Mrithi ajitokeze


B

Badourah

Member
Joined
Jun 10, 2012
Messages
68
Points
0
Age
62
B

Badourah

Member
Joined Jun 10, 2012
68 0
Miaka mitatu iliyopita kuna mwanamke mmoja mfanya biashara, alifikia nyumbani kwetu akitokea kwenye biashara zake, alikuwa akifikia kwetu mara kwa mara kwani aliwahi kusoma chuo cha tiba na dadangu na walikuwa marafiki, ingawa dadangu huyo kwa muda mrefu sasa anaishi nje ya nchi lakini huyu rafiki yake ilikuwa ni mazowea yake kufikia kwetu toka enzi za chuo na mwenzake.

Kwa kifupi, mara ya mwisho kufikia kwetu aliacha suitcase yake na kusema anaenda Zanzibar atarudi baada ya siku 3. Kwa bahati nzuri au mbaya, huyu dada hajarudi mpaka leo, na wiki mbili zilizopita, tukaamuwa kulifunguwa lile suitcase lake, jamani, tulichokuta humo hakisemeki...

Euro 259,000 taslim, US dollars 56,000 taslim na unga-unga mweupe kilo mbili na nusu, ambao baadae tulijuwa kuwa ni cocaine, imewekwa kwenye vifuko vya plastic vya gram 500 vitano.

Huyu dada kwao ni Mwanza na katika kuulizia kwa dadangu ambae ni rafiki yake, akasema huyo dada kwao ni Mwanza na ana ndugu zake kule, wazee wake walishafariki zamani na alipofika chuo akaanza maisha ya mjini, masomo yakamshinda na hakurudi tena huko Mwanza.

Jamani, Kama kuna mtu anamjua huyu dada yuko wapi, ajitokeze, anaitwa Angelina, ukimuona ni mrefu, ana umbo kubwa la Kinyamwezi, lakini mwenyewe ni chotara wa aina fulani ana damu mchanganyiko na anapenda kutabasamu saa zote, si muongezi sana na hana marafiki niwajuao hapa Dar. Kama alikuwa nao, basi ni siri yake.

Kama kuna nduguye au amjuae yeye au ndugu zake, tuwasiliane. Mpaka sasa nimekopa dollar 6,000 tu katika hiyo suitcase, kumalizia vishida vya hapa na pale.
 
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Messages
18,159
Points
2,000
charminglady

charminglady

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2012
18,159 2,000
we kula zote huenda kashafariki.... kama vp peleka police central
 
Kaizer

Kaizer

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2008
Messages
25,167
Points
2,000
Kaizer

Kaizer

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2008
25,167 2,000
He umekaa na bomu hebu weka contact zako hapa tuje kurithi
 
nitonye

nitonye

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2011
Messages
7,184
Points
2,000
nitonye

nitonye

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2011
7,184 2,000
nitamtuma bishanga umpatie huo mzigo maana ni kijana wangu aliuacha hapo
 
B

Badourah

Member
Joined
Jun 10, 2012
Messages
68
Points
0
Age
62
B

Badourah

Member
Joined Jun 10, 2012
68 0
we kula zote huenda kashafariki.... kama vp peleka police central
Polisi sipeleki, nimeileta humu nisije nikahisi sijafanya effort yeyote kumtafuta mwenyewe, baada ya wiki mbili Inabidi nitafute kiwanja.
 
St. Paka Mweusi

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2010
Messages
7,320
Points
2,000
St. Paka Mweusi

St. Paka Mweusi

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2010
7,320 2,000
we kula zote huenda kashafariki.... kama vp peleka police central

Red: ushauri mzuri japo anaweza kuja kutakiwa kujibu siku ya hukumu kama itakuwepo..
Blue: Hapo unamuingiza chaka,maana akizifikisha tu kituoni jamaa watamdunda kama
mbwa koko na kuna uwezekano wa kumbambikia kesi ya ujambazi ili wamzulumu
vizuri hizo pesa..
 
Nicole

Nicole

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2012
Messages
4,282
Points
0
Nicole

Nicole

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2012
4,282 0
Huenda alikamatwa ama hatunaye huo unga udispose toilet pesa zibadil kwa madafu then anzisha business ya kisela huwezi jua ndo ntoke vip umeletewa kwa mlango
Watu wa Kaskazini utawajuwa tu.
 

Forum statistics

Threads 1,284,371
Members 494,064
Posts 30,822,998
Top