Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Ukiona hivyo ujue...ushapigwa wewe... ndio maana anakuzungusha
Kesha pigwa vp yy hakumkopesha bali alimpatia mtaji na kutaka kumuongezea kama kweli alikuwa ameanza biashara lkn kwa ujinga wake ni kama alikula hiyo pesa ss hapo nn maana yake kajipiga mwenyewe kwa upumbavu wake ni tapeli huyo hana tofauti na muhongo.
 
Wakuu,

Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.

Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.

Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.

Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.

Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.

Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.

Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.

Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.

Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.

My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.

Naomba kuwasilisha.
Pole sana na hongera kwa moyo ulionao wa kupenda kujali wengine na kutaka kuwainua
 
Itakuwa si vizuri mkuu, lengo sio kumdhalilisha bali kumpa funzo ajirekebishe na wengine wajifunze kutokana na kisa hiki.

Hapana mtaje. Ataendelea kutapeli. Wee ulicho kipata ni somo ambalo wengine wanatakiwa kujifunza. Atatapeli na wengine. Muweke waz hapa tumfahamu. Tena kwenye post ya kwanza kabisa.
 
Itakuwa si vizuri mkuu, lengo sio kumdhalilisha bali kumpa funzo ajirekebishe na wengine wajifunze kutokana na kisa hiki.
Atakuja kutapeli wengine aisee, wengi sana wanakuja pm kuomba msaada tunashindwa kuwasaidia kwa kuogopa kutapeliwa.
 
natamani kufanya hichi kibiashara lenfo kbwa ni kupandish mtaji.
kwa mtu atayekuwa tayari anisupport kupata hivi.
bench mbili ndefu, mbili fupi kiasi
meza moja ndefu futi nne na nusu na upana wake futi mbili.
kitivi kidogo kwa ajili ya wateja
mabirika manne. makubwa mawili na madogo mawili
kahawa na tangawizi
karanga mbichi na za kukaangwa
kashata
themosi nne zote mdogo
vikombe vidogo pic20
vikubwa pic 20
vikombe vya plastic saiz ya kati pic20.
asante sana
Jamani!!!!!!. Naombeni.
 
Mkuu sisi wengine hatukuiona hiyo post uliyoituma mwanzo
Tubainishie mtu huyo ni Nani? Tuchukue Tahadhari tusije ingizwa Mkenge!!!
 
Kuna jamaa nilimkuta mashambani huko iringa wakati natafuta mali ya shamba, akawa anajaza mazao kwenye magunia na kupakia kwa gari kama kibarua, jamaa alikuwa na hali ngumi sana, nikamuhuhurumia nikamleta dar, tukawa tunafanya naye biashara, nilipo mzoea zoea, nikamtuma shambani sasa aende mwenyewe akachukue mzigo maana mimi ratiba zangu zilikuwa zinabana, akaenda alipofika shambani akaniambia mazao yamepanfa bei kwa hiyo nimtumie hela ya nyongeza, nikamuongezea hela, akatoroka na hela yangu nyingi tu, mpaka wa leo hajarudi, nyumbani kwao napajua, nikiamua naenda kumkamata, lakini kila nikijiuliza nimfanye nini bado sijajua cha kumfanya, hela alihonga wanawake zikaisha, mali anayo miliki ni shati na jinsi mbili zilizotoboka.

Naomba kuwasilisha.

MKUU una huruma kama mimi naomba ujifunze mimi najifunza ka njia ngumu sn ingaa deep inside nashindwa kuacha kusaidia,hongera sn kwa hiko MUNGU AKUBARIKI
 
kuna matapeli wa aina nyingi, ingawa na wewe uli risk sana
Amewaponza na wenye shida kweli
 
Kitu ambacho ni kibaya na kinajijenga katika jamii ya kibongo ni tabia ya upigaji. Yaani sio wafanyakazi wa supermarket au kiwandani au maofisini wengi nimeona wanamawazo ya kipigaji tu, yaani wasilate mwanya. Ni muhimu kuwa na utamaduni wa kuwa na uadilifu kama nchi.
 
watu kama hao ndio wanaossababisha wenzao walio serious kukosa misaada.
 
Kitu ambacho ni kibaya na kinajijenga katika jamii ya kibongo ni tabia ya upigaji. Yaani sio wafanyakazi wa supermarket au kiwandani au maofisini wengi nimeona wanamawazo ya kipigaji tu, yaani wasilate mwanya. Ni muhimu kuwa na utamaduni wa kuwa na uadilifu kama nchi.
Yaani sijui tuna fikra za namna gani, kuna siku niliagiza kitu flani kutoka china, kwa watu nisiowajua na hata wangenipiga nisingeweza hata kuwafuatilia licha ya kuwapata, lakini cha ajabu niliwatumia hela kwa western union walikiri kupokea na muda mfupi baadae walinitumia mzigo wangu na mpaka unafika airport dar, jamaaa wananiambia mzigo uko hapo airport wahi ukauchukue usije ukarudi, nikachukua mzigo wangu na nikakuta uko vile vile kama tulivyo kubaliana.

Nilishangaa sana kwa kweli huo uaminifu, maana ingekuwa bongo, ungeshangaa tu simu haipatikani tena.
 
Mkuu uko sahihi ila shida ni kwamba kwa sababu mbali mbali ambazo ama ziko ndani au nje ya uwezo wetu, watu wote hawawezi kuajiriwa kwa sasa, na kuna watu ambao wanamaliza chuo ila wanalelewa na ndugu zao walioishia la saba wanaouza magenge tu kwa sababu ya matatizo kadha wa kadha kubwa likiwa ni kujikuta kwenye mzunguko mzito wa umasikini.

Aidha, mimi mwenyewe niliwahi kupita huko na ndio maana nakuelewa vizuri ninapowaona wenzangu wakipita huko.
mkuu, kuajiriwa sio lazima serikalini au mgodini, vijana waajiriwe hata kuuza duka, kukata kucha salon kuendesha bodaboda, ili mradi jioni anapeleka hesabu na mwisho wa mwezi anapewa jasho lake, huyu kijana angeambiwa aende kuajiriwa kufuta vumbi supermarket ungeshangaa alivyo na bidii ya kazi,
 
mkuu, kuajiriwa sio lazima serikalini au mgodini, vijana waajiriwe hata kuuza duka, kukata kucha salon kuendesha bodaboda, ili mradi jioni anapeleka hesabu na mwisho wa mwezi anapewa jasho lake, huyu kijana angeambiwa aende kuajiriwa kufuta vumbi supermarket ungeshangaa alivyo na bidii ya kazi,
Hahahaha, ila huko dukani nako wengi wao wanapenda kudokoa kweli, wewe fikiria wengine mpaka pale airport wanadokoa licha ya makamera yote yale
 
Back
Top Bottom