Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Kwakweli hata mm naona hii ndoa iliisha since day one maana kitendo cha kumalizia nyumba kwa makubaliano kilikua kinaonyesha tayari kwamba mtafikia mwisho mtagawana ndo maana mlikua na makubaliano ya namna hiyo. Pole by the way lakini kama alivyo sema mjumbe mmoja hapo ni vizuri kusikiliza pande mbili isije kuwa mambo ya muwamba Ngoma.....
 
Pole mummy subira yavuta kher
Habari za mchana wapendwa

Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Jamii Forum na members mliotoa michango yenu. Nimeona si vizuri kukaa kimya bila kuleta mrejesho wa kinachoendelea kwenye kesi yangu ya ndoa. Kwa wale ambao hamkuweza kufatilia hii post yangu mnaweza kusoma hapa Maneno ya kejeli ya mume wangu na Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Baada ya kufungua kesi mahakamani yeye alikimbilia BAKWATA ila mahakama ikanishauri nikawasikilize watasemaje huku kesi ya msingi ikiwa inaendelea mahakamani. BAKWATA wakajitahidi kusuluhisha ikashindikana, upande wa familia yake ikasema wao hawako tayari hili suala lirudi nyumbani na upande wa kwangu vilevile na mimi sikuwa tayari kurudiana na huyu mwanaume kwani alikuwa tayari amehamia kwa hilo jimama lake na nyumba akapangisha.

Baada ya vikao vitatu BAKWATA huyu mwanaume akaomba nimrejeshee mahari yake nami nikafanya hivyo na nikapewa barua ya kupeleka mahakamani ikieleza kwamba usuluhishi umeshindikana na mwanaume kaomba arejeshewe mahari yake hivyo kwa sheria za kiislam hamna ndoa tena.

Barua ilisomwa mahakamani na hakimu akamuuliza je pingamizi la madai ya talaka akakaa kimya baade ikabidi akubali kwani ndoa ilikuwa kiini macho tu. Nikaambiwa nitaje kama kuna mali tulizochuma wote nikazitaja, kubwa ilikuwa ni nyumba ila yeye akajitetea kuwa nyumba niliikuta wakati naolewa na sikufanya marekebisho yoyote ambavyo si kweli.

Nikaelezea kwamba tulipo oana nyumba ilikuwa imepandishwa tu na kupigwa bati vilivyobaki tulimalizia kama wana ndoa na ushahidi upo. Tarehe 15 Decemba tunaleta mashahidi wa nyumba ambao nimeshawapata na vielelezo vipo vya kutosha. Pia tulipo oana tulikuwa tumepanga kwani nyumba ilikuwa bado kabisa kuisha na tulimalizia kwa makubaliano.

Sasa ivi na kwa yule mwanamke amefukuzwa yupo tu mtaani kwani nyumba alishapangisha bila hata idhini yangu. Yule mwanamke alimpigia baba mkwe (alitafuta namba hadi akaipata) na kumuelezea kwamba kwanza hampi matumizi toka aanze kuishi naye na pia alimdanganya kama hajaoa na mengine kibao ndio maana kaamua kumfukuza kwani anweza kuimfanyia kama alivyonifanyia mimi.

Nashukuru sana kwa kuwa wakwe zangu wapo pamoja na mimi kwani wananipenda na kuniheshimu

Gari yangu iko polisi kwa usalama zaidi mpaka hapo uamuzi wa mahakama utakavyotoka

Shukrani nawasilisha

Nacherewa
 
Mapenzi hayana fomula!, mimi nadhani kama ungempenda sana, tena sana!, msingefika huko!,maana naamini mali sio zao la penzi!, Pia watu waweza kukushauri hivi ama vile, lakini mwisho wa siku utaishia kuachana nae moja kwa moa au kurudiana!, nafikiri ambo kubwa sana kutoka kwako ni maamuzi ya busara utakayochua. maamuzi yako ndio mwisho wa kila kitu, hivyo basi ukiyaheshimu wewe kila mtu atakuelewa!
Kati ya dhambi kubwa za ndoa ni kuchepuka, aidha mwanaume au mwanamke. Mwanandoa anapoamuwa kuchepuka mwenza wake akijuwa hapatakuwa na amani. Hata hilo tendo la ndoa halitakuwa na utamu maana huwezi kumfuruhia tena msaliti. Raha na furaha kitoweka kwa kuchepuka ni vyema kila mtu aangalie mambo yake. Hii inakuwa muhimu maana "jasiri haachi asili" na "mchepukaji haachi kuchepuka"
 
Back
Top Bottom