Mrejesho: Biashara ya Ufundi Simu

Bossprota

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
253
243
Habari Wadau!

Mimi ni kijana mtafutaji wa hali ya chini kwanza niseme jamii forums n8 sehemu iliyonifanya nipate wazo hili ambalo naweza sema lime badilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa!

Mnano mwaka jana mwezi wa 9 nilifanikiwa kupata uzi hapa jf wenye ushauri juu ya biashara ya ufundi simu na nikajipanga na kuanza kuchukua hatua mwanzo nilikua nimeajiliwa kwenye kampuni fulani kwa mshahara wa Tsh laki 2 kwa mwezi nikajichanga huku najifunza basics za ufundi simu kama kuunga mic na spika kubadili systerm charge kuflash simu nk nikapata sehemu yakufanyia mazoezi golini kwamtu huku namlipa 30 kwa mwezi nikajifunza ufundi simu kila nikitoka kazini kwangu naenda kujifunza ilipofika mwezi wa kwanza nikajitosa lasmi kwenye ufundi simu.

Mrejesho
Nilianza kazi kwa mtaji wa Tsh 350,000/=
gun 6000/=
sodawire 20,000/= bunda
screw driver 8,000/=
chumba miezi 5 30@mwezi= 150,000/=
umeme 10,000/=
55,000/= hot air blower
Enga zakuwekea baadhi ya bidhaa
8 @1500=12,000/=
protectors 10@1200=12000/= flash(faster)3 @9,000/= gb32 =27,000/=
20,000/= line yalipa namba vodacom 30,000/= mabetri ya simu makava usb kardreader etc..

Hapo ndipo nilipouanza mwendo
Kwa mwezi wa kwanza sikuwa na makadrio maalumu maana nilianza biashara tar 17 hivyo sio mwezi lasmi saana japo siku ikiwa mbaya nalaza 10,000/= hasara zikawa zinakuja mixer kuharibu simu zawatu najikuta naenda kughalamia kwa fundi mwingine lakini hiki kipindi kilikuwa kigumu saana maana mteja analeta simu yenye tatizo la kubadilishiwa screen tatizo linaisha ahf mic inaharibika yaaan hadi sasa bado kwenye uharibifu ndio changamoto nayo pitia saaana lakini hadi nafika tar 31 january ninatsh 90,000/= mfukon nimesave ulipo anza mwezi wapili naeza sema ndipo nilipo anza rasmi biashara yangu maaana kunasiku naeza laza hadi 50,000/= nasiku mbaya naeza laza 15,000/=

Nikapambana hadi mwezi wa pili unaisha nimeingiza laki 6 kasoro yaani nilihisi ni uchawi aiseeeh hapo ndipo nikanunua blower kubwa ya 270,000/= ahf laki3 na50 ikabaki kama backup nanikama mtaji nilioanzia kiasi kwamba ningetaka kufungua goli lingine ningeweza hapo nilihisi sio mimi kabisa yaaan mwezi wa tatu kwenda wa4 nikajikuta nimelaza laki 7 na60 hapo nikiiangalia mpesa yangu najiona bakhresa flani hivi ndipo nikanunua desktop computer nakuinstall miracle thunder nakuongeza huduma zakuflash simu nakutoa pesa kwa lipa namba nnachofanya: mteja akija kutoa kuanzia 40,000/= anaacha tsh 2,000/= kama service charge kwa sasa kwasiku naeza pata hadi wateja 7 = >14,000/= day

Sasa huu mwezi wanne naeza sema nimefanikiwa kumiliki million kwenye account yangu mwenyewe kwa mara ya kwanza sasa ni mwezi wa tatu wa kazi yangu ya ufundi simu kwa haya mawndeleo najuta kwa nini nilichelewa kuisoma ile thread ya jamii forums
Malengo yangu: Kwa sasa hapa ninatengeneza simu nauza accesoriez nakutoa pesa kwa lipa namba

Kuanzia mwezi watisa nahitaji kuwekeza pia kwenye ufundi Tv,Deki,Sabufa,pasi,blenda nk.

Lengo ni kufungua branchi nyingine kwaajili ya shughuli hizo naombeni ushauri kwa mwenye uzoefu na hayo masuala ya ufundi Tv nk.

Nashukuru saana kwa wote mlioufanikisha uzi wakwanza wa ufundi simu..πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½πŸ™πŸ½
 

Bossprota

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
253
243
Je, ni kweli kwamba ili biashara isimame ni lazima uende kwa mganga(mtaalamu)?! Sema ukweli tu maana mostly hatujuani humu
Mh biashara yangu bado mpya kaka halafu me malengo ya biashara yangu nilitamani atleast niwe nalaza walau 10,000/= kwa siku ambapo nahisi most of time huwa ninapita hivyo nipo juu ya malengo yangu na mimi sio mzoefu wa biashara hivyo sijui chochote kuhusu hizo mambo za waganga ila nilichojifunza kwenye hii biashara waganga ni 1) mungu 2)ujuzi 3) afya 4) uwepo wako ofisini muda wote
5) uaminifu yaani kuwa mkweli kwa mteja na kuwa na mbinu za kumpumbaza mteja mfano mteja kaleta simu unajua kupona nileoleo basi mwambie aje achukue kesho na aache mawasiliano kabla haijafika kesho mpigie simu mwambie simu yako tayari hapo nafikiri ukiwa na hizo hapo juu basi ni waganga tosha aiseehπŸ€‘πŸ€‘πŸ€‘
 

G.25

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
1,637
1,701
Umeongelea miracle thunder, naomba nielezee kdg kuhusu hii kitu.
 

Bossprota

JF-Expert Member
Jul 16, 2015
253
243
Umeongelea miracle thunder, naomba nielezee kdg kuhusu hii kitu.
Hii ni software kwaajili ya kuflashia na kuread information za simu mbalimbali pia kupitia hii miracle thunder unaeza pia kufungua simu ambayo umesahau password unaeza kuijua password au pattern kama simu hujui pattern unaeza isoma halafu unafungua bila kufrash hivyo tuu
 
45 Reactions
Reply
Top Bottom