Mrema ampasha Mbowe: Sitaki uwaziri kivuli

Mrema ampasha Mbowe: Sitaki uwaziri kivuli

Niaibu aibu kwa Mbowe kusema hata niteua uwaziri kivuli Mbowe alishaa kuwa nani katika nchi hii mm sitaki kuwa kivuli nataka uwaziri kamili

Nimewahi kuwa NAIBU waziri mkuu na waziri Wa mambo ya ndani

Kuniita kibaraka Wa ccm ni kunipaka matope kibaraka Wa ccm ni seifu Wa Zanzibar anayelipwa na ccm mpaka sasa

Chanzo TBC live muda huu

Hata akikaa kimya hawezi kupewa. hii ni defence mechanism ili aonekane alikataa mwenyewe lakini anajishtukia kwamba hana chake hapo.
 
kama mtu anataka kumteua amteue uwaziri kamili siyo kivuli kwanza kivuli ndiyo nini! alihoji mh mrema.

Kama yupo bungeni na hajui maana ya waziri kivuli, basi anahitaji psychosocial support.
 
Zile vurugu alifanya Mambo ya Ndani ndiyo mambo makubwa ktk Taifa? Kuhujumu na kusambaratisha Vyama alivyoongoza ni jambo muhimu kwa Watanzania? Sema aliwafanyia kazi nzuri CCM kwa kuhujumu Upinzani kabla ya kustukiwa ni kibaraka wenu!

Nasema ni kibaraka kwasababu hata hiyo TLP hakuna kikao chochote kiliwahi kuketi na kuamua chama chao ni chama rafiki na CCM. Ni yeye binafsi anaye jipendekeza CCM! Vyama vya CDM,CUF na NCCR Mageuzi vimekubaliana kushirikiana,sasa yeye ngebe za nini??

Aliyeanzisha ngebe ni Mbowe, Pale aliposema kuwa hatamuweka Mrema na Cheyo kwenye Baraza kivuli la mawaziri.
Alichofanya Mrema ni kujibu tu kuwa hautaki huo uwaziri. Kosa lake ni lipi mpaka mnamtukana hivi.
 
Niaibu aibu kwa Mbowe kusema hata niteua uwaziri kivuli Mbowe alishaa kuwa nani katika nchi hii mm sitaki kuwa kivuli nataka uwaziri kamili

Nimewahi kuwa NAIBU waziri mkuu na waziri Wa mambo ya ndani

Kuniita kibaraka Wa ccm ni kunipaka matope kibaraka Wa ccm ni seifu Wa Zanzibar anayelipwa na ccm mpaka sasa

Chanzo TBC live muda huu

Mrema kalenga kupata kura tena arudi bungeni mwaka 2015 ndiyo akili yake sasa ana act ukichaa kweli njaa ni mbaya mno .
 
njaa ya mrema mbaya sana.
sikutegemea angetamka maneno kama hayo.
et sasa hivi anaunga mkono ccm!
what a byach!!

jeuri hii anaipata sababu mr LOOK V amemuahidi sasa kuachia mafao yake ya unaibu waziri mkuu aliyoyazuia (lukuvi) tangu bw mrema aikimbie ccm
 
Akizungumza na jambo tanzania mrema ambaye pia ni mbunge wa vunjo kwa tiketi ya chama chake amesema kuwa mbowe ametangaza kujumuisha vyama vya cuf,na nccr mageuzi lakini akavitosa vyama vya TLP NA UDP mrema amesema yeye haoni umhimu wa kuwepo kwenye hilo baraza la mawaziri vivuli kwanza mbowe hana mamlaka ya kumteua kwa nafasi yoyote.

Lakini pia mrema amekwenda mbali kwa kusema kuwa hataki siasa za makundi badala yake anafanya siasa za kusaidia watanzania siyo siasa za kuumiza watanzania kama wanavyofanya chadema kwenye siasa zao.

Mrema amemwambia mbowe kuwa amkome na aachane naye kabisa hataki kufuatwa fuatwa na wanasiasa wasiokuwa na sifa za kuwa wanasiasa kama mbowe.

kwenye mahojiano hayo ya asubuhi ya leo mrema amesema hagombei urais tena biashara za jumla hataki sasa anafanya biashara za rejareja,ameongeza kuwa kama mtu anataka kumteua amteue uwaziri kamili siyo kivuli kwanza kivuli ndiyo nini! alihoji mh mrema.

Kila kitu huwa kina mwanzo na mwisho. Ni kawaida hapa duniani. Kwa wanaoona na kutambua ukweli Mrema alishafika mwisho kisiasa. Hawezi kuwa na mpya katika dunia hii ya sasa yenye vijana wasijali chochote zaidi ya ukweli!

Pia kwa umri wake, it will be a miracle kama akili yake inaweza kuchaji kiasi cha kuja na wazo litakalofanya wengine wafikirie mara mbili. Ni umri. Na ukizeeka inakuwa hivyo. Ni kawaida pia. Ni wazee wachache sana waliopata uwezo wa kuzeeka na akili zao zikabaki na upeo.

Ushauri wangu kwa Mzee Mrema ni kuwa arudishe tu kadi ya TLP, ajiunge CCM. Hii itampa haki ya kuchangia na kufanya chochote ndani ya CCM bila kusimangwa.

Lakini pia nafikiri tatizo ni TLP kukosa maono. Inakuwaje chama chenye hadhi ya kitaifa kinabakia Vunjo tu na wanachama wamekaa wanaangalia? Mwenyekiti ndiyo Mbunge pekee wa chama na wao wameridhika? Halafu Mwenyekiti anakuja hadharani anawaambia kabisa amechoka na urais anataka ubunge tu na wao wanaona sawa tu? Nadhani ninapata wasiwasi na maono ya chama hicho kwa ujumla. Nadhani kuna haja ya kuwa na sheria ya tathmini ya vyama. Vyama vinavyokosa idadi flani a wanachama kifutwe tu.

Pia ninashindwa kuelewa jambo moja tu. Hivi ni kweli kwamba Vunjo nzima na wajanja wote ninaowajua, ni Mrema tu, wa TLP aliyebaki wa kugombea ubunge? Kweli? Hebu itendeeni haki jamii yenu! In case hamjaona bado, dunia ya sasa inahitaji kuwa na maono!
 
Wakuu huyu wa kiraracha anacheza na upepo ashajua kamwagwa kwenye ukawa sasa anatengeneza mazingira eti mbowe anamtaka wa nini cdm ilim kujiaminisha .kumbuka uchaguzi uliopita alisimamisha mgombea uraisi kama mwenyekiti,halafu wakati huo huo anasema urais mpeni kikwete mimi nipeni ubunge tu,,mtu huyo huyo anajihami hataki cheo huko,,nani ampee huyo,,,wewe mzee baki uliko lala salama achana na vijana watakuabisha...
 
Uaminifu na uvumilivu wa Mtu - Mpime kipindi cha njaa tu!!
 
kupewa uawaziri kivuli na mbowe sharti uwe tayari kuburuzwa lakini watu wenye misimamo kama mrema hawako tayari kuburuzwa kwahiyo siyo rahisi kuwajumuisha.
 
Mrema ni mtu aliyekwisha kupoteza hana cha kupigania zaidi ya anamalizaje maisha yake ya kisiasa? Anaamini CCM watamjengea heshima na kumlinda bila kujali namna gani atapata heshima hiyo....
 
Niaibu aibu kwa Mbowe kusema hata niteua uwaziri kivuli Mbowe alishaa kuwa nani katika nchi hii mm sitaki kuwa kivuli nataka uwaziri kamili

Nimewahi kuwa NAIBU waziri mkuu na waziri Wa mambo ya ndani

Kuniita kibaraka Wa ccm ni kunipaka matope kibaraka Wa ccm ni seifu Wa Zanzibar anayelipwa na ccm mpaka sasa

Chanzo TBC live muda huu

hivi mrema halipwi na serikali ya ccm?mbona anapigania kulipwa maslahi yake kwa kutumikia cheo cha naibu waziri mkuu,au ndio anatafuta ukibaraka.
 
1968517_orig.jpg


Mrema ni mchumia tumbo, na katika uzee huu anachohangaikia nini basi. Kwa nini aliikimbia CCM na leo anajibembeleza kwao?

Kinachoendelea kwa Mrema ni sawa na sungura mjanja alipozikosa ndizi mbichi kuzifikia akasingizia sizitaki mbichi hizi.

Mrema angerudisha kadi ya TLP, akachukue ya CCM, ameishiwa Sera, amebaki Historia, nikikumbuka hii siku, na nikikumbuka nyumbani kipindi kile 1995, 2000 TLP, tulipohama naye kwa mbwembwe, gari yake TZK ilipokamatwa hakumalizia mkopo, tukapitisha bakuli nchi nzima tukaigomboa gari..baadaye akatimuliwa kwenye nyumba masaki, chama kikamnunulia nyumba sinza tena sio kwa mkopo,..... Leo anataka kugombea ubunge anaenda kuomba hela SISIEM!

Hii laana haitamwacha kamwe
 
Trend yake inazidi kushuka kutoka kugombea Uraisi- Ubunge. sasa itakuwa Udiwani kwa mwaka 2015 akiwa na nguvu bado 2020 Uenyekiti wa mtaa.

Hata Mbowe alishaa wahi gombea uraisi na sasa Mbunge 2015 ni diwani Wa bomang'ombe Hai
 
kumzungumzia mrema, ni kupoteza muda, ni mchekeshaji wa ccm, ngoja tuangalie taifa linasonga vipi.
 
Tumsamehe huyu mzee ameshachoka hata kufikiri hawezi. Sisi vunjo hatuna mbunge. Yule kama siyo mzee ruksa ambae angempa madaraka
Niaibu aibu kwa Mbowe kusema hata niteua uwaziri kivuli Mbowe alishaa kuwa nani katika nchi hii mm sitaki kuwa kivuli nataka uwaziri kamili

Nimewahi kuwa NAIBU waziri mkuu na waziri Wa mambo ya ndani

Kuniita kibaraka Wa ccm ni kunipaka matope kibaraka Wa ccm ni seifu Wa Zanzibar anayelipwa na ccm mpaka sasa

Chanzo TBC live muda huu
 
Back
Top Bottom