Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Mrejesho: MwanaJF aliyeomba mtaji

Shemeji ile safari ni wiki kesho, kwa hiyo niandalie makazi kabisa.
Karibu sana Mwanza. wee sema unapenda hoteli ya hadhi ipi? au hata kama unapenda kufikia nyumba za wageni za hadhi ya chini sema tu nitafanyia reservation! ili ukija ulipie mwenyewe (booking)
 
Karibu sana Mwanza. wee sema unapenda hoteli ya hadhi ipi? au hata kama unapenda kufikia nyumba za wageni za hadhi ya chini sema tu nitafanyia reservation! ili ukija ulipie mwenyewe (booking)

Ha ha ha, eti nyumba za wageni.

Nina kona yangu moja iko U-Turn, ndo huwa nafikiaga hapo.
 
Ha ha ha, eti nyumba za wageni.

Nina kona yangu moja iko U-Turn, ndo huwa nafikiaga hapo.
Ni hiyo ambayo na jina lingine lakini key holder zina jina lingine. kama ni hapo napajua, ukiwa upande wa nyuma unaona kamsitu ka mlima wa machemba (ikulu ndogo siku hizi)
 
Ni hiyo ambayo na jina lingine lakini key holder zina jina lingine. kama ni hapo napajua, ukiwa upande wa nyuma unaona kamsitu ka mlima wa machemba (ikulu ndogo siku hizi)

Hiyo hiyo, shemeji inaonekana ni mzoefu wa zile safari za natoka Mwanza naenda Mwanza!
 
Hiyo hiyo, shemeji inaonekana ni mzoefu wa zile safari za natoka Mwanza naenda Mwanza!
hahahahahaaha, huwa mara nyingi nakuwa na wageni mbalimbali ambao ni jukumu langu kuwatafutia hoteli wakija Mwanza, hahahahahahahahahahaha. hahahaahahaha. Hoteli karibia zote nazijua na bei zake. hahahahahaah. hata aina ya huduma kama ni wa karimu au ovyo ovyo nazijua. hahahahahahah, umenifanya nicheke sana shemeji eti "natoka Mwanza naenda Mwanza"
 
Alichokifanya huyu jamaa ni UNACCEPTABLE.Atasababisha watu wenye uhitaji wa kweli kushindwa kusaidiwa.
USIKUTE ALIKUWA ANAHITAJI PESA AKAOE
 
hahahahahaaha, huwa mara nyingi nakuwa na wageni mbalimbali ambao ni jukumu langu kuwatafutia hoteli wakija Mwanza, hahahahahahahahahahaha. hahahaahahaha. Hoteli karibia zote nazijua na bei zake. hahahahahaah. hata aina ya huduma kama ni wa karimu au ovyo ovyo nazijua. hahahahahahah, umenifanya nicheke sana shemeji eti "natoka Mwanza naenda Mwanza"

Unajua ulivyoweza hadi kujua funguo zina jina lingine ndo nikajua utakuwa mwenyeji pale. Maana weekend kunakuwa na wageni wengi sana wa kutoka Mwanza mpaka vyumba hupati pale.

Mimi pale napapendea vitu vinne:-

1. Bei ni nzuri, kama hawajapandisha lakini (double)
2. Breakfast wanajitahidi sana
3. Ni jirani na mahali napoenda kufanya kazi, unatembea tu
4. Usalama kwa kiasi fulani ni mkubwa
 
hahaha, mie hoteli nyingi sana nazijua mpaka vyumbani. Ninakagua vyumba kabla sijamuandalia ofisa anayekuja. Na huwa kila mgeni ana interest zake! kwa hiyo inabidi nikague kwa kina kujua kama ina kidhi vigezo vya huyo bosi mtoka mbali ninayemuandalia chumba. Ngoja niingie inbox nikuulize kitu shemeji
 
Okay hapo nimekupata shemeji.
 
Wakuu,

Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.

Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.

Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.

Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.

Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.

Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.

Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.

Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.

Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.

My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.

Naomba kuwasilisha.
cna mengi yakuongea hapa ila tu mungu akubariki sana kwa moyo huo naamini mungu atakuzidishia baraka
 
betlehem. Baraka ziendele kuja na kusukwasukwa mpaka ushangae........binadamu wengine wanaweza kukukatisha tamaa kwa jambo jema unalotenda lakini kuwa na msimamo bado kuna wanaohitaji msaada wako japo ni vigumu kuwatambua nayo ni changamoto
 
Back
Top Bottom