Mengine haya huumiza, Tusaidiane...

Mpauko

R.I.P
Jan 19, 2019
2,323
3,353
Kwa wanajamiiforum,viongozi na taasisi mbalimbali.

Mimi ni kijana wa miaka 25,mkazi wa Mtwara na nina tatizo katika masikio(hearing impairment)

Ilikuwa mwaka 2004 nilipoamka na kukuta usikivu umepotea na kubaki na usikivu hafifu,hususani katika matamshi ni vigumu kuelewa bila kutumia facial expressions na lips reading.

Pamoja na mambo mengine,nilipata matibabu hositali ya Muhimbili ambapo walinipatia mashine (shimesikio) haikuweza kunisaidia kwani matamshi yalibaki kuwa changamoto bila kutumia facial expressions na lips reading.

Maisha ya shule yalikuwa na changamoto nyingi sana kwani nilisoma shule ya kawaida (Shangai Primary) hatimaye nilihitimu 2009 na kuchaguliwa kidato cha kwanza.

Mwaka 2013 nikahitimu kidato cha nne (Bright Angels Secondary) kutokana na changamoto nyingi sikupendelea kwenda kidato cha tano,hivyo nikajiunga na STEMMUCO,Mtwara kusoma Business administration.

Vijembe,dharau,kejeli na maneno ya hovyo vilifanya maisha yangu chuoni kuwa magumu mno ukizingatia mtindo wa ufundishaji vyuoni (leicture hall) haukuwa rafiki kwangu kwani sikuweza kuelewa chochote hii ikanifanya kutumia nguvu nyingi kutafuta notes na kujisomea mwenyewe.

Niliponaliza certificate nilikata tamaa ya kuendelea na masomo kwani ilikuwa vigumu kupitisha siku bila kukumbana na vijembe,kejeri na dharau toka kwa wanachuo na leicturer kutokana na hali ya kutosikia.

Mwaka 2016 kupitia stori ya dada mmoja kiziwi (Aneth Gerana) na mwingine ambaye alipatwa na ajali akiwa katika mahafali na kupooza(nimemsahau jina) nilipata motive sana ya kukaza moyo na kuendelea na masomo.

Hivyo nikajiunga na mafunzo ya ualimu Grade A na kuhitimu mwaka 2018(ST.Bernad TC).

Ingawaje nilihitimu lakini nilimaliza kwa neema tu,kwani sikumudu kulipia ada tena,nilibaki na deni la T.shs 1,160000/=,nikajiapiza kufanya vibarua kwa bidii ili nikomboe cheti changu.

Nikarudi nyumbani na kuanza kutafuta vibarua,mambo yalikuwa tofauti na matarajio yangu.

Hali ya usikivu hafifu ikawa fimbo yangu mwenyewe,nilizunguka huku na huko bila mafanikio kwani waajiri hawakuwa tayari kunipa ajira wala majaribio achilia mbali vibarua vidogovidogo.

Kwa miezi nane nilizunguka huku na huko bila mafanikio,hata volunteer (kujitolea) walikataa hivyo ikabidi nikae chini kubuni cha kufanya ili nijikwamue kwani afya yangu ilianza kuwa tete kutokana na ukosefu wa mlo wa kutosha(mara nyingi ni mlo mmoja kwa siku)

Kupitia jamiiforum nilipata ufahamu kidogo,nikaenda manispaa kujaribu kuomba msaada,hatimaye baada ya danadana nyingi,nikaenda ofisi ya DC.

Nako hakukuwa na matokeo mazuri sana zaidi ya kupewa kibali cha kuchangisha na najaribu.

Hivyo basi,ninaomba kwa yeyote mwenye uwezo wa kunisaidia asisite kufanya hivyo.

Najaribu kukomboa vyeti vyangu ili niweze kuvitumia kuombea ajira niweze kujikwamua kimaisha kupitia ajira maalumu za serikali.

Vilevile kwa mwenye kuweza kunisaidia wazo la biashara nayoweza kuifanya nikiwa na hali hii.

Naomba anayeweza kunisaidia mtaji wa biashara.

Kwa mawasiliano 0677421378Tigo

NAOMBA RADHI KWA WATAKAUCHUKIZWA NAMI PLEASE GO EASY ON ME.

manengelo
Avriel
MKUU WA KAYA
Maxence Melo
Paddy
kaburungu
copyright
moyes
IMG_20190827_235842_003.jpeg
IMG_20190828_005347_917.jpeg
IMG_20190826_120726.jpeg
 
Hilo tangazo lipo sawa kweli mkuu,?
Hujaweka namba za simu,
Hujaweka account za bank
Hujaweka physical adress

Mtu kama anakuchangia anakuchangia vipi ?
 
Boss kwa detail ulizotoa kama mtu akiwa willing kukuchangia atumie account ya mkuu wa Wilaya? Ama Katibu tawala maana hujaweka namba ya simu and likely!
 
Pole Sana Mkuu..Hayo yote ni Mapito tu yana mwisho wake na iko siku utasahau kama ulipitia changamoto hizo...

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Dunia ina changamoto sana,usikate tamaa
Nakushauri tafuta wazo ujiajiri.achana na mpango wa kukomboa vyeti kwa sasa.hata ukivipata unaweza jikuta unazunguka kulekule mwaka mzima.ni ngumu sana watu wenye ulemavu kuajiriwa labda kwa ajira za utumishi angalau.fungus hata duka,tafuta kijana utaekua unamlipa anasimamia mauzo,na hiyo elimu yako hushindwi kufanya mahesabu mwenyewe.vyeti utavikomboa baadae

Ni mawazo yangu tu.

Pia wenye matatizo ya usikivu wapi wengine saana,mpaka america na ulaya dunia mzima wapi kwa mamilioni,so usijione uko peke yako.na ni tatizo la kawaida sana.
Mwisho wa yote naomba umtafute sana Mungu,kwake hakishindikani kitu.kuwa mwaminifu kwa Mungu ukimtafuta kwa bidii nae atakuinua kwa wakati wake!
 
Pole sana...hizo ndio changamoto za maisha.

Tukirudi kwenye mada husika...umesema umeshaomba AJIRA, FIELD WORK, VOLUNTEER WORK na kote umekosa kwasababu ya tatizo lako right??? Sasa kwanini unakimbilia kukomboa cheti ili urudie kufanya kile kile ambacho umeshindwa kufanikisha kwa muda mrefu??? Je cheti chako kitabadilisha nini??? Kwasababu kama kinachokukosesha hizo nafasi na hali yako....je cheti kitasaidia vipi???

Binafsi ningekushauri mambo mawili....
#1 Acha kulalamika sana kuhusu tatizo lako na kulitumia kujiongezea unyonge. Wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kukumbana na changamoto kwenye hii dunia and the sooner you realise that and make peace with it the better!!!

Unamfahamu Wakonta wewe??? Kama umfahama please google her name au mtafute Instagram. Wakonta aligongwa kwenye graduation yake ya form 4 na matokeo yake aliparalyse mwili mzima si mikono,si miguu...which means hawezi ku-move around bila msaada.

Katika hali ya kawaida ungetegemea Wakonta awe mnyonge kupita maelezo ila hana unyonge wowote ndani yake. She is as strong as anyone could ever be. Mpambanaji haswa!!! (This is why I love her) na huwezi amini alipo sasa.

Anyway....my point is, kuna watu ambao situation zao ni much worse than your yours ila mentality yako ya "MNYONGE MIE, MASIKINI MIE" vinakurudisha nyuma na hicho cheti sio tiketi yako ya kupiga hatua kwenda mbele. Una miguu, mikono, akili na macho ambavyo vyote vinafanya kazi sawia...BE GREATFUL!!!!!

#2 Achana na swala la kuajiriwa kwasababu umeshaona sio swala rahisi kutokana na uelewa wetu waswahili kuwa mdogo. Badala yake fikiria KUJIAJIRI!!! Either tumia elimu yako kianzisha kitu chako mwenyewe au tumia talanta nyinginezo ulizonazo uanze biashara yako mwenyewe.

Narudia tena...msome Wakonta, pamoja na changamoto alizonazo yeye bado ameweza kufungua biashara yake, ni ambassador wa vitu mbali mbali na anaishi kwake pazuri (she pays her own rent and what not)....sasa kwanini wewe ushindwe????

Punguza kulalama na kulaumu then pambana utashangaa mwenyewe jinsi ambavyo utafanikiwa.
 
Nimeweka namba ya simu,nilisahau tafadhali naomba mnisaidie.
Boss kwa detail ulizotoa kama mtu akiwa willing kukuchangia atumie account ya mkuu wa Wilaya? Ama Katibu tawala maana hujaweka namba ya simu and likely!
 
Asante,naomba Mnisaidie
Pole Sana Mkuu..Hayo yote ni Mapito tu yana mwisho wake na iko siku utasahau kama ulipitia changamoto hizo...

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Gairo
 
Unaweza pitia threads zangu za mwanzo.

Nilijaribu kutafuta mtaji kwa hali na mali sikufanikiwa kujiajiri ni kipaumbele changu pia.

Nalazimika kukomboa cheti ili niweze kuomba ajira maalum za utumishi kwa sababu sina chaguo lingine.

Kwa namna yoyote unayoweza kuona itanikwamua naomba unisaidie.
Dunia ina changamoto sana,usikate tamaa
Nakushauri tafuta wazo ujiajiri.achana na mpango wa kukomboa vyeti kwa sasa.hata ukivipata unaweza jikuta unazunguka kulekule mwaka mzima.ni ngumu sana watu wenye ulemavu kuajiriwa labda kwa ajira za utumishi angalau.fungus hata duka,tafuta kijana utaekua unamlipa anasimamia mauzo,na hiyo elimu yako hushindwi kufanya mahesabu mwenyewe.vyeti utavikomboa baadae

Ni mawazo yangu tu.

Pia wenye matatizo ya usikivu wapi wengine saana,mpaka america na ulaya dunia mzima wapi kwa mamilioni,so usijione uko peke yako.na ni tatizo la kawaida sana.
Mwisho wa yote naomba umtafute sana Mungu,kwake hakishindikani kitu.kuwa mwaminifu kwa Mungu ukimtafuta kwa bidii nae atakuinua kwa wakati wake!
 
Ahsante kwa ushauri mzuri dada Lizzy.

Ahsante sana.

Ningependa kukusahisha kuwa silalamiki juu ya tatizo langu anymore,kuna kipindi fulani nililalamika lakini sasa najitambua hivyo katika thread hii sijalalamika pia.

Ni kweli Volunteer,field na ajira nimeshindwa kupata kutokana na tatizo langu.

Nataka kukomboa cheti baada ya kupata watu wenye uelewa juu ya ajira maalumu za serikali,ambapo wapo willing kunisaidia kuapply ajira hizo ndiyo maana nataka nipate cheti niweze kufanya mchakato huo,hatimaye ajira iweze kunikomboa kimaisha.

Vilevile kujiendeleza kielimu nitahitaji cheti hiko pia.

Mimi si mnyonge,nina amani sana even licha ya kuwa na hili tatizo nilipata marafiki wenye busara walionisaidia kujitambua zaidi na najitambua sana.

Kipindi fulani nilikata tamaa ya kuendelea na masomo,it was Wakonta na Aneth gerana walioniinspire kukaza moyo hadi nikarudi shuleni na kumaliza masomo.

Nakiri Wakonta hakuwahi kuwa mnyonge,she was always bright,thats why aliniinspire sana.

Wakati mwingine maisha yalinisukuma kulalamika na kuwa mnyonge kwa sababu...katika hali ya kawaida kuwa rejected kwa kosa ambalo halikuwa kusudi lako inaumiza pia,mimi ni binadamu tu hisia ninazo.

.hali halisi ya maisha mfano kulala na njaa,kula mlo mmoja,kulala sehemu isiyo salama,kuugua na kuonekana like si kitu si mtu hata kwa familia yako mwenyewe haya yalipelekea kuwa dhaifu sana kiasi nisimudu vibarua vya kutumia nguvu,miguu inaishiwa nguvu,kutetemeka mikono na kizunguzungu kikali.

Hivyo ni baadhi ya vitu vilivyoninyima amani na kunifanya niwe vile(kulalamika sana) lakini sasa silalamiki tena.

Suala la kujiajiri ni kipaumbele changu pia,lakini sina kitu kwa sasa kuweza kujiajiri nimefanya juhudi nyingi na jitihada nyingi sana lakini sijafanikiwa.

Kadhalika napambana sana dada natamani mafanikio ya watu kama Wakonta na Aneth,wapo wengi wa aina hii waliofanikiwa na wanaoendelea na mapambano.

Lakini hawakufanikiwa peke yao,kama ilivyo kwangu nipo peke yangu si ndugu si marafiki,hii inaniwia ugumu lakini si sababu ya mimi kuacha kupambana,bado najaribu.

Ndio maana nipo hapa leo,silalamiki bali najaribu kujikwamua.

Pole sana...hizo ndio changamoto za maisha.

Tukirudi kwenye mada husika...umesema umeshaomba AJIRA, FIELD WORK, VOLUNTEER WORK na kote umekosa kwasababu ya tatizo lako right??? Sasa kwanini unakimbilia kukomboa cheti ili urudie kufanya kile kile ambacho umeshindwa kufanikisha kwa muda mrefu??? Je cheti chako kitabadilisha nini??? Kwachokukosesha hizo nafasi na hali yako....je cheti kitasaidia vipi???

Binafsi ningekushauri mambo mawili....
#1 Acha kulalamika sana kuhusu tatizo lako na kulitumia kujiongezea unyonge. Wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kukumbana na changamoto kwenye hii dunia and the sooner you realise that and make peace with it the better!!!

Unamfahamu Wakonta wewe??? Kama umfahama please google her name au mtafute Instagram. Wakonta aligongwa kwenye graduation yake ya form 4 na matokeo yake aliparalyse mwili mzima si mikono,si miguu...which means hawezi ku-move around bila msaada.

Katika hali ya kawaida ungetegemea Wakonta awe mnyonge kupita maelezo ila hana unyonge wowote ndani yake. She is as strong as anyone could ever be. Mpambanaji haswa!!! (This is why I love her) na huwezi amini alipo sasa.

Anyway....my point is, kuna watu ambao situation zao ni much worse than your yours ila mentality yako ya "MNYONGE MIE, MASIKINI MIE" vinakurudisha nyuma na hicho cheti sio tiketi yako ya kupiga hatua kwenda mbele. Una miguu, mikono, akili na macho ambavyo vyote vinafanya kazi sawia...BE GREATFUL!!!!!

#2 Achana na swala la kuajiriwa kwasababu umeshaona sio swala rahisi kutokana na uelewa wetu waswahili kuwa mdogo. Badala yake fikiria KUJIAJIRI!!! Either tumia elimu yako kianzisha kitu chako mwenyewe au tumia talanta nyinginezo ulizonazo uanze biashara yako mwenyewe.

Narudia tena...msome Wakonta, pamoja na changamoto alizonazo yeye bado ameweza kufungua biashara yake, ni ambassador wa vitu mbali mbali na anaishi kwake pazuri (she pays her own rent and what not)....sasa kwanini wewe ushindwe????

Punguza kulalama na kulaumu then pambana utashangaa mwenyewe jinsi ambavyo utafanikiwa.
 
Unaweza pitia threads zangu za mwanzo.

Nilijaribu kutafuta mtaji kwa hali na mali sikufanikiwa kujiajiri ni kipaumbele changu pia.

Nalazimika kukomboa cheti ili niweze kuomba ajira maalum za utumishi kwa sababu sina chaguo lingine.

Kwa namna yoyote unayoweza kuona itanikwamua naomba unisaidie.
Ishu ndo mtaji...utapata tu

Ishu ni utapenda kufanya kipi kama kujiajiri ukiwa utapata mtaji?
Andika business idea ambayo utaimudu,ikikamilika waonyeshe watu,itawavutia zaidi kukuchangia ufikie lengo.pia ukishapata mtaji utawaonyesha biashara ulofungua kama uthibitisho
 
Pole sana...hizo ndio changamoto za maisha.
Tukirudi kwenye mada husika...umesema umeshaomba AJIRA, FIELD WORK, VOLUNTEER WORK na kote umekosa kwasababu ya tatizo lako right??? Sasa kwanini unakimbilia kukomboa cheti ili urudie kufanya kile kile ambacho umeshindwa kufanikisha kwa muda mrefu??? Je cheti chako kitabadilisha nini??? Kwasababu kama kinachokukosesha hizo nafasi na hali yako....je cheti kitasaidia vipi???
Binafsi ningekushauri mambo mawili....
#1 Acha kulalamika sana kuhusu tatizo lako na kulitumia kujiongezea unyonge. Wewe sio wa kwanza wala wa mwisho kukumbana na changamoto kwenye hii dunia and the sooner you realise that and make peace with it the better!!!
Unamfahamu Wakonta wewe??? Kama umfahama please google her name au mtafute Instagram. Wakonta aligongwa kwenye graduation yake ya form 4 na matokeo yake aliparalyse mwili mzima si mikono,si miguu...which means hawezi ku-move around bila msaada.
Katika hali ya kawaida ungetegemea Wakonta awe mnyonge kupita maelezo ila hana unyonge wowote ndani yake. She is as strong as anyone could ever be. Mpambanaji haswa!!! (This is why I love her) na huwezi amini alipo sasa.
Anyway....my point is, kuna watu ambao situation zao ni much worse than your yours ila mentality yako ya "MNYONGE MIE, MASIKINI MIE" vinakurudisha nyuma na hicho cheti sio tiketi yako ya kupiga hatua kwenda mbele. Una miguu, mikono, akili na macho ambavyo vyote vinafanya kazi sawia...BE GREATFUL!!!!!
#2 Achana na swala la kuajiriwa kwasababu umeshaona sio swala rahisi kutokana na uelewa wetu waswahili kuwa mdogo. Badala yake fikiria KUJIAJIRI!!! Either tumia elimu yako kianzisha kitu chako mwenyewe au tumia talanta nyinginezo ulizonazo uanze biashara yako mwenyewe.
Narudia tena...msome Wakonta, pamoja na changamoto alizonazo yeye bado ameweza kufungua biashara yake, ni ambassador wa vitu mbali mbali na anaishi kwake pazuri (she pays her own rent and what not)....sasa kwanini wewe ushindwe????
Punguza kulalama na kulaumu then pambana utashangaa mwenyewe jinsi ambavyo utafanikiwa.
good comment ever, kijana anapenda kulalamika sana badala ya kupambana zaidi, by the way kwanini watu wa kuchukie, vijembe na dharau bila sababu yoyote??
 
Nimeeleza kwa kina kuwa napambana sana sana na hapa sipo kulalamika bali naendelea kujaribu kujikwamua.

Kejeli na dharau kwa walemavu ni vitu vya kawaida,hakuna anayenichukia.
 
Ishu ndo mtaji...utapata tu

Ishu ni utapenda kufanya kipi kama kujiajiri ukiwa utapata mtaji?
Andika business idea ambayo utaimudu,ikikamilika waonyeshe watu,itawavutia zaidi kukuchangia ufikie lengo.pia ukishapata mtaji utawaonyesha biashara ulofungua kama uthibitisho
Mkuu jitihada hizo nimejaribu sana pia bila mafanikio
 
Hivi CHAVITA na TSD wameshindwa kukusaidia kwa kwa lolote?
TSD kikawaida ili usaidiwe unahitaji uende na cheti cha kuhitimu mafunzo, kama alivojieleza alihitimu lakini hakuweza pata cheti kwakuwa anadaiwa hivyo anatafuta usaidizi akagomboe cheti kisha akipeleke kwa wahusika wa ajira maalum...

CHAVITA kinasaidia lakini recently ukiwafuatilia sana changamoto kubwa ni funding kusupport members wao imekuwa finyu sana....
 
Kujiajiri right....
Show him the way, wakonta got support toka kwa family hasa mama yake,watu mbalimbali plus her personal intuition ndio inamfikisha pale, imagine asingepata support kutokana na madhira yake, let's me and you support him awe na initial point ajiestablish..
Fikiria MTU ambae hata kula kwake ni changamoto, maana yake hali ni tete sana upande wake japo hapaswi kuwa mnyonge kwa mazingira hayo!

Asante.

Back
Top Bottom