pistmshai
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,313
- 3,689
POLE KWA YALIYOKUKUTA MKUU..!
"..Sihitaji mahusiano na mwanaume yoyote kwa kipindi hiki.bali ntaongeza juhudi zaidi kumwomba MUNGU,.."
"..nisije tena dumbukia kwenye mahusiano ambayo Hayana msimamo na malengo.."
"..Sihitaji PM ambazo zisizo na maana.."
"..Sihitaji mahusiano na mwanaume yoyote kwa kipindi hiki.bali ntaongeza juhudi zaidi kumwomba MUNGU,.."
- Kifanye kiwe kipindi cha muhimu kwako cha kujitathimini mapungufu yako katika mahusiano.. na kujirekebisha.. Ujihoji kwanini ulihitaji mahusiano na umejifunza nini kwenye mambo uliyopitia katika mahusiano.. kisha JIREKEBISHE kwa ajili ya wakati mwingine ujao.
"..nisije tena dumbukia kwenye mahusiano ambayo Hayana msimamo na malengo.."
- usiruhusu kijiingiza katika mahusiano kwa bahati mbaya, mahusiano mazuri yanaanzia kwa mtu ambae mnafahamiana vizuri kabla ya kuingia katika mahusiano ya kimapenzi (kwa mfano URAFIKI),hapo itakuwa rahisi kupata muda ya kumtambua vizuri mtu unaempenda kabla ya kufanya maamuzi magumu. Utakuwa umeridhika kuwa unaanza mahusiano na mtu mnaeshare common interests and goals.
"..Sihitaji PM ambazo zisizo na maana.."
- Nakutakia kila heri upokee PM zenye maana tu!