Msaada anaejua gharama za kupima kiwanja na kuweka bikoni

Isaack Newton

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
535
224
Habari wakuu,

Nina kiwanja changu cha cha 20 kwa 30 ambacho hakijapimwa, kipo level kabisa maeneo ya tegeta-Dar es salaam, sasa nataka nikipime niweke na bikoni, mwenye uelewa kuhusu gharama za kupima huwa zinakuwaje anifahamishe.
 
Habari wakuu, nina kiwanja changu cha cha 20 kwa 30 ambacho hakijapimwa, kipo level kabisa maeneo ya tegeta-Dar es salaam, sasa nataka nikipime niweke na bikoni, mwenye uelewa kuhusu gharama za kupima huwa zinakuwaje anifahamishe.
Gharama inategemea jambo moja kubwa. Eneo limepangwa, kwa maana ya kuwa na mpango wa matumizi Bora ya Ardhi (AKA town planning drawing).. maana hatua hii ni lazima uwe imefanyika ili eneo lifae kwa upimaji

1) kama kumepangwa gharama za upimaji zitarange kutoka 150k kwamaeneo mnayopima kuwa kishirikiana kama jumuiya (almaarufu URASIMISHAJI), hadi kati ya 1m na 2m kwa maeneo unayoamua kufanya/kugharamia mwenyewe na pia kwa kulingana na mtaalamu utakayeonana naye na namna mtavyozingumza.

2) ikiwa hakuna mpango is a whole new story. Maana utalazimika kugharamia zoezi la kuandaa mpango wa matumizi Bora ya Ardhi juu ya gharama za kupima. Na gharama za maandalizi au marekebisho ya mpango wa matumizi huwa kati 1.5m mpaka 3m na kuendelea kulingana na aina ya changamoto za mpango zitakazobainika na kutishia kukwama kwa ziezi.

Usiku mwema. Stay Planned.
 
Back
Top Bottom