Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Mrejesho: Mume wangu amempa mimba mdogo wangu

Kuna ndoa nimesuruhisha last week kama kiongoz wa kanisa na kwa kweli wanaume tuna shida kubwa sana ujeuri, majigambo na dharau. Mama endelea na maisha yako, ni bht mbaya tu ndoto hazijatimia, si wewe wa kwanza wako wengi hata huyu niliye mshauri wanavunja ndoa yao mwezi ujao.

Pole sana Mungu akusaidie
 
There is some thing hidden behind Dada yangu. Issue ya kusikiliza upande mmoja ni ngumu kujua siwezi jua bt akili inagoma kuwa upande wa pili haukuomba samahani navyoelewa uliomba sema haukupewa nafasi. And then hio samahani aliyo ipa base ni ile ya ukingoni wakati washajua kosa lipo wapi na kila kitu kinajulikana. BT ungekuwa tumepata maelezo ya pande zote mbili tungejua.
Basi usimhukumu pia huyu dada subiri upande wa pili ndo utoe hukumu sahihi.
 
Pole sana Dada angu kiukweli mmeo kaonyesha zarau kubwa nakupongeza kwa uamuzi uliofikia mungu akusaidie sana upate chaguo jingine lililo sahihi usimuogope kwa vitisho vyake kwani no one who is above the law .
 
Pole sana Dada angu kiukweli mmeo kaonyesha zarau kubwa nakupongeza kwa uamuzi uliofikia mungu akusaidie sana upate chaguo jingine lililo sahihi usimuogope kwa vitisho vyake kwani no one who is above the law .

Jifunze kuandika Mungu na sio mungu
 
Nawaza tu!! Laiti angekubali kosa na kuomba msamaha ungekubali kuendelea nae
 
Ukiyasoma mambo kama haya ndiyo unajuwa uzuri wa Uislam.

Kiislam hapo ungemlamba yeye talaka.
 
Hiyo ni story ya upande mmoja
Kama Mr wako angekuja humu kujitetea, wengi tungeweza kubadirisha hukumu na wewe kuwa mwenye hatia.

Kuita ndugu zako/zake na wachungaji ni kosa kubwa ambalo siku ukituliza akili utanielewa ninachokisema hapa.

Siku hizi kina dada hasa hawa waliokaa darasani kidogo ni shida ktk mahusiano..kelele/ujuaji/ ligi nyingi ndani ya nyumba bila kujua ndio chanzo cha matatizo makubwa zaidi ndani ya mahusiano/ndoa.
Kweli mkuu, mimi binafsi wife tunalumbana sana kuhusu haki ya kindoa, anadai ana majukumu mengi sana, mara hajisikii, oooh mara hivi ooo mara hiki na kile ili mradi tu awe na sababu. Inaweza kupita hata wiki hatujashiriki. Siku mmoja niliwahi mwambia hivi unadhani kunifanyia hivi mwisho wake ni nini? Nani atalaumiwa iwapo nikiamua kwenda kutafuta haki hiyo nje ya ndoa. Huko nje wako wengi sana wanaojilengesha kwangu wengine ni watu wako wa karibu sana lakini nafanya jitihada za kuwekwepa ili nikutunzie heshima. Nikamuuliza au pengine siko moyoni mwako? Mwishoni nikamwambia sasa mimi sitahangaika tena kukutongoza wakati wapo watu wanaojitongozesha kwangu.
Alilia sana lakini mimi nikamwambia haisaidii kama hubadiliki unajua kabisa nakupenda na kukuheshimu lakini unakutumia vibaya huko kupendwa na kuheshimiwa.
Tangu nimemwabia hivyo amebadilika, ameanza kutoa ushirikiano ninapohitaji. Sasa sijui kama ni nguvu ya soda au la.
 
Ndio maana nilisema Mume wa mleta mada akijitetea tunaweza kujua mzani uta balance vipi.

Kifupi inawezekana mleta mada alikwenda kuongeza shahada wiki moja baada ya kuolewa na kumuacha mdogo wake wa kike hapohapo.

Hata ningekuwa mimi.....................
 
Kweli mkuu, mimi binafsi wife tunalumbana sana kuhusu haki ya kindoa, anadai ana majukumu mengi sana, mara hajisikii, oooh mara hivi ooo mara hiki na kile ili mradi tu awe na sababu. Inaweza kupita hata wiki hatujashiriki. Siku mmoja niliwahi mwambia hivi unadhani kunifanyia hivi mwisho wake ni nini? Nani atalaumiwa iwapo nikiamua kwenda kutafuta haki hiyo nje ya ndoa. Huko nje wako wengi sana wanaojilengesha kwangu wengine ni watu wako wa karibu sana lakini nafanya jitihada za kuwekwepa ili nikutunzie heshima. Nikamuuliza au pengine siko moyoni mwako? Mwishoni nikamwambia sasa mimi sitahangaika tena kukutongoza wakati wapo watu wanaojitongozesha kwangu.
Alilia sana lakini mimi nikamwambia haisaidii kama hubadiliki unajua kabisa nakupenda na kukuheshimu lakini unakutumia vibaya huko kupendwa na kuheshimiwa.
Tangu nimemwabia hivyo amebadilika, ameanza kutoa ushirikiano ninapohitaji. Sasa sijui kama ni nguvu ya soda au la.

Bora wewe uliamua kuvunja ukimya bila kukimbilia nyumba ndogo, si unaona amebadilika sasa
 
Habari zenu wadau wa MMU,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru mods na members wenzangu wote kwa mawazo, ushauri na michango yenu katika thread niliyoleta huku kipindi cha nyuma yenye kichwa kisemacho "mume wangu amempa mimba mdogo wangu"

Nimepata muda wa kutosha kutafakari michango ya mawazo yenu namna ya kumaliza tatizo hili na MUNGU amekuwa upande wangu na nimefanikiwa kufikia muafaka.

Jana ndo ilikuwa siku ya kukutana tena kwenye kikao pamoja na wazazi wa pande zote mbili na safari hii tukihusisha na wachungaji wetu na tulikaa na kufikia muafaka kama ifuatavyo;

Katika kusikiliza maelezo ya pande zote mbili yaani kutoka kwangu na kwa watuhumiwa, mume wangu aliamua kujibu vibaya kikao baada ya kuona anaandamwa na maswali ambayo haya kumfurahisha.

Nasikitika kusema alidiriki kujibu kuwa kama kosa limeshatokea waamue haraka yeye ana mambo ya muhimu ya kufanya kuliko hili.

Akaenda mbali zaidi kuwa hata wao wanajiona ni watakatifu kumuandama na maswali wana nyumba ndogo kibao sema ni kwa vile hawaja kamatwa. Pamoja nahayo akaongeza kuwa hajawahi jutia kosa lake kwani yule si dada yake wala hana ukoo nae kwahiyo ilikuwa ni sawa tu.

Wazazi wake walijaribu kumkatisha asiendelee kuzungumza lkn hakujali akapaza sauti zaid hapo ikabidi wamuache tu aongee mpaka amalize, aliongea mengi na magumu sana sina ujasiri wa kuyaandika hapa kwakuwa hayatamkiki kwa mtu mwenye akili timamu.

Baada ya kumsikiliza kikao kiliniuliza nasemaje kuhusu ndoa yangu.

Sikuwa na la zaidi, niliwaambia kwakuwa kwake ni jambo la kawaida sana na mimi kwangu si la kawaida nisingeweza kuendelea kuishi na mtu mwenye mtazamo tofauti.

Wachungaji walisema wao hawana mamlaka ya kuvunja ndoa ya kikristo lakini kwakuwa mwanaume ameongea maneno yenye dharau inaonesha hana moyo wa toba na angeendelea na uzinzi hivyo wanaungana na mimi katika maamuzi yangu.
Walinishauri nifuate taratibu za kisheria kuvunja ndoa.

Kwa upande wa mdogo wangu yeye alishanifuata zaidi ya Mara kumi kuniomba msamaha, sikuona sababu ya kutomsamehe nilimsamehe na jana niliuthibitisha msamaha wangu katika kikao lakini nilimtahadharisha kutoendelea na shemeji yake nae hakupingana nami katika hilo.

Mwanaume ameanza vitisho kwamba nijiandae kupambana.
Binafsi siogopi nipo tayari kupambana lakini sipo tayari kuendelea kuishi na mwanaume fedhuli kama yeye.

Hapo ndipo tulipo fikia na najiandaa kutafuta talaka kisheria.

Asanteni sana naamini hili limepita imebaki utekelezaji wa utenguzi wa ndoa.

Nakaribisha michango yenu ya mawazo..

Pia niwashukuru kwa kampani yenu katika kipindi kigumu
Nafasi ikiwa wazi nipo tayari kuziba hilo pengo naahidi kuwa muaminifu kwako
 
Dada mwenyewe ana sura ya upole mkarimu na anaonekana ana mapenzi ya dhati kabisa. Pole mdogo wangu usijali kila kitu hutokea kwa sababu. Pengine kupitia kwa msara huu watu wengi wamejifunza na kupata majibu, watu wengi wamepata majibu ya matatizo yao, hata wewe kuna kitu umefunguliwa. Uwe na amani sasa ikiwezekana tafuta mradi mkubwa wa kuwekeza uanze kuutekeleza utasaidia kukuweka busy na itakuwa rahisi kusahau yaliyopita.
 
Basi kama ulifuatiilia Uzi toka mwanzo nafikiri pia hukuuelewa,Huu jamaa hajawahi kuomba msamaha toka mwanzo,
Pili watu walioalikwa ni wazazi wa pande zote mbili yaani wazazi wake Na mwanaume,mwanamke, Na wachungaji waliofungisha ndoa yao ni Nani tena unafikiri angeweza kumshawishi huyu MTU??
Iwapo wazazi wake,Na wazazi wa mkewe pia walezi wake wa rohoni kawavunjia heshima kwakuwambia hata wao wana nyumba ndogo pengine unafikiri huyu bwana yuko sawasawa?
Hapana usimtete kwa kua ni mwanaume huyu akili yake haiko sawasawa angekua mwingine toka mwanzo wa hii inshu angekua ni mtu wakujutia kile alichofanya kwa kuomba msamaha kwa idadi isihesabika.
Ona mdogo mtu pamoja Na huo uovu aliomtendea dadake lakini tunaambiwa kamfuata dadake zaidi ya Mara kumi kwenda kuomba msamaha Huu ndo ungwana hata mtu una shawishika kusamehe.
Mkuu nao, nathamini mawazo yako..lakini ukirejea kwenye Uzi wa awali.. Bi dada huyu anasema wazi kwamba mumewe alikiri kosa kinyooonge kabisa.. Sasa ni muhimu pia kukumbuka kwamba hii stori ni one-sided.. Laiti tungemsikia mumewe pia...naamini wengi msingekuwa the same anymore..
Mimi naona Huyu Bi dada anaeleza kwa kufukia mapungufu yake binafsi na kufukua ya mwenzie... Sidhani kama huyo mme ni kichaa kiasi cha kureact vibaya kwenye kikao cha pili wakati kikao cha kwanza alikuwa mpole na akakiri kosa..(probably aliapologize pia)...lazima kuna kitu nyuma ya pazia huyu bi-dada hakisemi...
Pia, lazima huyu dada azingatie aina ya jamii tuliyonayo..asingepaswa kutegemea ati mumewe naye atamuomba msamaha Mara kumi kumi kama mdogo wake.
NB: Kumbuka Huyu mdada ndo aligoma kumzalia mumewe mpaka asome masters yake amalize.
 
mimi nilikwambia wewe, pia utakuwa na shida usije rudia kosa ukipata mme mwinginwe habari za kusema ohooo,subiri mpaka nimalize mastaz, au subiri mpaka nimalize siku zangu, mtu anachepuka mwishowe unalia tena, unapoingia kwenye atua fulani jipange kuitumikia.
 
Sasa mlikua mnaamuliza nini wakati ukweli wote mnaujua na yeye ni mkosaji mkubwa. Tayari ameshaathirika kisaikolojia mme wako huyo. Atajibu anavojisikia koz anaona dunia iko agaist yake. Mmekosea kweli kuweka kikao cha kumuuliza tena. Mngemwacha akae mwishowe angejutia na kuja kuomba samahani mwenyeww
Ni kweli wangemuacha tu
 
Back
Top Bottom