Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mkuu, halafu niligundua kuwa wanaume anaweza kukuambia kuwa anashida ya msingi sana, ukimuhurumia ukimsaidia, badala ya kwenda kufanya kilichokusudiwa anahonga warembo angalau apate hata kimoko

Nikafikiri wanawake wana afadhali labda wako serious kumbe nao sometimes!!!!!!!!!!!!!!!!!?
Kwa clue hii inamaanisha uliyemsaidia ni mwanamke. Na uliamini kwamba kwasababu ni wa kike hatokuwa tapeli. Haya wale wanaotaka kumfahamu endeleeni kufilter....ni ke na sio me!
 
Hujawahi kujiuliza kwanini makampuni mengi ya kibongo/africa ma manager ni wahindi/raia wa asia? ndiyo maana dangote kwenye kiwanda chake uongozi wa juu wote kaweka raia kutoka nje ya bara la africa..... Wabongo wanacho kiwaza hata shetani anaweza kula kona.... Mawazo yao ni wizi wizi tu....
 
Mkuu, Mara nyingi ukisaidia we saidia na usigeuke nyuma, mpumbavu kama huyo uliemsaidia huwa anawaza aliposimama hawazi hatua mbili mbele kuna nini, binafsi nimekerekwa maana huyo mtu hana tufauti na makalio yake, yaani mtu upoteze muda kumfuata then anakwambia umechelewa!!!!! Stupid sana, nimechelewa!!!! Huu mji umejaa matapeli, Mimi binafsi nikimsaidia mtu hata sitaki kujua au kutaka mrejesho,lkn njia ya muongo ni fupi sana
 
Binadamu haaminiki, na hawa wapuuzi ndio wanawaharibia wenzao ambao wapo serious
 
Huyo ni maskini wa akili kwa kiwango cha lami,
umempa mtaji afu anaanza kukuwekea masharti ya kwamba hajui ni kwa nini umechelewa kwenda kumtembelea, kwa haraka gani aliyonayo mpaka anakukimbia donor wake , na hawa ndiyo wanaosababisha wenye matatizo ya kweli waashindwe kusaidiwa
 
Ndiyo sababu wengine humu tunafikiria mara mbili mbili kutoa msaada kwa kuhofia kutapeliwa.

Miezi michache iliyopita kuna mtu alikuja kuandika hapa kwamba amepungukiwa pesa ya ada shuleni. Kuna bi dada mmoja mwenye roho nzuri sana humu akawasiliana naye na kumsaidia pesa za ada na pia za matumizi.

Kwa mshangao wake zikawa zinaibuka IDs mpya na nyingi hata kabla ya kuandika humu wenye ID zile wakawa wanaandika moja kwa moja kwake kuomba msaada kwa matatizo mbali mbali ya kimaisha. Machale yakamcheza ndipo akaniomba ushauri afanye nini,

Mie nikamwambia uwezekano mkubwa ni mtu yule yule anataka kuchuma zaidi toka kwake.

Kuna watu wana shida za kweli kabisa lakini kabla ya kujitoa kusaidia ni lazima mtu/watu wajiridhishe kwa kina kwamba huyu anayehitaji msaada ni kweli anahitaji msaada au ni tapeli tu.
😀 😀 😀 😀 😀 😀 😀 wabongo balaa walishamuona ni chuma ulete
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Itakuwa aliwezesha.
Ila ujiandae akikuwezesha hata hilo rejesho lazima atafanya foloapu kujua hiyo hela umeifanyia yale yaliyokuwa yametarajiwa au umenunulia viwalo Maliedo, hahahahaha. Akikupa hakikisha zinakwenda kwa lengo tarajiwa na atakuja kukagua physically, kama ni rejesho atakwenda kwenye hiyo taasisi wanaokudai na kukagua vitabu vyao mahesabu ajiridhishe kuwa ni kweli huo mtonyo uliupeleka hapo SACCOS/VICOBA/BENKI,hahahahah usitegemee kukata ganji shost yangu
we huyo Miss Natafuta sio mwenzako, juzi tu kanunua harrier mpya ya rangi ya kijivu.
 
Mkuu hakika una moyo wa kusaudia si mara moja umekuwa ukiguswa na kujitoa kwa jf members wenye uhitaji. Nakumbuka kipindi Fulani ulikuwa unatafuta mtu mwaminifu umpe kazi.

Tatizo huyo uliyemsaidia hajui nia uliyonayo. Labda ni msanii tuu au anafikiri utatake over bss from there na yeye ameshaanzisha mawazo yote hayo ni stupidification of the mind. Najua anasoma bandiko lako hapa anaweza kujirudi na kukutafuta lakini ajue jf members hawako pleased naye kwa haya anayoyatenda.
 
Na hiyo itasababisha watu wenye shida wasisaidiwe, kumbe pengine wako serious. Sema tu sisi wengine tatizo letu tuna huruma saja jambo ambalo mara nyingi hutuponza.
Najaribu kuwaza kwa umakini sana! Wahenga walisema tenda wema uondoke zako usingoje shukrani... Mkuu wala usikate tamaa endelea tu na kuwasaidia wengine.. Life is too short in this world my be kule tuendako kama kupo.. Utapata malipo yako!
 
Wakuu,

Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.

Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.

Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.

Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.

Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.

Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.

Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.

Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.

Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.

My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.

Naomba kuwasilisha.
Pole mnoo
La muhimu hajakukata mikono, yeye ataendelea kuwa masikini tuu
 
Pole Mkuu ila bado kama ulivyosema kuna watu wanna shida ila kuwatambua ni vigumu lakini akichokufanyia usiseme akioza ssmaki mmoja basis wote, ukiwa na moyo huo na Mungu kakuwezesha Fanya japo kauyafiti kadogo, wahenga walisema njia ya mwongo ni fupi, Ila huna asara mwenye asara yeye kajifungia
 
ww nawe ujielewi unampaji MTU mtaji bila kumjua anapoishi unapo Fanya jambo usikurupuke
 
Lakini mleta mada amesema alijitolea tu kumpiga tafu jamaa. Sidhani kama alimkopesha chochote. Kama nimeelewa vema.
Hata kama hajamkopesha.....

Kapigwa maana jamaa katumia ujanja wa shida kumkwapulia pesa
 
Wakuu,

Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.

Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.

Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.

Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.

Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.

Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.

Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.

Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.

Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.

My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.

Naomba kuwasilisha.
Mkuu pole Sana ila

Mkuu mtu anaekuja kwa lengo la kutaka kusaidiwa mtaji wa biashara hapewi PESA

Ataje ni biashara gani then unampa bidhaa

Hapo kidogo itasaidia

Hata mwenye njaa hununuliwa chakula si kumpa pesa
 
Back
Top Bottom