Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Kwanza nakupongeza kwa kuwa mstaarabu!!! maana ingekuwa mie heading ya uzi huu ingesoma hivi "MWANA JF CHIKIRA MTABARI ALIYEOMBA MTAJI KUMBE NI TAPELI"
wewe ni muungwana kwa kweli barikiwa sana
 
Kwanza nakupongeza kwa kuwa mstaarabu!!! maana ingekuwa mie heading ya uzi huu ingesoma hivi "MWANA JF CHIKIRA MTABARI ALIYEOMBA MTAJI KUMBE NI TAPELI"
wewe ni muungwana kwa kweli barikiwa sana
Hahahah, chikira shigha ki vhi chike, hanini wechikira huvho
 
Sijui ni tusi lp lnamsatahl huyo mpumbavu maana lengo lako ni jema sana. Tatizo vijana wengi tumekua sio waaminifu, waadilifu na tumeweka upgaj mbele. Kumbe lengo lako lilikua jema tena umuongezee mtaji zaidi. Hl linauma ila lisikukatishe tamaa kusaidia walio tofauti na mpumbavu huyo. Pole sn ndugu na hongera kwa moyo wako mwema hakika Mungu atakulipa kwa njia nyingine.
 
Mimi siku zote huwa nasisitiza hili kuwa, baadhi ya watu ni maskini sabb ya kutokuwa waaminifu. Huwezi kufanikiwa kama si mkweli na mwaminifu
 
Asilimia kubwa ya watanzania iko hivyo, wala sijashangaa....maneno mengi vitendo 0
 
Mkuu mtoa mada wewe ulitimiza Wajibu wako, ulifanya vile moyo wako ulivyo.....
Part yako umemaliza!!!
Usiache kusaidia wenye uhitaji sema badirisha kidogo style ya kusaidia, usije kusaidia watu ambao hawahitaji msaada!!
 
Wakuu,

Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.

Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.

Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.

Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.

Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.

Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.

Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.

Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.

Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.

My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.

Naomba kuwasilisha.


Mkuu Pole sana nitachangia baadae kuna shughuli naimalizia Katika Mchango wangu nitaongezea na Hili suala linalozagaa la watu kuhitaji Mume/Mke kumbe ni waongo ambayop kwa namna moja ama nyingine inafanana na Utapeli wa kupotezeana Muda.

Nitakuja Baadae.
 
Mkuu Pole sana nitachangia baadae kuna shughuli naimalizia Katika Mchango wangu nitaongezea na Hili suala linalozagaa la watu kuhitaji Mume/Mke kumbe ni waongo ambayop kwa namna moja ama nyingine inafanana na Utapeli wa kupotezeana Muda.

Nitakuja Baadae.
ahahaaa pole sana mbona mimi nilimpata wa rafiki yangu juzi ?
 
kumbe ni mwanamke? labda alitaka kufanya biashara na wewe na wewe ukawa huelewi. hebu na mimi naomba unifinance hichi kiproject changu nitakupa location uje anytime
Hahahahahahaha, wewe si nimesikia unamtafutia mchumba rafiki yako?
 
Back
Top Bottom