Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Miss Natafuta
shosti upo? sijakuona siku mbili tatu hizi shoga yangu!! au ulikuwa busy kwenye msiba wa Kitwana Kondo?
 

Nishapigwa laki 8 zangu huku nilimkopesha mtu hata simjui amalizie ada zake za mwisho wa mwaka kwa lengo kwamba akipangiwa kitu cha kazi (ni mwalimu ataanza nilipa 50.000 kwa mwezi) mpaka atakapomaliza, tena nikamwambia akiajiriwa afanya kazi miezi 6 kwanza ajijenge ndo aanze nilipa. Nikaja ona jina lake kapangiwa kitu kanambia yupo poa, SIKUWAHI KUMSIKIA TENA TENA TENA TENA!!!!! NIMESEMAGA SITASAIDIA MTU TENA labda yule nayemwona pale anakufa njaa nimpe chakula halafu nilale mbele.

Ninafanya biashara, sasa kuna jamaa alikuwa fresh from school, akalia sana katoka Kigoma hana hata pakukaa na kupata kazi mpaka awe na wa kumshika mkono. Nikampa kazi hapo kwenye biashara yangu. Baada ya kujua biashara na kuniibia akaanza ya kwake, na kujaribu ongea na wateja wangu ahame nao kwa bei nafuu na quality ile ile (maana nilimfundisha kila kitu akawa ndo mbadala wangu nikisafiri), HILI NI funzo la pili. USISAIDIE MTU hawafai kabisa.
 
pole saana mkuu ndo maisha sio lazima ulipwe na binadamu .wala usihesabu hasara
 
Mkuu nikuheshimuye sana, utoaji ni kitu kizuri sana endapo utatoa bila kutaka mrejesho. Toa kama sadaka na unamtolea Mungu. Mimi huwa natumia ule mstari wa Biblia usemao;( loloye ulitendalo kwa neno au kwa tendo fanya kama kwa Bwana)
Ukifuatilia matokeo au alichokifanyia mwombaji utakata tamaa ya kusaidia wengine.
Ndiyo maana Agano la kale sadaka zilikuwa zinateketezwa ili mtoaji asipate nafasi ya kuzifuatilia matumizi na kuanza kunung'unika endapo zitatumika vibaya.
Kutoa ni kubarikiwa, fuatilia sana mtu yeyote mtoaji hakosi vitu/baraka bila kujali ana dini au hana, hii ni kanuni ya Kimungu..(wapeni watu vitu nanyi mtapewa kwa kipimo cha kujaa na kusukwasukwa hata kumwagika...kitabu cha Luka by Jesus)
Haina haja kufuatilia matumizi, masikini anashida nyingi, anaweza kuomba mtaji ukimpa siku hiyohiyo mwenye nyumba akaja kudai kodi so akaishia kulipa kodi au chakula.
 
Ndio maana unaweza shangaa kuna watu wanauwezo lakini hawawasaidii wanaohangaika. Inakera sana, unajitoa kwa moyo kusaidia jitu halafu linaleta ujinga. Majinga ya namna hii yako mengi na ni mzigo wa familia na taifa.

Hongera kwa kusaidia. Next time toa msaada kwa mtu uliyemchunguza na kumuona anajua maaana ya kujituma. usiache kusaidia.
 
Ukiona hivyo ujue...ushapigwa wewe... ndio maana anakuzungusha
Lakini mleta mada amesema alijitolea tu kumpiga tafu jamaa. Sidhani kama alimkopesha chochote. Kama nimeelewa vema.
 
Mkuu, betlehem nimekukubali sana, ila iwe chachu ya kuwasaidia wengine. Mimi mwenyewe nishasaidia watu wengi, lakini huyu mmoja alikuwa karibu na ofisini kwetu, maana unapoingia unamkuta, unapotoka unamkuta. Nikamuuliza ndugu yangu nikusaidieje? Akasema nikopeshe elfu50 tu, niweke sigara, pipi na maji hapa kwenye meza utaona mrejesho wake. Mimi nikampa hiyo hela, cha ajabu baada ya kumpa hata salamu akawa amesitisha, sasa sijui ni chuki, sijui imetoka wapi au anajihami katumia hela kwa mambo mengine, nimebaki kimya tu.
 
ahahaaaa aliwezesha kweli au swaga tu ?
Itakuwa aliwezesha.
Ila ujiandae akikuwezesha hata hilo rejesho lazima atafanya foloapu kujua hiyo hela umeifanyia yale yaliyokuwa yametarajiwa au umenunulia viwalo Maliedo, hahahahaha. Akikupa hakikisha zinakwenda kwa lengo tarajiwa na atakuja kukagua physically, kama ni rejesho atakwenda kwenye hiyo taasisi wanaokudai na kukagua vitabu vyao mahesabu ajiridhishe kuwa ni kweli huo mtonyo uliupeleka hapo SACCOS/VICOBA/BENKI,hahahahah usitegemee kukata ganji shost yangu
 
huyu mtu kaharibia wana jf wengine wenye nia mpuuzi sana

Kuna watu genuine wenye shida na hawatapa sababu ya mtu mmoja, ila mi nashawishika sana kwamba hawa watu haifai saidia. Tabu tu. nina maumivu sana ya kusaidia watu maishani mwangu.
 
Kuna watu genuine wenye shida na hawatapa sababu ya mtu mmoja, ila mi nashawishika sana kwamba hawa watu haifai saidia. Tabu tu. nina maumivu sana ya kusaidia watu maishani mwangu.
hilo ni tatizo ujinga tu
 
Kwakweli matapeli ni wengi sana ndugu yangu. Pole sana kwa lilokutokea, mwenyezi mungu atakurudishia kwa njia nyingine
 
Ukishasaidia ww tembea.ukitaka uone muendelezo utakutana na hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…