Msaada: Basi luxury la Dar - Tabora

Msaada: Basi luxury la Dar - Tabora

CEYLON

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2012
Posts
314
Reaction score
151
Habari wana jf?

Naomba kujua basi luxury linalofanya safari za Dar-Tabora. Kuna ndugu yangu ana mtoto mchanga anatarajia kusafiri hivi karibuni,sasa ili asafiri comfortably ningependa apande basi zuri.

Kwa anayejua naomba anijulishe.

Natanguliza shukurani zangu kwenu.

Ahsante
 
Mkuu namimi nina safari ya Tabora j3!
Ilikuwa niweke Uzi hapa kuulizia hilo ulilouliza!
Ngoja tusubirie majibu!!!
 
Basi Luxury Tabora? We sema basi lenye nafuu, nani apeleke basi lake la maana porini
 
Chekini na NBS coach nadhani wana buses ambazo ni luxury, namba ya ofisi yao ni 0754384369
 
Hakuna mabasi luxury Dar-Tabora, yote ni siti za Two by three tena ni NBS kwa sababu kutoka Singida pale barabara ni vumbi matajjiri wengi hawapeleki magari mazuri. Kama unaweza panda ndege au panda ya Mwamza then ulale kesho yake ndo uende Tabora
 
Treni mpya ya Jumapili kata first or second class kwa vile una mtoto mchanga.
 
Habari wana jf?
naomba kujua basi luxury linalofanya safari za dar-tabora.kuna ndugu yangu ana mtoto mchanga anatarajia kusafiri hivi karibuni,sasa ili asafiri comfortably ningependa apande basi zuri.kwa anayejua naomba anijulishe.
natanguliza shukurani zangu kwenu.
ahsante

Atapande Zhong Thong za kichina za kwenda Mwanza au Kahama then ashuke Nzega na alale hapo,asbh atapanda Yu tong mpya ya kutoka Mwanza to Urambo ya kampuni ya Allys na itamshusha Tabora,lakini ukisema apate bus zuri la moja kwa moja toka Dar to Tbr atapata yale mabus yetu ya watu wanatembea wanatafuna mahindi na karanga,nipo Nzega hapa kikazi ukipenda tutamsaidia,undugu hutokea hata hapa jf.karibu yake
 
Wiki iliyopita kwa mara ya kwanza nlisafiri kutoka dar kwenda nzega magari yenyewe duu ni noma.
Hiyo nbs ndin kwanza naisikia.
 
Mpandishe NBS atleast lina uafadhali ukilinganisha na mengine.
 
atapande zhong thong za kichina za kwenda mwanza au kahama then ashuke nzega na alale hapo,asbh atapanda yu tong mpya ya kutoka mwanza to urambo ya kampuni ya allys na itamshusha tabora,lakini ukisema apate bus zuri la moja kwa moja toka dar to tbr atapata yale mabus yetu ya watu wanatembea wanatafuna mahindi na karanga,nipo nzega hapa kikazi ukipenda tutamsaidia,undugu hutokea hata hapa jf.karibu yake

haha haaa,mmbavu zangu! But ahsante mkuu
 
Kuna basi jipya luxury linaitwa TABORA MOJA rangi ya kijani ,linapaki na ofisi zao zipo magomeni mapipa karibu na hotel ya jangwani.Nenda mkuu ukawasiliane nao.
 
Back
Top Bottom