Mrema wa TANROADS Kikaangoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mrema wa TANROADS Kikaangoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkaa Mweupe, Jun 2, 2010.

 1. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inasemekana kwamba Mtendaji Mkuu wa TANROADS Ephraem Mrema yupo katika wakati mgumu ambapo atamaliza muda wake kesho tarehe 3 June 2010.

  Habari zilizopatikana katika gazeti la Tanzania Daima zimeeleza kuwa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) wanamsubiri kwa hamu ili aweze kujibu tuhuma zake.

  Tuhuma zinazomkabili ni pamoja na ufujaji wa fedha, matumizi mabaya ya madaraka na uongozi mbaya. Inasemekana kuwa aliteuliwa na aliyekuwa waziri wa miundombinu Chenge.

  SOURCE: Tanzania Daima

  Kwa msaada wa JF member Halisi naambatanisha na ushahidi kwa chini:

  [​IMG]
  [​IMG]

  na

  [​IMG]
   
 2. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni utumbo mtupu, yale yale mambo ya kitanzania ya kilofa. Kuna mantiki gani kumngoja mtu achezee raslimali za nchi na madaraka aliyokabidhiwa kwa muda woooote mpaka mwisho wa mkataba ndio ujifanye unamhoji? Hakuna lolote la maana hapo. Mtu anapokosea awajibishwe hapo hapo badala ya kungoja mwisho wa maisha yake na huku wananchi wanateseka.

  Mfumo wa uwajibishaji unatakiwa uanzie ngazi ya juu kabisa serikalini (kwa rais). Kama rais mwenyewe anachezea raslimali za nchi na madaraka yake kiasi hicho na hachukuliwi hatua kuna haki gani kuwachukulia hatua wa chini yake?
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huo ni mchango wa msanii Hosea wa kampeni ya uchaguzi wa CCM. Tutaona usanii mwingi tu wa huyo bwana hadi siku ya uchaguzi.
   
 4. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #4
  Jun 2, 2010
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Yetu macho na masikio....,...
   
 5. K

  Keil JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tukirudi kwenye ujinga wa PCCB, hivi kwanini huwa wanasubiri mtu astaafu kwanza ndipo wampeleke mahakamani?

  Liyumba kama angeshitakiwa kabla ya kustaafu, angefukuzwa kazi na wala asingepewa mafao (terminal benefits) baada ya kuhukumiwa kifungo.

  Mgonja, wamemsubiri kastaafu na kavuta mafao yake ndio wakaja kumpeleka mahakamani. Hivi nikisema kwamba huu ni usanii na kwamba hao wanaohukumiwa kifungo ni kwamba wanafungwa kwa bahati mbaya tu, nitakuwa nimekosea?

  Kwanini PCCB wasimshike na kumshitaki wakati akiwa bado yuko kazini? Halafu wanasema wazi ili kum-alert kwamba fukia mashimo yote maana ukiondoka tu tunakuja kukuchunguza na kukupeleka mahakamani. Kama walishachunguza na uchunguzi umekamilika na wakaona ana makosa, kwanini wasubiri mpaka baada ya kustaafu?
   
 6. W

  WAMURUBHERE JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2010
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  tulikwisha sema wakati huu wa uchaguzi tutaona mengi,lini mtuhumiwa akasubiriwa astaafu apate kiinua mgongo chake then ndo ahojiwe kujibu tuhuma! Doctorate nyingine hizi taabu kwelikweli!
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Labda Sheria ya Kuzuia Rushwa ya 2007 inasema hivyo -- kwamba mtuhumiwa asihojiwe kwa tuhuma zake za ufisadi hadi hadi hapo atakapoacha kazi!

  Mimi sitashangaa iwapo Sheria inasema hivyo kwa sababu kuna madudu mengi tu katika sheria hiyo: Kwa mfano anayepatikana na hatia aweza kulipishwa faini tu (atatoa kutoka hela alizoiba) , vyombo vya habari visiandike chochote kuhusu kuchunguzwa kwa mtuhumiwa. Lakini yote hayo ni tisa -- kumi ni kwamba katika utangulizi wake wa fasiri (interpretation and general clauses) Sheria hiyo haina definition yoyote ya neno 'corruption.'
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  si ndivyo walivyofanya kwa Mgonja? Ili aondoke na pensheni yake kwanza, kwani akitimuliwa kabla ya mwisho wa mkataba wake anaweza kupoteza vyote alivyofanyia kazi.. that is the reasoning behind..
   
 9. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakerwa sana na staili hii ya kutuhumu watu na kuwalaumu kwa kufuata mkumbo tu. Nchi haitaendeshwa kwa magazeti ya mengi. Kuna vyombo vya kutosha kabisa kusaidia taifa hili likaenda mbele bila ufisadi. Huu ufisadi unaohubiriwa na vyombo vya habari kwa masilahi ya watu na kundi fulani katika nchi yetu mimi nauita upuuzi mtupu.

  Kwa staili hii ya kuwatuhumu watu wanaolitumikia taifa bila ushahidi wowote, tunatengeneza utamaduni mbaya sana. Leo nikikuchukia na kama nina mahusiano mazuri na wenye vyombo vya habari basi kazi ya kukumaliza inakuwa rahisi sana.

  Wangapi wanachafuliwa majina yao na haya magazeti yenye dhamira na maslahi ya wamiliki. Dr Rashidi kaandikwa wee, lakini huyu ni mmoja wa watu waliokuwa wanadhamira ya dhati ya kuliendesha shirika la umeme kwa mafanikio. Mrema kaandikwa wee, lakini haondolewi kwenye nafasi sasa maana yake nini?

  Tuache tabia ya kuharibiana na kushadidia mambo ambayo hatujui kichwa wala miguu.
   
 10. K

  Kagasheki Member

  #10
  Jun 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachotushangaza wengi ni kuwa na jeuri kushinda mamlaka zilizo juu yake kiutawala kufikia hatua ya kutokumsikiliza Waziri na Katibu Mkuu wake.Huyu bwana amekuwa Mungu mtu kwenye taasisi hiyo na ndio maaana miradi mingi ya barabara imekwama kwenye kipindi chake.Bado tunahoji mamlaka zilizohusika na mchakato wa uteuzi wake
   
 11. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Unamaanisha kama zile kesi zilizoandaliwa serikali ishindwe? anyway tulishaona hizo kuanzia kwa akina Naila Kiula na hata mshikaji Liyumba lazima atashinda rufaa yake na utaambiwa kuwa ni uhuru wa mahakama,
   
 12. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  USANII KILA KONA
  Sasa wakimsubiri ndo nini ili atokee kwake afu aseme ..doc hizo sina ziko ofisini na mimi nimestaafu/mkataba umeisha...
  Kitakachoendelea ndo senema ya sasa ya akina Yona na wenzie
  Rubish..... Wanaharibu taaluma zao kwa kuchumia tumbo
  Heshima kwa mtanzania inapotea kwa staili hii ya utendaji...
  Waamue moja kuwasiriaz na kazi au wale bata kama kawaida
  TAKUKURU ZIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Suala hili sio uzushi hata kidogo, very solemn.
  Kana unafuatilia Raia Mwema, walianza kipindi kidogo kuchimba habari hizi, na sasa wanaelekea ukingoni kutoa ripoti kamili.
  Ila kwa kadri nilivyosoma hizo makala, Mrema Efraem analaumiwa kwa kukiuka kanuni za manunuzi, kutofuata maelekezo na ushauri wa wakala wa manunuzi wa serikali (PPRA) katika kutoa zabuni za ujenzi wa barabara na manunuzi mengine ya Tanroads. Kuna tuhuma nyingine kibao pia.
   
 14. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Gazeti ni Tanzania Daima na si Mtanzania Daima kama nilivyoandika mwanzo.

   
 15. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama kuna tuhuma za uongo kwenye gazeti, aliyetuhumiwa na asimame atueleze ukweli. Kama PCCB wanasemewa na magazeti isivyo kweli na wakakaa kimya basi wameridhia. Ukweli wa tuhuma ni swala lingine, ila linalotukera zaidi ni ukweli usiopingika kuwa kuna utamaduni unaowaruhusu wenye mamlaka kutenda watakavyo na hawachukuliwi hatua yoyote hata kama matendo yao yanajulikana hadharani.

  Mimi nakerwa na kukaa barabarani masaa, kutolala ili niwahi kukaa barabarani kungoja foleni, kukosa maji, umeme, huduma za afya, shuleni walimu matatizo.... yaani listi ni ndefu mno na huku hela zetu zikitumika bila mpangilio. Safari zisizo na maana kila kukicha, mikutano, magari ya bei mbaya, nk nk. Nashangaa bado serikali iko madarakani eti mpaka imalize mkataba na sidhani kama itahojiwa!

   
 16. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2010
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Lakini Tanzania Daima sio gazeti la Mengi. Halafu mbona unaonekana una hasira sana na taarifa hizi? Zimekugusa enh?
   
 17. K

  Keil JF-Expert Member

  #17
  Jun 2, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Chanzo cha habari siyo Gazeti la Mengi. Umeambiwa ni Tanzania Daima inayomilikiwa na Freeman Mbowe. Pia kwa kuongezea tu, Raia Mwema wameandika sana kuhusu hili swala la Mrema mpaka waki-quote barua za Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundo Mbinu. Sasa kipi ambacho ni uzushi? Kama ingekuwa ni uzushi, Katibu Mkuu wa Wizara angemtaka Mrema ajieleze kwanini alifanya maamuzi bila kuishirikisha Wizara?

  Wewe ndiyo unasema kwamba hakuna ushahidi, lakini ushahidi upo. Tatizo ni kwamba serikali yetu kwa kushirikiana na vyombo vya dola wamekuwa wakifunika ushahidi ili kesi zisiende mahakamani. Hata pale ambapo pana ushahidi wa wazi kabisa, tumeshuhudia mambo yakiachwa kama yalivyo. Chenge aliishia kujiuzulu, kama alikuwa anazushiwa ilikuwaje akakubali kujiuzulu? Kesi yake mpaka leo imedoda na hakuna kinachoendelea na bado wewe unataka tuamini kwamba ni uzushi?

  Kama wanaona kwamba wanachafuliwa majina yao, si waende mahakamani kudai haki. Sumaye alichafuliwa na wanamtandao kwa kutumia gazeti flani hivi, alipoenda mahakamani gazeti liliamuliwa kumlipa fidia. Kama mtu anachafuliwa jina, njia iko wazi kwenda mahakamani kudai haki. Nani ambaye yuko tayari kuchafuliwa jina lake ili kuharibu career yake ama credibility yake?

  Tatizo nimeishalisema hapo juu, serikali yetu kwa kushirikiana na vyombo vya dola wamekuwa wakiangalia ni nani apelekwe mahakani na yupi ushahidi wake uchimbuliwe kiasi kwamba akienda mahakamani akose upenyo wa kupona.

  Kesi za EPA ushahidi uko wazi, lakini ni kampuni chache ambazo zimefikishwa mahakamani. Akina Malegesi wanaendelea kudunda mtaani na hawajapelekwa mahakamani na hata waliopelekwa mahakamani utashangaa mwisho wa siku wanaachiwa kwa kigezo kwamba hakuna ushahidi ama upande wa mashitaka umeshindwa kuwatia hatiani.

  Hukumu ya Liyumba imetolewa na pande mbili, hakimu mmoja kamuona hana hatia, mahakimu wengine 2 wanasema ana hatia. Liyumba alishasukuma mzigo kwa Ballali, na ni wazi Liyumba alikuwa chini ya Ballali hivyo asingefanya maamuzi yoyote bila ya maelekezo ya Ballali. Ukiwauliza PCCB walikuwa wapi wasimhoji Ballali akiwa hai ili wawe mashitaka ambayo ni concrete? Wanasubiri mhusika mkuu anapoteza maisha ndipo wanakuja kupeleka kesi mahakamani. Kesi ikikosa maelezo ya mhusika mkuu, nguvu ya mashitaka inapungua. Liyumba alipofungwa miaka 2, serikali na wapambe wao wanajisifu kwamba wanawashughulikia mafisadi. Kifungo cha miaka 2 hakiendani na hasara ya pesa zilizozama kwenye ujenzi wa Twin Towers, kama kesi hiyo ingeanza zama za uhai wa Ballali wengi wangeunganishwa na wala Liyumba asingefungwa miaka 2 tu.

  Hii ni siasa na wizi mtupu!
   
 18. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Mimi na pinga ufisadi wa aina yoyote lakini watu wa KILIMANJARO-Kweka,Yona,Mramba,Mgonja na Mrema- ndiyo wao tu waliotumia madaraka yao vibaya?Watu wa sehemu nyingine zaidi ya Liyumba kama Dr rashid, "mzee wa vijisenti" mpaka kwenye magazeti ya nje wameandikwa,Lowassa,Msabaha, Karamagi na wengineo wengi mpaka sasa hakuna aliyesubutu kuwagusa.Wakisha malizana na Mrema waende kule TRA kuna mwingine.
   
 19. Shishye

  Shishye JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wa Tanzania - wakiongozwa na rais wao Kikwete ndio wanaotumia madaraka yao vibaya. Naona hapo kwenye nyekundu unataka kutuanzishia ubaguzi hapa, tafadhali usiende huko.
   
 20. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,993
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Mkuu nia yangu sio kuanzisha ubaguzi,wala sitaki kuamini kama Chenge angekuwa Massawe asingekuwa uraiani.Mafisadi wako lukuki lakini wanashugulikiwa ni wachache tena wa sehemu moja.
   
Loading...