Habari zenu wadau wa MMU,
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru mods na members wenzangu wote kwa mawazo, ushauri na michango yenu katika thread niliyoleta huku kipindi cha nyuma yenye kichwa kisemacho "mume wangu amempa mimba mdogo wangu"
Nimepata muda wa kutosha kutafakari michango ya mawazo yenu namna ya kumaliza tatizo hili na MUNGU amekuwa upande wangu na nimefanikiwa kufikia muafaka.
Jana ndo ilikuwa siku ya kukutana tena kwenye kikao pamoja na wazazi wa pande zote mbili na safari hii tukihusisha na wachungaji wetu na tulikaa na kufikia muafaka kama ifuatavyo;
Katika kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kutoka kwangu na kwa watuhumiwa, mume wangu aliamua kujibu vibaya kikao baada ya kuona anaandamwa na maswali ambayo haya kumfurahisha.
Nasikitika kusema alidiriki kujibu kuwa kama kosa limeshatokea waamue haraka yeye ana mambo ya muhimu ya kufanya kuliko hili.
Akaenda mbali zaidi kuwa hata wao wanajiona ni watakatifu kumuandama na maswali wana nyumba ndogo kibao sema ni kwa vile hawaja kamatwa. Pamoja nahayo akaongeza kuwa hajawahi jutia kosa lake kwani yule si dada yake wala hana ukoo nae kwahiyo ilikuwa ni sawa tu.
Wazazi wake walijaribu kumkatisha asiendelee kuzungumza lkn hakujali akapaza sauti zaid hapo ikabidi wamuache tu aongee mpaka amalize, aliongea mengi na magumu sana sina ujasiri wa kuyaandika hapa kwakuwa hayatamkiki kwa mtu mwenye akili timamu.
Baada ya kumsikiliza kikao kiliniuliza nasemaje kuhusu ndoa yangu.
Sikuwa na la zaidi, niliwaambia kwakuwa kwake ni jambo la kawaida sana na mimi kwangu si la kawaida nisingeweza kuendelea kuishi na mtu mwenye mtazamo tofauti.
Wachungaji walisema wao hawana mamlaka ya kuvunja ndoa ya kikristo lakini kwakuwa mwanaume ameongea maneno yenye dharau inaonesha hana moyo wa toba na angeendelea na uzinzi hivyo wanaungana na mimi katika maamuzi yangu.
Walinishauri nifuate taratibu za kisheria kuvunja ndoa.
Kwa upande wa mdogo wangu yeye alishanifuata zaidi ya Mara kumi kuniomba msamaha, sikuona sababu ya kutomsamehe nilimsamehe na jana niliuthibitisha msamaha wangu katika kikao lakini nilimtahadharisha kutoendelea na shemeji yake nae hakupingana nami katika hilo.
Mwanaume ameanza vitisho kwamba nijiandae kupambana.
Binafsi siogopi nipo tayari kupambana lakini sipo tayari kuendelea kuishi na mwanaume fedhuli kama yeye.
Hapo ndipo tulipo fikia na najiandaa kutafuta talaka kisheria.
Asanteni sana naamini hili limepita imebaki utekelezaji wa utenguzi wa ndoa.
Nakaribisha michango yenu ya mawazo..
Pia niwashukuru kwa kampani yenu katika kipindi kigumu
dada leah pole sana, mwanzo wa hii story sikuwa makin maana, nliona tu ni story, ila baada ya mrejesho kunajambo nichangie,
ndoa ni taasisi pekee dunian yenye kila aina ya changamoto, uzr ni kuwa inawahusisha watu 2, waliokubaliana kwa pamoja kuwa wataishi pamoja wakiwa wanalala bila nguo, ila mchana wanavaa nguo na kuendelea na kazi.. biblia inasema mwanamke na mwanaume wataondoka kwao na kuambatana nao watakuwa mwili mmoja
sasa mdogo wako, ambae ni ndugu yako kabisa, baada ya lile tukio, kosa la kwanza ulilofanya, ni kui expose hyo isu, kabla ya kuifanyia kazi, maana mwisho wa siku ulijua matokeo kuwa hata kama itakuwaje hutobadili ukwel kuwa mme wako kampa mimba mdogo wako..
nmemuuliza mke wangu, hli jambo kanijib kwa lugha rahis sana, kuwa atakachofanya ni kumchukua mdogo mtu na kumrudisha nyumbani na yy ndiye atakaesema kuwa hyo mimba ni ya nani...
sina uhakika kama lilikuwa jib zr ila nahisi lingekuwa pia kwako, ndoa haina mbadala ktk din ya kikiristo, hakuna siku utasema et upate taraka kwa kuwa unataka kuwa huru,
jenga NENO MSAMAHA, HATA KAMA NI KOSA KUBWA KIASI GANI, MUNGU AMESEMA ASIYE WEZA KUMSAMEHE MTU HATA YEYE HAWEZI KUSAMEHEWA, KWA HYO KAMA UNATAKA AMANI MSIME VZR YESU, JIFUNZE UPENDO WAKE,TAFAKARI KISHA MUULIZE JE NI HARARI KUMUACHA MMEO KWA KOSA HILO?
kwa kuwa tumekusikiliza upande wako pekee na kwa kuwa kesi yako haina maon kutoka kwa mme wako, yatosha kusema ndoa haivunjwi au haibatilishwi na Mahakama, ila ni Mungu mwenyewe,
mwisho, bado nakushauri kama unahis kuwa umekwazwa sana, jitenge na mme wako hata kwa mwaka 1 tafakari pekee yako, fanya kazi zako, naamin ukipata mda mzr utaamua vzr, kujitenga na mme anu mke ni kanunu ya biblia ila shart ni moja usiwe na mme/mwanaume au mpenzi kwa kipindi chote, ukipata ham rudi kwa mmeo...
zingatia hutopata amani hata kama utapata taraka, ni aheri kutafuta Amani ndani ya ndoa kuliko kutafuta Aman nje ya ndoa..... ninachokuambia ni kwali na hakika, ukiweza kanuni hii itakusaidia kuwa na AMANI YA KWELI SI BANDIA