Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Mmmh dada kapumzishe nafsi yako kwani umezaliwa nae?! Akwendreee na sperms zake chache, mfyuuuuu! Siku ukihitaji kuzaa utazaa kwa uwezo wa Mungu, utashangaa una ovarian sijui nini na unazaa. Huyo X mume wako haku deserve
 
Mapenzi hayana fomula!, mimi nadhani kama ungempenda sana, tena sana!, msingefika huko!,maana naamini mali sio zao la penzi!, Pia watu waweza kukushauri hivi ama vile, lakini mwisho wa siku utaishia kuachana nae moja kwa moa au kurudiana!, nafikiri ambo kubwa sana kutoka kwako ni maamuzi ya busara utakayochua. maamuzi yako ndio mwisho wa kila kitu, hivyo basi ukiyaheshimu wewe kila mtu atakuelewa!
 
mimi sijui huwa nikoje, if at all i have to loose the husband, aseeeee question ya nyumba, gari, sijui vitanda na vijiko navyo viende tu, nianze upya!

huyu ni mimi lakin!
 
mimi sijui huwa nikoje, if at all i have to loose the husband, aseeeee question ya nyumba, gari, sijui vitanda na vijiko navyo viende tu, nianze upya!

huyu ni mimi lakin!

Una msimamo...😉
 
Una msimamo...😉

kimsingi, ndoa ikishafika hapo, nakuwa nimeshapoteza mnoooooo, tena nakuwa nimepoteza priceless time, priceless esfor?o, priceless friend, priceless com mi tmen, priceless Everything, so hivyo vyenye bei wacha tu viende!
 
kimsingi, ndoa ikishafika hapo, nakuwa nimeshapoteza mnoooooo, tena nakuwa nimepoteza priceless time, priceless esfor?o, priceless friend, priceless com mi tmen, priceless Everything, so hivyo vyenye bei wacha tu viende!

What U're saying is true on the other side!
 
Michepuko sawa kuama nyumbani ni ujinga kabisa piga show yako ukimaliza rudi home
 
hapa nilipo ipo kesi inanguruma ya BAKWATA jamaa hatoi matumizi na wala hashiriki na mke tendo muhimu. Mke anasema hana nyumba ndogo ila mimi naona no.
 
Naogopa kuchangia kwa kuwa uzi unaonesha kesi ingali mahakamani! Je, siyo kuingilia uhuru wa mahakama kwa kuleta jambo hili hapa jukwaani? Wanasheria naomba mwongozo kabla sijachangia.
 
Ndo ukubwa huo, kua uyaone, ndo hayo sasa si magorofa ya kariakoo, Katika vitu vinavyohitaji umakini mkubwa kuvifanya nasi ndoa ni miongoni mwao, nakusihi uwe na subira ila usiache kudai haki yako.
 
mimi sijui huwa nikoje, if at all i have to loose the husband, aseeeee question ya nyumba, gari, sijui vitanda na vijiko navyo viende tu, nianze upya!

huyu ni mimi lakin!

I agree, mimi ningeondoka na nguo tu. Na wanangu pia kama tumebahatika kupata watoto. Niache watoto! Over my dead body.
 
Habari za mchana wapendwa

Kwanza napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Jamii Forum na members mliotoa michango yenu. Nimeona si vizuri kukaa kimya bila kuleta mrejesho wa kinachoendelea kwenye kesi yangu ya ndoa. Kwa wale ambao hamkuweza kufatilia hii post yangu mnaweza kusoma hapa Maneno ya kejeli ya mume wangu na Mrejesho: Maneno ya kejeli ya mume wangu

Baada ya kufungua kesi mahakamani yeye alikimbilia BAKWATA ila mahakama ikanishauri nikawasikilize watasemaje huku kesi ya msingi ikiwa inaendelea mahakamani. BAKWATA wakajitahidi kusuluhisha ikashindikana, upande wa familia yake ikasema wao hawako tayari hili suala lirudi nyumbani na upande wa kwangu vilevile na mimi sikuwa tayari kurudiana na huyu mwanaume kwani alikuwa tayari amehamia kwa hilo jimama lake na nyumba akapangisha.

Baada ya vikao vitatu BAKWATA huyu mwanaume akaomba nimrejeshee mahari yake nami nikafanya hivyo na nikapewa barua ya kupeleka mahakamani ikieleza kwamba usuluhishi umeshindikana na mwanaume kaomba arejeshewe mahari yake hivyo kwa sheria za kiislam hamna ndoa tena.

Barua ilisomwa mahakamani na hakimu akamuuliza je pingamizi la madai ya talaka akakaa kimya baade ikabidi akubali kwani ndoa ilikuwa kiini macho tu. Nikaambiwa nitaje kama kuna mali tulizochuma wote nikazitaja, kubwa ilikuwa ni nyumba ila yeye akajitetea kuwa nyumba niliikuta wakati naolewa na sikufanya marekebisho yoyote ambavyo si kweli.

Nikaelezea kwamba tulipo oana nyumba ilikuwa imepandishwa tu na kupigwa bati vilivyobaki tulimalizia kama wana ndoa na ushahidi upo. Tarehe 15 Decemba tunaleta mashahidi wa nyumba ambao nimeshawapata na vielelezo vipo vya kutosha. Pia tulipo oana tulikuwa tumepanga kwani nyumba ilikuwa bado kabisa kuisha na tulimalizia kwa makubaliano.

Sasa ivi na kwa yule mwanamke amefukuzwa yupo tu mtaani kwani nyumba alishapangisha bila hata idhini yangu. Yule mwanamke alimpigia baba mkwe (alitafuta namba hadi akaipata) na kumuelezea kwamba kwanza hampi matumizi toka aanze kuishi naye na pia alimdanganya kama hajaoa na mengine kibao ndio maana kaamua kumfukuza kwani anweza kuimfanyia kama alivyonifanyia mimi.

Nashukuru sana kwa kuwa wakwe zangu wapo pamoja na mimi kwani wananipenda na kuniheshimu

Gari yangu iko polisi kwa usalama zaidi mpaka hapo uamuzi wa mahakama utakavyotoka

Shukrani nawasilisha

Nacherewa

Mimi nimekuwa interested sana na hii story yako Aunt lakini haisaidii lolote mana ulichokileta hapa ni maneno uliyotoa wewe mdomoni tu., hatujapata nafasi ya kusikiliza na upande wapili wewe umechukua nafasi ya kujielezea wewe na aliyekuwa mumeo pia umemtolea wewe maelezo, ni vyema mume naye aje hapa aeleze ya kwake kuhusu wewe hapa then tujue nani ni mnafiki otherwise wanawake tunawajuwa munatabia ya kubadilisha maneno sana.
 
Jaribu Kukaa chini upya we na mwenzi muyamalize,hiyo nyumba isikutoe roho dada yangu maana unaonesha dhahiri akili yako ni hicho kijumba,Sio leo mmeachana we umepata wako mpya na yeye ana mtu wake halafu mnaanza kutafutana tena mnarudiana kwa siri.Hiyo ni mihemko tu utakapo kosa mgao wa nyumba ndio utakoma.
 
Back
Top Bottom