Wakuu,
Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.
Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.
Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.
Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.
Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.
Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.
Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.
Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.
Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.
My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.
Naomba kuwasilisha.
nipo busy shost si unajua mwisho wa mwezi marejeshoMiss Natafuta
shosti upo? sijakuona siku mbili tatu hizi shoga yangu!! au ulikuwa busy kwenye msiba wa Kitwana Kondo?
pole saana mkuu ndo maisha sio lazima ulipwe na binadamu .wala usihesabu hasaraNishapigwa laki 8 zangu huku nilimkopesha mtu hata simjui amalizie ada zake za mwisho wa mwaka kwa lengo kwamba akipangiwa kitu cha kazi (ni mwalimu ataanza nilipa 50.000 kwa mwezi) mpaka atakapomaliza, tena nikamwambia akiajiriwa afanya kazi miezi 6 kwanza ajijenge ndo aanze nilipa. Nikaja ona jina lake kapangiwa kitu kanambia yupo poa, SIKUWAHI KUMSIKIA TENA TENA TENA TENA!!!!! NIMESEMAGA SITASAIDIA MTU TENA labda yule nayemwona pale anakufa njaa nimpe chakula halafu nilale mbele.
Ninafanya biashara, sasa kuna jamaa alikuwa fresh from school, akalia sana katoka Kigoma hana hata pakukaa na kupata kazi mpaka awe na wa kumshika mkono. Nikampa kazi hapo kwenye biashara yangu. Baada ya kujua biashara na kuniibia akaanza ya kwake, na kujaribu ongea na wateja wangu ahame nao kwa bei nafuu na quality ile ile (maana nilimfundisha kila kitu akawa ndo mbadala wangu nikisafiri), HILI NI funzo la pili. USISAIDIE MTU hawafai kabisa.
Ndiyo sababu wengine humu tunafikiria mara mbili mbili kutoa msaada kwa kuhofia kutapeliwa.
Miezi michache iliyopita kuna mtu alikuja kuandika hapa kwamba amepungukiwa pesa ya ada shuleni. Kuna bi dada mmoja mwenye roho nzuri sana humu akawasiliana naye na kumsaidia pesa za ada na pia za matumizi.
Kwa mshangao wake zikawa zinaibuka IDs mpya na nyingi hata kabla ya kuandika humu wenye ID zile wakawa wanaandika moja kwa moja kwake kuomba msaada kwa matatizo mbali mbali ya kimaisha. Machale yakamcheza ndipo akaniomba ushauri afanye nini,
Mie nikamwambia uwezekano mkubwa ni mtu yule yule anataka kuchuma zaidi toka kwake.
Kuna watu wana shida za kweli kabisa lakini kabla ya kujitoa kusaidia ni lazima mtu/watu wajiridhishe kwa kina kwamba huyu anayehitaji msaada ni kweli anahitaji msaada au ni tapeli tu.
Ongea kwa unyenyekevu na betlehem akuwezeshe, hahahahahaahahah.nipo busy shost si unajua mwisho wa mwezi marejesho
ahahaaaa aliwezesha kweli au swaga tu ?Ongea kwa unyenyekevu na betlehem akuwezeshe, hahahahahaahahah.
Lakini mleta mada amesema alijitolea tu kumpiga tafu jamaa. Sidhani kama alimkopesha chochote. Kama nimeelewa vema.Ukiona hivyo ujue...ushapigwa wewe... ndio maana anakuzungusha
Mkuu, betlehem nimekukubali sana, ila iwe chachu ya kuwasaidia wengine. Mimi mwenyewe nishasaidia watu wengi, lakini huyu mmoja alikuwa karibu na ofisini kwetu, maana unapoingia unamkuta, unapotoka unamkuta. Nikamuuliza ndugu yangu nikusaidieje? Akasema nikopeshe elfu50 tu, niweke sigara, pipi na maji hapa kwenye meza utaona mrejesho wake. Mimi nikampa hiyo hela, cha ajabu baada ya kumpa hata salamu akawa amesitisha, sasa sijui ni chuki, sijui imetoka wapi au anajihami katumia hela kwa mambo mengine, nimebaki kimya tu.Wakuu,
Kuna mwana jf alijitokeza humu akiomba wana jf tumsaidie mtaji kidogo aanzishe biashara baada ya kumaliza chuo, kukosa ajira na kushindwa kuanzisha mradi wowote kutokana na kukosa mtaji.
Kutokana na alivyokuwa anajieleza, na kwa kuwa mara nyingi nimekuwa nikihamasisha kuwa tujenge utamaduni wa kisaidiana, nilijikuta nikishawishika kumsaidia mtaji. Hata hivyo, kwa makusudi, sikumpatia kiasi chote alichokiwa akihitaji, bali nilimpatia kama 80% na kumueleza kuwa aanze kidogo kidogo halafu mbele ya safari tuone maaendeleo ya biashara kwanza. Lengo langu lilikuwa ni ili nimsome kwanza na kimuelewa ni mtu wa namna gani na yuko commited kiasi gani.
Basi nikamtumia hiyo hela na akanieleza kuwa kashafungua biashara na inaendelea vizuri kwa kuwa bado ni ndogo. Kwa kuwa alieleza kuwa yeye yuko dsm na mimi niko mkoani, nilimueleza kuwa, nitakapokuja dsm, ningeenda kuona biashara yake inavyoendelea.
Baada ya muda, nikaenda dsm, nilikuwa na mambo mengi na muda kidogo wa kukaa dsm lakini nikaona pia ingekuwa vyema nikamuona na kuhakikisha kama kweli alianzisha biashara.
Nilipofika dsm, nikampigia kumjulisha kuwa niko dsm na ningependa kumtembelea.Akanielekeza biashara ilipo ila nilipotaka kwenda akawa anatoa dharura mbali mbali. Muda wangu ukaisha nikaondoka dar.
Mara ya pili nilivyorudi dar, bikampigia tena, akaniambia niende mpaka eneo flani, nikifika hapo nimjulishe maana biashara yake ilipo nikaribu na hapo.
Nikaenda mpaka aliponielekeza, nilipofika ilikuwa ni jioni hivi kwenye saa kumi na mbili na robo.Nilivyomueleza kuwa nimefika, akaniambia nilikuwa nimechelewa, hivyo nisingeza kumuona na anashindwa kuelewa ni kwa sababu gani nilichelewa kiasi hicho.
Nikashikwa na hasira, lakini nikakumbuka moja ya vitu vyenye hasara tu na visivyona faida ni hasira.Nikakumbuka madhara ya hasira kwenye afya ya binadamu, nikageuka kulia na kushoto, nikatabasamu. Mbele kama hatua tano hivi nikaona duka, nikasogea hadi dukani, nikaagiza pepsi yenye ubaridi karibu kuganda. Nikaimiminia mdomoni karibu nusu.Ingawa nilishaelezwa kuwa kiafya kuwa pepsi si nzuri, nilipata burudani iliyokaribiana na ile iliyomfanya wakili mashuhuri ajiuzulu nafasi zake zote. Nikachukua boda na kutoweka eneo lile.
Lengo kuu la kwenda kumuona mwana jf huyo, lilikuwa ni kuhakikisha kuwa kama kweli ameanzisha biashara na yuko serious, nifanye mpango wa kumuongezea kamtaji kwa vile ambavyoingewezekana. Haina maana kuwa nina uwezo mkubwa, bali lengo ni katika jitihada tu za kuungana mkono kwa kuwa sisi sote ni binadamu na ni vizuri kusaidiana.Lakini mpaka naandika uzi huu, sijamuona muhusika wala sijaona biashara iliyoanzishwa na kuzinguliwa nimezinguliwa vile vile.
My take.
Kuna watanzania wanaishi kwenye hali ngumu sana ya kimaisha kutokana na kutokujitambua na ujinga, wengine kwa sababu ya kiburi na dharau.Hawa wataendelea hivyo hivyo tu hamna namna ya kuwatoa hapo mpaka wenyewe waamue tu kubadilika. Hata hivyo kuna wengine wamekwama kama sehemu ya mitihani ya maisha na tukisaidiana wanaweza kuwa watu waliofanikiwa sana.Hata hivyo changamoto kubwa ni kwenye kujua yupi ni yupi.
Naomba kuwasilisha.
Itakuwa aliwezesha.ahahaaaa aliwezesha kweli au swaga tu ?
huyu mtu kaharibia wana jf wengine wenye nia mpuuzi sana
hilo ni tatizo ujinga tuKuna watu genuine wenye shida na hawatapa sababu ya mtu mmoja, ila mi nashawishika sana kwamba hawa watu haifai saidia. Tabu tu. nina maumivu sana ya kusaidia watu maishani mwangu.
kwani alitoa sh ngapi jamani? maana hela ingine ya kula tuhuyu mtu kaharibia wana jf wengine wenye nia mpuuzi sana
duh laki mbili labdakwani alitoa sh ngapi jamani? maana hela ingine ya kula tu