Mrejesho: Naomba msaada wa ada

Io pesa bora ufanyie biashara icho cheti na hicho chuo ulichosoma kupata kazi ya maana ni majaliwa kwa tz ya sasa
Mi naonA io pesa fanyia mtaji kwenye harakati zako.
Asante kwa ushauri mkuu.

Itanilazimu kulipa ada ili kuonesha uaminifu.

Nakihitaji cheti ili niweze kupeleka TSD niweze kupewa ajira maalum za serikali.
 
Ndio na hawakutoa siku moja.

Ni baada ya kuwasumbua miezi zaidi ya nane bila kukata tamaa,i gues walinipa ili kuepuka usumbufu.

Yaani hao DC na DAS wao wawili wameshindwa kukusaidia hata m 1 wameamua kukupa barua ya kuchangisha!??

Ila kila la kheri mungu atakusaidia mkuu
 
M
Mrejesho: habarini za asubuhi wanajamvi natumaini tu wazima humu,
Baada salamu naomba kwenda kwenye mada iliopo na kuwaletea kile ambacho niliahidia nitafuatilia kujua ukweli, ndugu zangu nimeamka leo mapema na kwenda kukitafuta hicho chuo alichosoma mwenzetu na kujua kama kweli amesomea hapo .
Ukweli ni kwamba huyu mwanafunzi amesomea hapo kweli na chuo ni chenyewe kweli kinamilikiwa na kanisa la Romani catholic, kwa bahati mbaya sikubahatika kuonana na mkuu wa chuo hiki nimeambiwa yupo safarini ila nimekutana na makamu wake kwa jina anafahamika kama ERNEST JUMBANI (vice principal) na kwa bahati nzuri zaidi huyu nae akawa ni mnyaturu tena tumetoka kijiji kimoja hivyo tuliongea kwa lugha ya kinyumbani zaidi na kunihakikishia kuwa kijana huyu amemfundisha yeye na anafahamu kila kitu kuhusu mwenzetu huyu na yeye ndio alipigania asifukuzwe chuo bali asome atakuja kulipa baadae kutokana na hali yake, japo wenzie ambao walikuwa hawajalipa kama yeye walifukuzwa chuo.

Ni kweli anadaiwa ila makamu huyu hakuwa tayari kutaja gharama halisi akiogopa kujichanganya maana mhasibu hakuwepo lakini aliniambia ni zaidi ya milioni moja, na akasema waliwahi kupata simu kutoka kwa mkuu wa wilaya ya huko mtwara alipo huyu ndogo yetu na waliombwa kutoa gharama zote na walipewa gharama hizo lakini mpaka sasa wapo kimya na hawajatekeleza chochote, lakini makamu wa chuo hichi ameniahidi mara tu mkuu wa chuo atakapo rudi atanipigia simu na kwenda kunipa gharama zote na kunipa mrejesho kutoka kwa DC huyo aliewahi kuulizia gharama zote anazodaiwa kijana huyu.

Maoni yangu:
Nianze mimi mwenyewe kuwa nimeridhika na maelezo yote na nipo tayari kumchangia mwenzetu huyu kiasi cha Tsh.100,000/= na nilikuwa na ombi kwa wanajamvi watakao kuwa tayari kumsadia mwenzetu wafanye hivyo kwa moyo mmoja huyu bwana ni kweli ana shida hii.

Swali: Je! hii fedha tumchangie kumpa yeye au tumwambie mkurugenzi wetu Melo atukusanyie na mara itakapotimia apewe account ya chuo alipe then amtumie pay slip ndugu yetu akachukue cheti?
Naomba kupata mawazo ya namna ya kukusanya michango hii?
 
Niombe pia kama hizo taarifa sio za kweli na kama hamjui huyo makamu basi akanushe hapa hadharani kama kuna wadau pia watahitaji kupata mawasiliano ya viongozi hao wa chuo nipo tayari kuziweka hapa
 
Asante sana kaka,sina cha kukulipa,kwa muda wako,rasilimali zako na kujitolea kwako,Mungu akubariki.

Mkurugenzi melo nadhani ni mtu mmoja bussy sana,ningeshauri wewe mwenyewe ndiye ukusanye chochote kitakachopatikana na ulipe na kunipatia payslip endapo bado upo huko Singida.

Mbali na yote,narudia tena Mungu awabariki kwa Moyo wa ukarimu na kujitoa kwa mtu baki,ingawaje bado kila mtu ana matatizo yake pia.
 
Niombe pia kama hizo taarifa sio za kweli na kama hamjui huyo makamu basi akanushe hapa hadharani kama kuna wadau pia watahitaji kupata mawasiliano ya viongozi hao wa chuo nipo tayari kuziweka hapa
Rudia kusoma ulichokiandika
 
Ngoja waje wanajamvi washauri pia wao kwa hili mkuu
 
Pointi sana hii ,ikifanyiwa kazi itatupa imani
 
Cc Mpauko

Chuo kinaitwa ST. BERNARD TEACHER'S COLLEGE Kilianzishwa mwaka 2012, zamani kilikuwa chuo cha biblia, Chuo kipo mkoa wa SINGIDA, WILAYA YA SINGIDA MJINI, ENEO LA MISUNA TAKRIBANI KILOMETA 1 TOKA STEND MPYA MISUNA.

Chuo kinamilikiwa na kanisa katoliki dayosisi ya singida.

Mkuu wa chuo anaitwa Fr. Gilbert mwiru, Makamu ni Mr. Ernest Jumbani, mwadili ni Mr. Amasi.

Mawasiliano ya mkuu wa chuo ni 0786013103 (Fr. Mwiru)
 
Asante..data zote ni sahihi,Barikiwa.
 
Mungu akubariki Sana Kaka yangu.
Chukua hili Neno hes6:24-26
 
 

Sorry kwa kunukuu maoni marefu ila ushauri wangu haya maelezo yako yaweke juu kabisa kwenye uzi wa mhusika ili watu wanaposoma wajue ufwatiliaji ulishafanywa. Pia muweke namba za kuchangia
 
Sorry kwa kunukuu maoni marefu ila ushauri wangu haya maelezo yako yaweke juu kabisa kwenye uzi wa mhusika ili watu wanaposoma wajue ufwatiliaji ulishafanywa. Pia muweke namba za kuchangia
Ahsante kwa ushauri mkuu, na nahisi fedha zote ziende kwa mhusika kuna namba zake hapo juu zipo mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…