Msaada: Bata wanataga sehemu moja

jeipm

JF-Expert Member
Sep 28, 2018
500
820
Hawa bata ni wa ukoo mmoja na ndo Mara ya kwanza wao kutaga ila tatizo wanataga wote sehemu moja.

Nimejaribu kumtenga mmoja kwa kumfunika, na kila nikimfunika sehemu tofauti hatagi hiyo sehemu, ukimfunua anaenda kutaga sehemu ile ile ya mwenzake.

Kitu gani wadau naweza kufanya ili kuwatenganisha hawa bata maji?
 
Mkuu fanya iv nenda kazibe pale wanapo tagia alafu chukua yai weka sehemu unayo itaka wewe kama chambo baada ya siku kadha kila mmoja atakuwa na sehemu yake ya kutaga lakini kama mayai yao unatumia kwa biashara mbona akuna shida yoyote ile Mkuu
 
Mkuu fanya iv nenda kazibe pale wanapo tagia alafu chukua yai weka sehemu unayo itaka ww kama chambo baada ya siku kadha kila mmoja atakuwa na sehemu yake ya kutaga lkn kama mayai yao unatumia kwa biashara mbona akuna shida yoyote ile Mkuu
Nasikiaga ana tabia ya kuzira mayai au hata kutotaga kabisa kama kuna MTU au adui anayemtatiza wakati wa utagaji
 
Pole mkuu wanasumbua sana,iliwahi kunitokea,inafika mpaka mahali wanagombea kutagia sehemu hiyohiyo wakati kulikuwa na matundu kama sita,hata ukichukuwa mayai ukasamabaza kwenye matundu mengine wanataka hapohapo,nilichokuwa nafanya niliamua kuwaacha ila ikifika jioni nilikuwa naenda kuchukuwa mayai nawaachia moja,mpk ilipofikia wakati wa kulalia ndio nikaanza kuyagawa kwenye matundu mengine...
 
Mkuu fanya iv nenda kazibe pale wanapo tagia alafu chukua yai weka sehemu unayo itaka ww kama chambo baada ya siku kadha kila mmoja atakuwa na sehemu yake ya kutaga lkn kama mayai yao unatumia kwa biashara mbona akuna shida yoyote ile Mkuu
Yai atakaloligusa kwa mikono yake lazima litaoza hata kabla halijaanza kuatamiwa, na kuna uwezekano likayaozesha hata na yale mengine yatakayokuja kutagwa baadaye. Mayai yanayotagwa kwa ajili ya kutotolesha vifaranga kwa njia ya asili yakiguswa na binadamu huwa yanaoza
 
Back
Top Bottom