Mrema ampasha Mbowe: Sitaki uwaziri kivuli

Mrema ampasha Mbowe: Sitaki uwaziri kivuli

Hivi hawa mawaziri vivuli huwa wanapewa posho zozote zaidi au ni jina tu?
 
Aiseeee!
Nimewahi kuwa naibu waziri mkuu.
Nimewahi kuwa waziri kamili,teh teh teh
Kwani wewe ni nani kwa sasa Mrema!

BACK TANGANYIKA
 
image.jpg Ameongea yote hayo kutokana na michango hii......
 
Mrema ana akili sana tena huenda zaidi ya hao mnaodhani wanaakili. Ameifanyia nchi mambo mengi yenye faida kwa Taifa hili . Hao akina Mbowe wamefanyia nini Taifa hili
 
Mrema ana akili sana tena huenda zaidi ya hao mnaodhani wanaakili. Ameifanyia nchi mambo mengi yenye faida kwa Taifa hili . Hao akina Mbowe wamefanyia nini Taifa hili

Hii nayo ni point ya muhimu sana. Tatizo hawa vijana hawaelewi historia ya nchi hii.
 
Niaibu aibu kwa Mbowe kusema hata niteua uwaziri kivuli Mbowe alishaa kuwa nani katika nchi hii mm sitaki kuwa kivuli nataka uwaziri kamili

Nimewahi kuwa NAIBU waziri mkuu na waziri Wa mambo ya ndani

Kuniita kibaraka Wa ccm ni kunipaka matope kibaraka Wa ccm ni seifu Wa Zanzibar anayelipwa na ccm mpaka sasa

Chanzo TBC live muda huu

Augustino Mrema 2014???
 
mkuu anachohoji mrema ni kwa nini mbowe aoneshe kuwa na uwezo wa kuteua watu wakati hana sifa ya kuteua watu na kumwita yeye ni kibaraka wa ccm kwanini kibaraka asiwe katibu mkuu wa cuf anayelipwa na serikali ya ccm.

Jibu langu kwa Mrema lingekuwa hili,Mbowe anauwezo wa kuchagua au kuteua kulingana na cheo chake cha KUB kama ndivyo wapinzani walivyojiwekea.Kumbuka yeye ni Waziri Mkuu Kivuli,na anamajumu ya kusimamia yale yanayohusu Kambi ya Upinzani.

Tofauti na CUF pamoja na kwamba anapokea Mshahara toka Serikalini kumbuka Katiba ya Zanzibar inaruhusu alipwe na ni Wanzanzibar walikubaliana hivyo kisheria hapokei mshahara kama favour anapokea kama haki yake ya msingi ya kufanya kazi ya UMAKAMU wa kwanza kama Katiba ya nchi inavyoelekeza.Na kumbuka kwa Zanzibar Serikali si ya CCM ni ya marithiano ya kitaifa,na pia Katibu wa CUF anatoa anachofikiri ni sahihi na kilicho ndani ya akili yake.

Tofauti na Mrema kupata tu huo UBUNGE CCM walimsaidia na majibu au maswali yake Bungeni zaidi si ya kuhoji ila ya kuisifia serikali tu,hakuna kuhoji,na kile wapinzani wakihoji kwa uhalali yeye si sawa.Huyu utamtofautidhaje na Mwanachama wa CCM?

Haya ndiyo yangekuwa majibu yangu kwa Mrema,akitaka kupata heshima ya upinzani aanze kujipambanua siyo kwa kutukana ila kwa kuhoji maovu,na kusifia mazuri.Siyo kila siku imekuwa stori nilikuwa nilikuwa tumeshajua alikuwa sasa kinachofuata awajibike kama mpinzani.
 
Trend yake inazidi kushuka kutoka kugombea Uraisi- Ubunge. sasa itakuwa Udiwani kwa mwaka 2015 akiwa na nguvu bado 2020 Uenyekiti wa mtaa.
 
Naona mmeanza matusi sasa ugonjwa unahusiano gani na uwaziri kivuli hata wewe unaweza kuugua.

Mkuu wewe ni mheshimiwa sasa hivi.

Ni kweli hata mimi naweza kuugua, ila kwa sasa mrema ni mgonjwa na huo ugonjwa unafanya decision impairing
 
Lakini pia katoa maneno makali kidogo kwa mbowe kwa kumwambia kuwa amkome kabisa wala asimfuatefuate.


Amkome? Duu! Kwani mrema amekuwa na uwezo wa kujifungua na kunyonyesha siku hizi? Wazee wengine wanadhalilisha tu mama na dada zetu bure.
 
Haya usubirr huo uwazir kamili nyau wee, hata hujielewi mafao yako yenyewe mpk uyaendee kwa mganga utakufa kwa kutumikia watu burebure
 
Hii nayo ni point ya muhimu sana. Tatizo hawa vijana hawaelewi historia ya nchi hii.

Zile vurugu alifanya Mambo ya Ndani ndiyo mambo makubwa ktk Taifa? Kuhujumu na kusambaratisha Vyama alivyoongoza ni jambo muhimu kwa Watanzania? Sema aliwafanyia kazi nzuri CCM kwa kuhujumu Upinzani kabla ya kustukiwa ni kibaraka wenu!

Nasema ni kibaraka kwasababu hata hiyo TLP hakuna kikao chochote kiliwahi kuketi na kuamua chama chao ni chama rafiki na CCM. Ni yeye binafsi anaye jipendekeza CCM! Vyama vya CDM,CUF na NCCR Mageuzi vimekubaliana kushirikiana,sasa yeye ngebe za nini??
 
Hapo CCM walikuwa wanamchangia pesa za kwenda kuchukua form za ubunge, utumwa aina hii siko tayari.

Sasa badala ya chama chake kumchangia alienda kuomba hela CCM? CCM haohao ndio wamemfikisha hapo alipo kiafya labda hajitambui. Mabomu na sindano alizochomwa enzi hizo vimemlemaza Mh. Sasa anarudi kwa CCM kuwapigia debe. Hapo ni kusema Mrema hajui anatetea nini hapa nchini? Basi asingetoka CCM kwani alipokuwa huko alifanya kazi kwa ufanisi mzuri tu na akaona madudu ndani ya serikali ya CCM ndio sababu akatoka ili akatetee wananchi akiwa nje lakini wapi njaa ilipombana karudi kulekule.

Kwa sasa hivi na ugonjwa wake aachwe apumzike na CCM wamlee hadi siku ya mwisho wake hapa duniani. Ila kama angekuwa na afya angekuwa waziri kivuli angefaa sana maana anajua siri na mbinu zote za CCM!

Cha kumwambia ni kwamba bado wananchi tunanyanyasika vilivyo kila mahali na ndio sababu tunamwomba Mungu Rasimu ya Warioba ipitishwe ili walalahoi angalau wapate huduma za afya na elimu bila rushwa!
 
Niaibu aibu kwa Mbowe kusema hata niteua uwaziri kivuli Mbowe alishaa kuwa nani katika nchi hii mm sitaki kuwa kivuli nataka uwaziri kamili

Nimewahi kuwa NAIBU waziri mkuu na waziri Wa mambo ya ndani

Kuniita kibaraka Wa ccm ni kunipaka matope kibaraka Wa ccm ni seifu Wa Zanzibar anayelipwa na ccm mpaka sasa

Chanzo TBC live muda huu

Sikujua kama TLP ni sehemu ya huo ushirikianowa vyama katika kuhakikisha katiba huru inakidhi matakwa ya wananchi ujulikanao kama UKAWA. Sasa Mrema kukurupuka eti hataki uwaziri kivuli ina uhusiano vipi na huo muungano? By the way Mh. Mrema kishachoka sasa hivi na anahitaji mapumziko ya hali ya juu, but pesa is better kuliko afya yake (kwa mtazamo wake).
 
Jaman nyie mnajisumbua bure kukajadili haka kazee,
Huyo mzee akili zlifyatuka zaman kwasababu ya ule uginjwa wake,
Hapo alipo huwa anapelekwa mirembe kisirisiri, eti kanasema mboye amkome kumfuatafuata,
Amkome?
Nauzee uzee ule mboye amkome au alijua nn?
 
Mrema ni mzee sn Nape aliwah kusema wazee wanakaribia kufa ndo wanapendekeza ......... mtamalizia wenyewe,
Kwa kaul ya Nepi huyo mzee amekaribia kufa,
Si kauli ya ni ya Nepi
Sorry si Nepi ni Nape
 
Huyu mzee nafikiri hata kumjadili ni kupoteza muda. Hao CCM wenyewe wanamdharau ila wanamtumia kipropaganda. Unakumbuka uchaguzi mkuu wa 2010? Kama mwenyekiti wa TLP anasimama kujiombe kura halafu za urais anasema wampe JK na wamuache yule wa TLP. Mtasema yuko timamu kweli huyo?


Sent from my iPad using JamiiForums

Chakaza,
Unamtuhumu Mrema kumpigia kampeni mgombea wa CCM? Basi mtuhumu na Dr. Slaa kumpigia kampeni mgombea wa CCM.

Kule Kyela Dr. Slaa majukwaani alikuwa anampigia kampeni mbunge wa CCM na kumwacha mgombea wao wa CHADEMA.

Tunavyoandika tuwe na kumbukumbu na siasa za Tanzania na sio kukimbilia kuwaita watu eti vibaraka.

Katika wanasiasa ninaowaheshimu nchi hii ni pamoja na Mrema. Ana historia ya kutenda na alipokuwa madarakani alitenda na sio maneno matupu majukwaani.
 
Back
Top Bottom