Dar es Salaam ni jiji la kitalii?

Dar es Salaam ni jiji la kitalii?

Joined
Jul 6, 2023
Posts
40
Reaction score
84
Binafsi sioni kama Dar es Salaam ni jiji la kitalii!

Nilijaribu ku- search kupitia Google " Je, Dar es Salaam ni salama kwa watalii?"

Majibu yakaja " Kuwa mwangalifu kwa mazingira yako na uangalie kwa karibu usalama wako wa kibinafsi. Unyang'anyi wa kutumia silaha, wizi mdogo mdogo na vitisho vya vurugu ni mambo ya kawaida nchini Tanzania, hasa jijini Dar es Salaam. Kuwa mwangalifu zaidi ndani na karibu na Arusha kaskazini mwa Tanzania. Ujambazi wa kutumia silaha, utekaji nyara wa magari na uvamizi wa nyumbani umetokea."

Lakini nahisi labda Google wanapaswa kubadilisha mtazamo huu. Bila shaka hayo ni majibu ya Dar es salaam ya zamani na Arusha iliyopita na siyo sasa.

Turudi kwenye lengo kuu la mada hii, wote tunajua kuwa Dar es Salaam ni jiji la kibiashara. Lakini kwanini lisiwe jiji la kibiashara na kitalii? Achana na utalii uliopo sasa, kwa sasa sioni kama kuna miundombinu sahihi inayoweza kumtoa mtalii wa ndani kutoka Bukoba kuja kwaajiri ya utalii tu pekee hapa Dar es Salaam. Au mtalii kutoka Ulaya kuja Tanzania kwaajiri ya kufanya utalii katika jiji la Dar es salaam pekee na kurudi kwao. Hii ni ngumu sana kutokea kwa mtu anayejua thamani ya pesa na muda wake.

Hitimisho: Kwanini kusifanyike mambo haya yafuatayo ili kuleta mabadiliko na kulifanya jiji la Dar es salaam kuwa jiji la kibiashara na kitalii kweli kweli.

Baada ya kumaliza mradi mpya wa mwendo kasi, ingependeza sana sehemu yote ya mjini kati ya Dar es salaam, kuwekwa paving kila sehemu ya Watembea kwa miguu, pembezoni mwa barabara zote na maeneo yote ya wazi yawekwe square paving na kuondoa kabisa mwonekano wa mchanga na majani yaotayo ovyo katikati ya jiji, tuachane na utaratibu wa kupanda nyasi pembezoni mwa barabara maana tumekuwa tukishindwa kuzitunza , tatizo la kujaa maji lizingatiwe hasa wakati huu wa ujenzi wa barabara nyingi mjini.

Pia baadhi ya kuta na majengo yaliyopo pembezoni mwa barabara yanaweza kuchorwa kwa ustadi picha zinazoangazia taifa letu kuanzia enzi za uhuru hadi sasa na ingekuwa muhimu zaidi kuongeza ishara za sanamu za waasisi wetu na watu mashuhuri waliofanya vizuri katika historia ya Tanzania, mfano kujenga sanamu ya shaba ya bibi titi mohamedi pale kwenye makutano ya barabara iliyopewa jina lake, ingeongeza nafasi ya utalii wa jiji zaidi kwa kuchora michoro mbali mbali ya maeneo maarufu hapa Tanzania juu ya mapaa yote ya vituo vya mwendo kasi, ikiwa pamoja na bendera ya Tanzania, magari yote ya mwendo kasi yenye ruti ya kupitia air port yawe tofauti kwa rangi na yenye maandishi ya welcom Tanzania, karibu Tanzania na lugha nyingine huku yakiambatana na rangi zinazoonyesha bendera ya Tanzania nk, kwanini kusiwe na bango kubwa lenye maneno I Love Dar es salaam na likawa sehemu ya wazi ya jiji ambapo watu wataweza kufika hapo na kulipa pesa kidogo kwaajiri ya kupata picha za kumbukumbu? Huku eneo hilo kukiwekwa mfano wa ramani kubwa ya jiji yenye majengo yanayopatikana mjini?

Liwe jiji la kitalii almashauri ya jiji iweke mpango wa kutangaza na kuweka utaratibu wa watu wageni na wenyeji kusimama na kulipia kupiga picha katika sanamu ya Askali nembo ya jiji la Dar es Salaam, maana sioni sababu ngumu kuzuia jambo hilo.

Ukanda wote wa pembezoni mwa bahari, uelekeo wa kwenda kupanda kivuko kuelekea Kigamboni kuwekwe mabango ya vioo yenye kutoa mwanga usiku na kuonyesha picha za machifu wetu, historia zao, picha za waasisi wetu, picha za wanamichezo wetu maarufu, picha zinazoonesha orodha ya majina ya mashujaa wa vita ya kagera, vita ya kwanza na ya pili ya Dunia, picha za maneno ya majina ya koo mbalimbali zinazopatikana Tanzania.

Jengo jipya la soko kuu la kariakoo liwe na uwezo wa kuwaka taa zinazoonyesha bendera ya Tanzania kwa nyakati za usiku hasa kwenye matukio na siku maalumu za kitaifa na acheni chumba kimoja maalumu kwaajiri ya makumbusho ndogo ya soko hilo kongwe ambapo watu wataweza kutembelea hapo kufanya manunuzi na kuona historia pana na mwanzo wa soko la kariakoo.

Inapendeza kama nyumba zote za (National housing) zingepakwa ranga mpya na nyumba chakavu kuboreshwa na kupendezesha mji.

Eneo lote la mnazi mmoja ni eneo la wazi lakini, kwa sasa halina kazi yoyote zaidi ya kufanyia mikutano na matukio ya kitaifa kwa nyakati chache. Pale kwenye mnara wa mashujaa kuwekwe utaratibu wa watu kutembelea hapo na kupata picha nzuri za kumbukumbu na pia kuwepo na watu maalumu wa kuwapa historia ya matukio kuhusu mnala ule. Hii sio ya kuacha eneo hilo linaweza kuboreshwa zaidi na kuwekwa miundombinu itakayoruhusu watu kukaa hapo na kupumzika.

Kwanini tusiwe na Forodhani mpya ndani ya Dar es salaam? Nitawoonyesha eneo hapa. Ukiwa unavuka na pantoni kuelekea kigamboni , upande wako wa kulia , ile sehemu yenye parking ya mitumbi ya wavuvi ni eneo sahihi kabisa la kuitengeneza Forodhani ya Dar es salaam ambapo mtalii wa ndani na nje atapata fursa na nafasi nzuri ya kushuhudia meli kubwa na ndogo zikiingia bandari ya salama huku upande wa pili akijionea soko kuu la kimataifa la samaki na majengo marefu ya jiji la Dar es salaam. Tuwe wabunifu kidogo tu. Sioni sababu yoyote ngumu kiusalama au kimwonekano.

Ukiwa unatokea Zanzibar, wakati boti inaingia Bandarini utaanza kuona majengo marefu kuanzia mbali. Sasa kwanini lile jengo la bandari lisiwekewe bango kuubwaa na la kibunifu likiandikwa Karibu Dar es salaam mji mkubwa wa kibiashara na kitalii Tanzania?

Mabango makubwa ya kidigitali mfano lile bango kubwa zaidi Dar es salaam linalopatikana eneo la mnazi mmoja, kwanini lisiwekewe matangazo ya kuwahamasisha watanzania kutembelea vivutio vyao? Lionyeshe maeneo mbali mbali ya jiji ambayo ni muhimu mkaazi kutembelea huko hasa siku za weekend, litangaze fukwe zetu, majengo ya kihistoria yaliyopo Dar es salaam, makumbusho, picha za wakaazi na kuhamasisha watu kutunza mazingira na usafi wa jiji kwa moyo wote.

Tutengeneze Nyerere square nyingine hapa Dar es salaam, si mnaona ile ya makao makuu ya nchi inavyopendezesha jiji? Basi kuwe na sehemu kama ile, na sanamu ya baba wa taifa kama ile na eneo lifanane kwa muonekano na hata jina la eneo.

Kungekuwa na uwezekano wa jengo moja refu zaidi lijengewe sehemu maalumu ambayo mtalii wa ndani na nje anaweza kupanda juu kabisa na kuona sehemu kubwa ya jiji la Dar es salaam kwa macho yake kwa kulipia kiasi kidogo cha fedha, na kujiwekea historia yake ya kusimama juu ya jengo refu zaidi Tanzania?

Kuna baadhi ya madaraja ni ya muda mrefu, mfano daraja la Selandar, pale kuwekwe bango zuri la kitalii linaloelezea historia ya daraja hilo tangu kuanza kujengwa kwake, picha zake za zamani, makanisa yote makongwe pale mjini yawekewe utaratibu maarumu na vyumba vya makumbusho ndogo vitakavyoruhusu watu kutembelea na kuona historia ya majengo hayo na vivyo hivyo kila eneo lenye historia muhimu kwa Taifa liwekewe mtindo huo wa maelezo kwa lugha tatu kubwa Duniani ikiwemo na kiswahili.

Kuongezwe utalii wa kuruka na parachute, hasa sehemu za fukwe maarufu na kuweka utaratibu wa safari nafuu zaidi za watalii wa ndani kutembelea visiwa vya Dar es salaam kila mwisho wa wiki na kujionea utajiri wa jiji Lao huko.

Najua kuna mengi mnapaswa kuongezea hapa ndugu zangu watanzania, kazi kwenu sasa na tukianza na mambo haya machache tunaweza kuleta mabadiliko na kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje na kufanya Dar es salaam kuwa moja wapo ya mji unaotembelewa sana Afrika.

#allabouttanzanialife 🔴🟠⚪️
 
Ili kufanikisha yote hayo serikali itahitaji almost tilioni 5 kitu ambacho serikali ya ccm hawawezi kufanya bora watumie billion 50 kuwalipa wasanii wafanye propaganda na kuwaaminisha watanzania mambo yapo poa
 
Sina uhakika mkuu, ila km una line ya tigo 👇🏻

Kwa watumiaji wa Tigo Pata GB za bure kwa kufuta maelekezo haya.



1. Ingia TigoPesa app (Kama hauna download play store)

2. Ingia Invite & Earn

3. Bonyeza Redeem

4. Weka hii code 2ZJVO8ZK

Baada ya hapo utapata 2GB na DK kibao bure kabisa!!
 
Kwanza hongera sana una mawazo mazuri na fikra nzuri na tunaendana kwa mitizamo flani.

Ni kweli kuna fursa kubwa mno ya kufanya utalii jijini Dar ila watu hawalijua hilo kikamilifu.

Pia wapo watu wachache kutoka ndani na nje ya nchi wanafika Dar kwa utalii tu. Kikwazo kikubwa Dar kutokuwa jiji la utalii ni miundombinu mibovu na finyu. Mabarabara tumeanza kuyajenga hivi karibuni.

Kwa kifupi hata ule mji wetu wa kitalii Arusha bado hatujaweza kufanya la maana kuuboresha uwe mji wa kitalii kweli.

Mwisho mapungufu hayo yote ni fursa kwako, changamkia fursa hizo.
 
Kwanza hongera sana una mawazo mazuri na fikra nzuri na tunaendana kwa mitizamo flani.

Ni kweli kuna fursa kubwa mno ya kufanya utalii jijini Dar ila watu hawalijua hilo kikamilifu.

Pia wapo watu wachache kutoka ndani na nje ya nchi wanafika Dar kwa utalii tu. Kikwazo kikubwa Dar kutokuwa jiji la utalii ni miundombinu mibovu na finyu. Mabarabara tumeanza kuyajenga hivi karibuni.

Kwa kifupi hata ule mji wetu wa kitalii Arusha bado hatujaweza kufanya la maana kuuboresha uwe mji wa kitalii kweli.

Mwisho mapungufu hayo yote ni fursa kwako, changamkia fursa hizo.
Fursa kwangu🤔 umenipa changamoto nzuri.
 
Back
Top Bottom