Kwanza nianze kuwatakia heri ya Mwaka Mpya.
Mwishoni mwa mwaka jana nilikuja na mada niliyoita Ushauri: Mke wangu anapenda maisha ya matawi ya juu
Nashukuru wadau kwa michango yao mazuri.
Kifupi ni kuwa nilikubaliana naye tukasafiri kwenda mapumziko Zanzibar kwenye hoteli alizokuwa ameona ndo "size" yetu kukaa. Pesa ilinitoka kweli lakini nilivumilia machungu hayo.
Wakati wa mapumziko hayo tulitenga muda wa kutafakari malengo tuliyojiwekea kwa mwaka 2016 na kwa kiwango gani tumeweza kuzifikia. Vilevile kwenye tulizungumzia mipango kwa 2017.
Hivyo pamoja na mambo mengine, tumekubaliana kuwa kuanzia mwaka 2017 Kipato changu na faida inazopatikana kwenye biashara yetu itatumika kuangalia usitawi wa maendeleo ya familia ikiwemo kujenga nyumba za kupangisha kwenye kiwanja chetu kile. Pili, pesa za "kula bata" na kwenda next mapumziko kama itakuwa nje ya Dar zitatoka kwenye akiba yake (mshahara wake).
Tuliongea mengi na kimsingi nimeandaa kabisa muktasari wa kikao na maamuzi. Hivyo akitaka tena kwenda sijui Dubai, Comoro natoa muktasari wa kikao na kumuuliza ameshajiandaa kiasi gani.
Nimalizie kuwashukuru wadau na tuendee kusaidiana kimawazo hapa jukwaani.