Mkuu nao, nathamini mawazo yako..lakini ukirejea kwenye Uzi wa awali.. Bi dada huyu anasema wazi kwamba mumewe alikiri kosa kinyooonge kabisa.. Sasa ni muhimu pia kukumbuka kwamba hii stori ni one-sided.. Laiti tungemsikia mumewe pia...naamini wengi msingekuwa the same anymore..
Mimi naona Huyu Bi dada anaeleza kwa kufukia mapungufu yake binafsi na kufukua ya mwenzie... Sidhani kama huyo mme ni kichaa kiasi cha kureact vibaya kwenye kikao cha pili wakati kikao cha kwanza alikuwa mpole na akakiri kosa..(probably aliapologize pia)...lazima kuna kitu nyuma ya pazia huyu bi-dada hakisemi...
Pia, lazima huyu dada azingatie aina ya jamii tuliyonayo..asingepaswa kutegemea ati mumewe naye atamuomba msamaha Mara kumi kumi kama mdogo wake.
NB: Kumbuka Huyu mdada ndo aligoma kumzalia mumewe mpaka asome masters yake amalize.