Mrejesho wa connection za wataalam(waganga) wa kutoa UTAJIRI, ukimuona tajiri mpe HESHIMA YAKE

Ukiona mtu anatafuta mganga ili awe tajiri basi ni mjinga kiwango cha lami. Skia dogo hata kwenye maandiko yanasema Mungu atakubariki kwa kazi za mikono yako. Anzisha mradi au biashara fanya kwa juhudi alafu tafuta mganga utatoboa mbali na hapo utaenda kuombwa spika uone waganga wabaya wakati huna chochote ha kujishughulisha. Hakuna mganga anaetoa utajiri bali wanafanya soothruning ya mambo yako utajiri ni plani zako. Ua mama ua baba na watoto uwe tajiri ila utalala chini na hutavaa vizuri wala kula vizuri ndo utajiri unaotaka sio?
 
Kuwa makini kijana waganga wanasema ukikosa wa kienyeji leta hata broila.
Kuna mmoja aliniambia in a very simple way "Nitumie hiyo 30k, mwizi wako utakutana naye kesho akija kulia mlangoni kwako", hapo nilikuwa nimeibiwa ka-laptop kangu. Nikaona anataka apokee hela alafu afanye uganga kwa bluetooth nikapotezea. Toka siku ile sijawahi amini haya mambo ya kina manyanga
 
Huwa nasikia wapo, japo huhusisha kafara . Kuwapata Nako ni tizi sana zaidi utapata matapeli utapigwa kweli kweli . Piga kazi mda ukifika utatoboa mkuu.
Mwanangu kazi nshapiga mpaka basi ila daaaah kutoboa ni kipengele
 
Kuna bibi mmoja yupo hapo Morogoro maeneo mang’ura Kwa chini kidogo vijiji vitatu au vinne kutoka hapo uhakika kabsa ila nilifuta namba zake na kuwaacha jamaa zangu walionishinikiza twende kwa mganga kutafuta utajiri mimi sikutaka wao walikuwa na nia kweli na leo ni matajiri na nna uhakika kabsa utajiri wamepewa na huyo bibi

Ana utajiri wa pete- hii pete unaongea nayo yaani kama binaadamu mwenzako unataka nini? Na inakupatia hii pete ina mashart mengi sana yaani- sio nzuri

Ana utajiri wa kuoza - hii mnatakiwa muwe wawili na anawapa na dawa ya kuoza yaani zamu zamu kuoza uafunga mlango unampaka hivyo vimaji mwenzako sijui vimafuta then unamfungia mlango anaanza kuoza wale wadudu wanaotoka ndio wanakuja geuka pesa unaoza siku 3 mwenzako anachota wale funza na kuwajaza kwenye beseni au jaba baada ya siku tatu wanageuka elf 10 , 10 na zamu yako ikifika hivyo hivyo

Ana utajiri wa nyoka- unatakiwa uwe wewe na mke wako nyoka mnamfungia chumbani na kila baada ya mda unatakiwa umpeleke mke wako kwenye hicho chumba nyoka amlambe ukeni mke wako mpaka anaporidhika na pesa zinamiminika baada ya mda

Kutoa kafara wazazi- hapa ndio alinifanya nikatae utajiri wa kiganga yaani nitoe kafara baba na mama yangu nipate pesa- sikuweza hata kuvumilia kukaa kusikiliza tajiri zingine niliomba kuondoka, nawapenda sana wazazi wangu aisee japo kuwa watu wazima waache waendelee kuishi mpaka M/Mungu atapowapitishia nusra yake.. nilisepa

Tulienda na kukutana kwenye biashara na ndio tulikutana na kushahuriana kwenda kwa huyo mganga na tulienda na mimi niliwaacha wenzangu sasa hivi ni matajiri mbaya aisee na nawaogopa hata namba zao sizitaki aisee coz najua fika utajiri wao sio
 
Back
Top Bottom