Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Nacherewa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
285
Reaction score
457
Habari za mchana wapendwa

Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Jamii Forum na members mliotoa michango yenu. Nimeona si vizuri kukaa kimya bila kuleta mrejesho wa kinachoendelea kwenye kesi yangu ya ndoa. Kwa wale ambao hamkuweza kufatilia hii post yangu mnaweza kusoma hapa https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/876139-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.html na https://www.jamiiforums.com/mahusia...-mrejesho-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.html

Baada ya kufungua kesi mahakamani yeye alikimbilia BAKWATA ila mahakama ikanishauri nikawasikilize watasemaje huku kesi ya msingi ikiwa inaendelea mahakamani. BAKWATA wakajitahidi kusuluhisha ikashindikana, upande wa familia yake ikasema wao hawako tayari hili suala lirudi nyumbani na upande wa kwangu vilevile na mimi sikuwa tayari kurudiana na huyu mwanaume kwani alikuwa tayari amehamia kwa hilo jimama lake na nyumba akapangisha.

Baada ya vikao vitatu BAKWATA huyu mwanaume akaomba nimrejeshee mahari yake nami nikafanya hivyo na nikapewa barua ya kupeleka mahakamani ikieleza kwamba usuluhishi umeshindikana na mwanaume kaomba arejeshewe mahari yake hivyo kwa sheria za kiislam hamna ndoa tena.

Barua ilisomwa mahakamani na hakimu akamuuliza je pingamizi la madai ya talaka akakaa kimya baade ikabidi akubali kwani ndoa ilikuwa kiini macho tu. Nikaambiwa nitaje kama kuna mali tulizochuma wote nikazitaja, kubwa ilikuwa ni nyumba ila yeye akajitetea kuwa nyumba niliikuta wakati naolewa na sikufanya marekebisho yoyote ambavyo si kweli.

Nikaelezea kwamba tulipo oana nyumba ilikuwa imepandishwa tu na kupigwa bati vilivyobaki tulimalizia kama wana ndoa na ushahidi upo. Tarehe 15 Decemba tunaleta mashahidi wa nyumba ambao nimeshawapata na vielelezo vipo vya kutosha. Pia tulipo oana tulikuwa tumepanga kwani nyumba ilikuwa bado kabisa kuisha na tulimalizia kwa makubaliano.

Sasa ivi na kwa yule mwanamke amefukuzwa yupo tu mtaani kwani nyumba alishapangisha bila hata idhini yangu. Yule mwanamke alimpigia baba mkwe (alitafuta namba hadi akaipata) na kumuelezea kwamba kwanza hampi matumizi toka aanze kuishi naye na pia alimdanganya kama hajaoa na mengine kibao ndio maana kaamua kumfukuza kwani anweza kuimfanyia kama alivyonifanyia mimi.

Nashukuru sana kwa kuwa wakwe zangu wapo pamoja na mimi kwani wananipenda na kuniheshimu

Gari yangu iko polisi kwa usalama zaidi mpaka hapo uamuzi wa mahakama utakavyotoka

Shukrani nawasilisha

Nacherewa
 
pole sana kwa yaliyokukuta hakika chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho fanya kazi maisha yaendelee....ipo siku atakutafuta na kukuomba msamaha
 
Haya wachepukaji...mjifunze..maana hapo mchepuko kasomaa ramani hamana kitu hapo!
 
Kwann iyo nyumba mliimlizia kwa makubaliano! Hii ndoa ilishavunjika tangu mlipoanza kuwekeana makubaliano. Mwanamke akishakolezwa na kipindi cha wanawake live, ni shida tupu.
 
Pole ningekuwa mimi ningeachana na madai tu ya mali Mungu atakusaidia utavuna vingine vingi. Be careful asikutegeshee majambazi
 
Habari za mchana wapendwa

Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Jamii Forum na members mliotoa michango yenu. Nimeona si vizuri kukaa kimya bila kuleta mrejesho wa kinachoendelea kwenye kesi yangu ya ndoa. Kwa wale ambao hamkuweza kufatilia hii post yangu mnaweza kusoma hapa https://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/876139-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.html na https://www.jamiiforums.com/mahusia...-mrejesho-maneno-ya-kejeli-ya-mume-wangu.html

Baada ya kufungua kesi mahakamani yeye alikimbilia BAKWATA ila mahakama ikanishauri nikawasikilize watasemaje huku kesi ya msingi ikiwa inaendelea mahakamani. BAKWATA wakajitahidi kusuluhisha ikashindikana, upande wa familia yake ikasema wao hawako tayari hili suala lirudi nyumbani na upande wa kwangu vilevile na mimi sikuwa tayari kurudiana na huyu mwanaume kwani alikuwa tayari amehamia kwa hilo jimama lake na nyumba akapangisha.

Baada ya vikao vitatu BAKWATA huyu mwanaume akaomba nimrejeshee mahari yake nami nikafanya hivyo na nikapewa barua ya kupeleka mahakamani ikieleza kwamba usuluhishi umeshindikana na mwanaume kaomba arejeshewe mahari yake hivyo kwa sheria za kiislam hamna ndoa tena.

Barua ilisomwa mahakamani na hakimu akamuuliza je pingamizi la madai ya talaka akakaa kimya baade ikabidi akubali kwani ndoa ilikuwa kiini macho tu. Nikaambiwa nitaje kama kuna mali tulizochuma wote nikazitaja, kubwa ilikuwa ni nyumba ila yeye akajitetea kuwa nyumba niliikuta wakati naolewa na sikufanya marekebisho yoyote ambavyo si kweli.

Nikaelezea kwamba tulipo oana nyumba ilikuwa imepandishwa tu na kupigwa bati vilivyobaki tulimalizia kama wana ndoa na ushahidi upo. Tarehe 15 Decemba tunaleta mashahidi wa nyumba ambao nimeshawapata na vielelezo vipo vya kutosha. Pia tulipo oana tulikuwa tumepanga kwani nyumba ilikuwa bado kabisa kuisha na tulimalizia kwa makubaliano.

Sasa ivi na kwa yule mwanamke amefukuzwa yupo tu mtaani kwani nyumba alishapangisha bila hata idhini yangu. Yule mwanamke alimpigia baba mkwe (alitafuta namba hadi akaipata) na kumuelezea kwamba kwanza hampi matumizi toka aanze kuishi naye na pia alimdanganya kama hajaoa na mengine kibao ndio maana kaamua kumfukuza kwani anweza kuimfanyia kama alivyonifanyia mimi.

Nashukuru sana kwa kuwa wakwe zangu wapo pamoja na mimi kwani wananipenda na kuniheshimu

Gari yangu iko polisi kwa usalama zaidi mpaka hapo uamuzi wa mahakama utakavyotoka

Shukrani nawasilisha

Nacherewa

Kwanza hongera kwa kuitikia wito wangu kufaka utupe mrejesho wa hatma ya ndoa yako! Lakini pia hongera sana kwa hatua uliyofikia ktk kutafuta amani ya moyo wako!
Nacherewa nina uhakika utafikia mwisho mwema wa hili suala lako!
 
Last edited by a moderator:
hongera mamy Mungu akupigania..... iala now days wanaume wachache sana aiseee
 
daaaaah pole sana kwa mtihani ila hongera kwa maamuzi magumu...hyo ndo dawa ya wachepukaji na ujuaji mwingi.. mwanaume kuchepuka its not right na wanawake we shouldnt settle for less.... watakuja kunyooka tu!!!
 
Kweli tumebaki wachache sana, kuna haja wanaume wachache tuliobaki tupewe ulinzi maalum!😉

hahahahahahhaa usijali mtasindikizwa mpk na magari ya washawasha... tracking device zitawahusu... !!!
 
Back
Top Bottom