokea nje ya nyumba tafuta oil chafu zungushia nyumba yako yote
 
Pole kwa kuvamiwa na Tandu mkuu, fata ushauri wa wakuu hapo juu itakusaidia pia usiogope sana tandu hayupo kama anavyoelezewa mitaani
Shukran mkuu
 
B
Huwa nasikia kuweka barafu eneo la jeraha inasaidia. Japo sijawahi kutana na case ya mtu kuumwa na tandu.

Pia tafuta mawe wanauza wamasai yapo vizuri kwa sumu za wadudu.

Kikubwa fanya fumigation maana balaa la tandu hata akikutembea tu kama unangozi laini unavimba
Baracu Ni kwa nyuki lakini kwa ng'e na tandu hapana kwani MAUMIVU YAKE TU NI GANZI TENA PALIPO UMWA PANAKUWA BARIID KM BARAFU
 
Mkuu dawa ya kuumwa na Tandu ni very simple. Nilishawahi kuumwa na Tandu, maumivu yake sitoyasahau kwa kweli nililia ka Mtoto. MAFUTA YA TAA (KEROSINE) ndo dawa mkuu, unapakaaa pale alipopauma dakika kumi nyingi maumivu yanapotea kabisa yaan.
 
Shukran mkuu niwahi mapema uhai upo mashakani.
Dah...acha ujinga...mbona tandu chakula kizuri tu..cha msingi ni kujua jinsi ya kuwatayarisha....
626807.jpg
 
Hahaaaaa Karibu Mbezi Mkuu

Mimi niliumwa na tandu nadhani May mwaka huu mwezi mmoja tu tokea nihamie.
Maumivu yake acha kabisaaaaaa

Nilipanic hatari maana nilikuwa nikisikia sumu yake ni kali kuliko nyoka basi nikakiona kifo hiki hapa.
Bahati nzuri alikuwepo mtu karibu hivyo alivyoniuma tu yeye akamuona akamuwahi kumuua.

Sasa wakati anamuua mimi huku pressure juu like “Unataka nife? Yani badala uniwahishe hosp unahangaika kumuua?” Hapo najisikilizia ndio nakufa nini jamani? Hahaaaaa

Kwa hofu nilikimbilia ndani nikatafuta kitunguu swaumu kilipo nikakiponda harakaharaka nikasugua kwa nguvu juu ya jeraha maana palianza kuvimba (mimi hutumia kitunguu swaumu kama tiba nikiumwa na wadudu kama nyuki,nyigu n.k)
Nilifanya vile mara 3 kwa siku ile japo palikuwa panauma sana,baada ya hapo nikameza dawa za maumivu basi.

Maumivu yaliendelea hadi baada ya wiki yakapotea ila eneo aliloniuma ngozi ilibabuka.

Cha kufanya fanya fumigation ya nguvu hapo,zingatia na usafi pia.
Ila ondoa shaka,tandu haui.
Pole sana jamani.
Kwa kumuona tu huwa namuogopa sana, sasa ndio nirealize ameniuma! Sipati picha.
 
Wanasema uking'atwa wahi kumuaa, kadri anavyotembea ndio na maumivu hua makali zaidi

Uking'atwa pale alipokuuma pachanje na wembe miminia mafuta ya taa kidogo.

Nawaogopa hawa wadudu

Archduke
Tafadhali jamani. Tunaishi karne nyingine mpya sasa. Mafuta ya taa yaingie drect kwenye blood circulation? Mbona naona ni hatari hata kuliko sumu ya mdudu mwenyewe? Kuna mwingine nae kasema uchanchwe chale halafu uweke tandu aliyeunguzwa na kusagwa! Haya mambo yanaongeza matatizo kama siyo muda huo basi ni baadae.
 
Honestly sjawahi kuumwa na tandu lakini hivo ndio husema watu nimetoa tu kile nachokifaham.
Tafadhali jamani. Tunaishi karne nyingine mpya sasa. Mafuta ya taa yaingie drect kwenye blood circulation? Mbona naona ni hatari hata kuliko sumu ya mdudu mwenyewe? Kuna mwingine nae kasema uchanchwe chale halafu uweke tandu aliyeunguzwa na kusagwa! Haya mambo yanaongeza matatizo kama siyo muda huo basi ni baadae.
 
daah usiku wa kuamkia leo huyo ndumila kuwili kunipiga bite aisee hayo maumivu nayoyapata siyo mchezo..

huyo mdudu hafai kabisa mpaka sasa sijatumia dawa yeyote najikaza tu hapa na haya maumivu ila si mdudu mxuri....
sasa ivi naandaa vita na tandu ni mwendo wa kuwauwa tu maana washanikosesha amani
 
Sisi watu wa porini tunakutana sana nao hao! Nishang'atwa na Tandu 2 times!! Hawana issue yeyote!! Nyoka ndio hatari bites yake unaweza kushindwa kutembea na lazime uende hospital ila hivyo vipedecenti na scorpion hamna kitu.
 
Mkuu ondoa hofu nikweli ana sumu kali pia si mwepesi wa kupiga bite. Nadra sana ujue umejichanganya sana kwake.

Wa kumuogopa ni scorpion yaan huyo ukikatiza tu kwenye himaya yke unakula bite. Ila jihadhari na tandu ana sumu kali sana.

Huwa akikomaa anaota km mabawa hivi mkiani asee km sio kuzimia ni kudata
Sasa umemsaidia nn hapo km sio blabla tu!!!!
 
Wacha tu wakung'ate we kwanini uwachokoze kwa kuingilia makazi yao? [emoji30] [emoji30] ila mdau hapo juu kakushauri vyema ni kweli sio wadudu korofi ila akikupiga pini sumu yake ni hatari ni vyema ukachukua tahadhari mapema kwa kufanya fumigation na kuziba sehemu zenye nyufa ndani na pembezoni mwa nyumba kwani ndiko hasa wanakofanya makazi...
Hv humu watu hawajui Kiswahili au ni kulazimisha kuonesha unajua sana bila kulenga shida ya mleta mada??!! Mtu ameshaumwa tayari, anachoomba hapa ni jinsi ya kujiweka sslama na sumu ambayo tyr ipo mwilini. Fumigation inahusikaje hapa??? Asggh... Mnaboa sometimes.
 
Dawa yake uking’atwa na tandu chukua nyanya ikamulie kwenye jeraha au uchanje na kiwembe kwenye jeraha kisha kamuliapo hiyo nyanya yale maji maji ya nyanya dakika 10 mingi sana maumivu kwisha na yanaathiri nguvu ya ile sumu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom