Msaada baada ya mimba kutoka

mahirtwahir

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
613
311
Mubarikiwe nyote
Nisaidieni kwa anaejua mke wangu hua anakawaida ya kupunguzia akiwa na mimba (hua anapata hedhi japo kidogo) sasa katika mimba hii naona imekua nno yaani ametoka damu nyingi zaidi ya siku zake za kawaida baada ya kuenda hospital tukaambiwa mimba imechoropoka labda ka kazi ngumu ama sababu nyengine.
Kwa sababu ya maumivu makali ikabidi tupige Ultrasound ikabainika kua anauchafu katika fuko lake la uzazi (incomplete Abortion) tukashauriwa asafishe.

Tatizo amegoma kabisa kusafishwa anasema anaogopa maana kasikia inauma sana pia anasema kuangaliwa uchi wake na mtu mwengie haiwezekani.

Naombeni dawa ya kuweza kusafisha ili atumie maaana ameshapoteza damu nyingi.
 
Huo uchafu utakuwa unamsababishia maumivu makali, dawa ni kusafisha na huwa hawatumii ganzi. Ukitoka tu kwenye kitanda cha theatre vunaweza hata kukimbia marathon.
Eti anasema kuna chuma linaitwa mdomo wa bata unaingizwa nacho kwa ajili sijui kama ya kutanuliwa hilo nalo pia analiogopa na daktari ni wa kiume pia ni shida ya pili eti anaona aibu kumuonesha papuchi.
 
Uzima wake una umuhimu mkubwa kuliko aibu ya dakika chache za kuonwa papuchi yake na atakayemsafisha pia kutosafishwa inaweza kabisa kuwa chanzo cha madhara makubwa ikiwemo kutokupata ujauzito tena.

Eti anasema kuna chuma linaitwa mdomo wa bata unaingizwa nacho kwa ajili sijui kama ya kutanuliwa hilo nalo pia analiogopa na daktari ni wa kiume pia ni shida ya pili eti anaona aibu kumuonesha papuchi.
 
Eti anasema kuna chuma linaitwa mdomo wa bata unaingizwa nacho kwa ajili sijui kama ya kutanuliwa hilo nalo pia analiogopa na daktari ni wa kiume pia ni shida ya pili eti anaona aibu kumuonesha papuchi.
Avumilie tu jamani iaijemdhuru tu
 
Huyo mdomo wa bata unafanya kazi kama jerk ya gari, , unapandishwa mpaka daktari apate njia ya kufanyia kazi.

Mkienda private hospital mnaweza kuomba huduma ya daktari wa kike na wewe unaweza kuomba umshike mkono katika process nzima ili kumpa assurance.
 
Avumilie tu jamani iaijemdhuru tu
Usiku wa kuamkia leo ametoka kitu kama cha ajabu hivi naomba niweke picha
IMG-20180322-WA0022.jpg
 
Mubarikiwe nyote
Nisaidieni kwa anaejua mke wangu hua anakawaida ya kupunguzia akiwa na mimba (hua anapata hedhi japo kidogo) sasa katika mimba hii naona imekua nno yaani ametoka damu nyingi zaidi ya siku zake za kawaida baada ya kuenda hospital tukaambiwa mimba imechoropoka labda ka kazi ngumu ama sababu nyengine.
Kwa sababu ya maumivu makali ikabidi tupige Ultrasound ikabainika kua anauchafu katika fuko lake la uzazi (incomplete Abortion) tukashauriwa asafishe.

Tatizo amegoma kabisa kusafishwa anasema anaogopa maana kasikia inauma sana pia anasema kuangaliwa uchi wake na mtu mwengie haiwezekani.

Naombeni dawa ya kuweza kusafisha ili atumie maaana ameshapoteza damu nyingi.
Akasafishwe haraka iwezekanavyo.

Kwani mimba isingetoka asingezalishwa na mtu? Kama ndio anaogopa kuangaliwa tupu yake.
 
Optionaly nenda pharmacy kwa dr. Ambaye ni rafiki yako mnayeshibana sana. Huwa kuna vidonge vinauzwa elf 30 kama sikosei mm nlivitumia kwa mschana wanagu alitoa mimba haikutoka yote. Mwambie akununulie hiyo dawa. Dam itatoka kwa mabonge na baada ya wiki moja atakaa sawa. Vidonge hivi vinauzwa kama madawa ya kulevya anayekuuzia lazima awe anakufahamu
 
Pia kwa vile kuna prolonged bleeding namshauri anywe antibiotic kama amoxylin na flagyl kwa siku saba. Ili kuzuia infection la sivyo atapata matatizo makubwa sana. Ila zingatia sana misoprostol lazima ipatikane, hiyo ndo mwisha wa matatizo
 
Unatumiaje hio misoprostol?
 
Bora tu akasafishwe kwa uhakika Na usalama zaidi akumbuke hayo ndo maisha yake . Na asiposafishwa ataendelea tu kubleed ambayo ni shida Na pia anaweza pata uvimbe kwenye kizazi Na kupelekea kansa kwa hiyo aweke aibu pembeni asafishwe
 
Eti anasema kuna chuma linaitwa mdomo wa bata unaingizwa nacho kwa ajili sijui kama ya kutanuliwa hilo nalo pia analiogopa na daktari ni wa kiume pia ni shida ya pili eti anaona aibu kumuonesha papuchi.
Mkuu amelijua hilo chuma si ndiyo?

Ama ameabort mwenyewe au amesikiliza stori za jikoni.
 
Back
Top Bottom