Mrema adai Sh 1 bilioni kwa Spika Sitta

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
%5Cmremamrema.jpg
Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema akizungumza katika mkutano na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam jana juu ya kumfungulia kesi ya madai Spika wa Bunge, Samwel Sitta katika Mahakama Kuu kwa kile alichodai kuwa alimkashfu na kumvunjia heshima.

MWENYEKITI wa Tanzania Labour Party(TLP) taifa, Augustine Mrema amemfungulia kesi ya madai Spika wa Bunge la Tanzania Samuel Sitta kwa kile alichodai kuwa ni kumkashfu na kumvunjia heshima.

Kesi hiyo ya madai yenye namba 32 ya mwaka 2010ilifunguliwa Mahakama Kuu juzi baada ya kumalizika kwa muda wa siku saba alioutoa kwa Spika Sitta ili aweze kuuomba radhi kutokana na kashfa alizomtolea.

Katika kesi hiyo Mrema anamtaka Sitta kumlipa fidia ya Sh 1 bilioni za kitanzania katika kipindi cha siku saba tangu alipopokea barua yake.

Hivi karibuni Sitta alinukuliwa na gazeti hili akimwelezea Mrema kuwa amekwisha kisiasa, na kipesa (amefulia) hali ambayo Mrema alisema ni kuvunjia heshima hivyo, kumpa notisi ya siku saba ili aweze kumuomba radhi, lakini Sitta hakutekeleza.

Mrema ambaye hivi karibuni alionekana kumtetea Rais Kikwete kwa kiasi kikubwa alisema, kitendo alichokifanya Sitta hakikuwa cha heshima na kuwa lengo lake lilikuwa ni kumuundia njama kwa polisi ili wamkamate kwa kuwa anakula rushwa.
Hii yote ni njama ya Sitta aliyotaka kuniundia kwa mapolisi ili waje wanikamate kwa kuwa eti natumiwa na CCM katika kukipigia kampeni, mimi sipokea wala sitoi rushwa jamani, kwanini nipigie kampeni chama kingine wakati nina chama changu, alihoji Mrema.

Mrema alisema, Sitta hajatumia madaraka yake vizuri kwa kuwa amekiuka misingi anayotakiwa kuwa nayo Spika wa Bunge lolote, na kuwa anaongoza moja kati ya mihimili mitatu ndani ya nchi.

Spika ni mhimili na kiongozi muhimu katika nchi anatakiwa kuongoza kwa haki tena bila kubagua, lakini yeye anaongoza kwa makundi kwa nini,alihoji.

Mrema aliongeza kuwa madaraka aliyoyatumia Sitta yamemvunjia heshima yake aliyokuwa nayo kwa sababu tangu amtolee kashfa hizo baadhi ya wananchi wameanza kumdharau.

Watu wote wameshanza kunidharau sasa, hivyi kweli heshima yangu niliojijengea tangu uongozi wangu wote nilipokuwa Serikalini mpaka hapa nilipo leo hii Mwenyekiti wa Chama Taifa halafu natupiwa matusi na kashfa kiasi hicho, mbona amenidhalilisha sana huyu Sitta jamani,alisema Mrema.

Mrema aliendelea kuwa, bado anahofia maisha yake kwa kukamatwa na polisi kwa kuwa Sitta yuko katika kamati kuu na ni mjumbe hivyo anaweza kuaminika na mtu yeyote.

Aidha Mrema alimtaka Sitta kuacha kutumia jina lake katika kupiga kampeni za kumchafua Rais Kikwete na kuwa kama ana malengo ya kumchafua Rais amfuate moja kwa moja.

Hizi ni kampeni chafu, Kama Sitta anataka kumkashfu Kikwete asinitumie mimi apite moja kwa moja akamweleze alisema Mrema.

Alisema yeye hawezi kuipigia kampeni CCM kwa kuwa hata yeye ana chama chake na kuwa kama CCM ilipata ushindi wa kishindo katika miaka ya nyuma bila yeye kufanya kampeni iweje iwe mwaka 2010.

"Tangu mwaka 1995 hadi 2005 CCM ilipata ushindi wake kwa nguvu bila kupigiwa debe na mrema iweje iwe mwaka huu, mimi ni mtu mdogo sana kwa nafasi hizo" alisema Mrema.


http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18760
 
Sh 1 billion? Hela za uchaguzi nini? Maana kiwango hicho si ndiyo limit ya kugombania uraisi?
 
Watu wote wameshanza kunidharau sasa, hivyi kweli heshima yangu niliojijengea tangu uongozi wangu wote nilipokuwa Serikalini mpaka hapa nilipo leo hii Mwenyekiti wa Chama Taifa halafu natupiwa matusi na kashfa kiasi hicho, mbona amenidhalilisha sana huyu Sitta jamani,alisema Mrema.

Mtaji watafutwa huo!
Nae huyu hawezi kujieleza bila kutaja kazi alizofanya akiwa sisiem!
 
the guy now is geting too old 2 b on stage, anajiaibisha tu,wazee wenzake si wamshauri.
 
Back
Top Bottom