Mrejesho: Manunuzi ya mtandaoni (ebay)

Mr. MTUI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
8,130
8,351
Ukatumwa tarehe 16 na leo umefika..

NILICHOJIFUNZA

1. Wakati mwingine woga wetu ndio unaotufanya kuwa nyuma kimaendeleo.. Dunia ya sasa imekua kijiji unaweza pata bidhaa yeyote toka ulimwengu wowotena kwa bei rahisi cha msingi ni kutumia njia sahihi wakati wa manunuzi..

2. Wizi wa pesa kwenye acount.. Kuna wakati nilikua na wasi wasi kwamba uenda jamaa wangenipiga ela zangu kwenye acount.. Hii si kweli jamaa wa ebay wapo makini sana hasa hasa ukiwa na acount ya paypal yani chagua bidhaa ebay lakini lipa kwa kutumia paypal..
Kuna jamaa mmoja alikweka bidhaa kiwizi wizi nikainunua jamaa wa paypal walipogundua wakamblock jamaa na fedha zangu zikarudishwa kwenye acount yangu.. Haijalishi ni kiasi gani kitarudishwa..

View attachment 489334
KUHUSU ZIP CODE NA POSTAL CODE

Hizi zisiwasumbue.. Andika detail zako za nchi, mkoa na wilaya, na code yetu pendwa ya +255 plus jina lako kamili trust me mzigo wako utafikishwa posta kuu ya mkoa wako na watu wa posta watakupigia simu uufate mzigo wako mara unapofika.. Hasa wakituma kwa register..

Usiandike P. O. BOX kwani wengine huwa hawataki mtu atumie P. O. Box.

2. Kuna vingine vingi ambavyo ukiwa interested unaweza jifunza cha msingi tuache woga.
 
Mie bado nina magutugutu ya kununua mtandaoni kutokana na watu kulizwa. Kuna jamaa yangu alinunua viatu vizuri sana vya kiume kwa 10% ya bei ya dukani lakini mie bado machale hayajatulia lakini niko tayari kujaribu siku chache zijazo za usoni.
 
Usipokuwa makini utalizwa hackers wapo.. Na kuna njia ya kuwatambua... Mara nyingi hacker wanakutumia email zinazofanana na za ebay na link link za ajabu ukizifungua hzo link ndo mwanzo wa kuibiwa.. Ebay hawatumi email zenye link au attachments.. Mfano hii hapa ni email ya hacker
1490979000108.jpg

Hyo @ kabla ya ebay inaonyesha kwamba imetoka kwa hacker.
 
Kwahiyo hakuna haja ya kuwa na PO BOX HATA KAMA MZIGO WAKO UTASAFIRISHWA KWA POSTA ?
 
Yah... Wengine hawataki kabisa mambo ya p. O. Box.. Andika nchi na mkoa na wilaya.. Na ile zip ckde +255 mzigo unafika.
UNAFIKA WAPI NA UTAJUAJE AU NITATAKIWA KUANDIKA NAMBA YA SIMU BADALA YA PO BOX ?
 
UNAFIKA WAPI NA UTAJUAJE AU NITATAKIWA KUANDIKA NAMBA YA SIMU BADALA YA PO BOX ?
Ukiregister acount yako ya ebay utaweka namba ya simu ambayo wataitumia wakati wa kutuma mmzigo.. Wakikutumia mzigo wako wataweka namba yako ya simu ambayo itatumiwa na watu wa posta kukutafuta..
 
Hivi ni kuanzia bidhaa ya bei gani ndio unaweza daiwa kodi? au kwa njia ya posta hukutani na watu wa kodi?
 
Ukiregister acount yako ya ebay utaweka namba ya simu ambayo wataitumia wakati wa kutuma mmzigo.. Wakikutumia mzigo wako wataweka namba yako ya simu ambayo itatumiwa na watu wa posta kukutafuta..
Shukhrani sana
 
Back
Top Bottom