Mrejesho ajali ya coaster Tanga

Mrejesho ajali ya coaster Tanga

View attachment 506991 Tarehe 7/ May nilikuwa miongoni mwa abiria,nikiwa na mtoto wangu 3yrs old tukitoka kumsalimia Babu yake Tanga mjini.
Ajali ilipotokea ni umbali wa dakika 3 mpaka kituo tulichokuwa tushuke. Dereva akiwa speed kwenye kujaribu kuovertake,akaona mbele gari inakuja kasi na pembeni kuna koronga na Scania lilipark,tukasikia break kali na mayowe yakatamaaki.

Dalili ya ajali ilijia,nikamkumbatia mwanangu mapajani huku kalala,dereva akachomeka upande kwenye roli,mshindo mkubwa,mtoto akaanguka chini,nikarushwa mbele kidogo. Mtoto akaanza kulia,nimebanwa na siti kwenye mguu,ikavuta na watu,mtoto akaokotwa,hali ya kuchanganyikiwa ikanijaa,nikajikaza nabubuj8ka damu kichwa kizima,nikatoka na dirishani nikipiga yowe namtaka mwanangu!

Nilijibiwa kashapelekwa hospital,watu wakizidi kujaa kushangaa bila ya wengi kutoa msaada,vijana wakijazana kwenye basi huku nikiugulia chini baada ya nguvu za kysimama kuniisha huku nikipaza sauti "naomba mnipeleke hospital"

Dada mmoja akaja akanifunga na kanga yake kichwani kwani damu zilizidi,akaenda ndani ya bus,hatimae msamaria mwema mmoja akanibeba na mwenzie kwenye pikipiki na kuniwahisha hospital. Nikampa simu yangu awap8gie wazazi na ndugu,simu nyingine ziliibwa,hata saa ya mkononi dikumbuki nilivuliwa saa nggapi japo sikuzimia,Mungu mkubwa!

Nikamkuta mwanangu akishonwa huku akimlilia baba,nikalazwa pembeni yake,akaniona,akapunguza kulia,akapelekwa ward ya watoto.

Nikashonwa kichwani kwa zaidi ya masaa mawili na kibatari pia umeme ulipikatika,bila ganzi,wakahamia na mkononi ila baadhi nikagoma waniache,maumivu ya nyama za mkono yalizidi,hiyo ni hospital ya teule.

Kesho hadi saa 8 mchana sijafanyiwa dressing ya vidonda,kisa umeme hamna na vyombo havijachemshwa,tukapambana nikahamia hospital ya mkoa baada ya wazazi na ndugu kuja juu.

Nashukuru Mungu,naimarika,nafarijika.

Well,wanasema watoto ni malaika,I reserve my comment ila wakati tunapanda mtoto alichagua siti ya mwisho kabisa,nikamwambia njoo huku,akasema hapa,huku,hapa,hatimae akanitii akaja,akakaa dirishani. Nilimchagulia siti karibu na mbinuko wa tyre ili aweze kukanyaga vizuri pia watu wawili,he is 3yrs old.

Siti aliyochagua hakuna aliyekufa,siti yetu tumejeruhiwa,wa mbele yetu wanne walifariki palepale. Mungu awarehemu.

Naendelea kyjiuguza,Ahsanteni,mbarikiwe!
pole sana, kwa ajali ,na maumivu ,Mungu akupe ahuaeni urejee katika hali yako
 
Daaaah! Nimeshindwa kumalizia kusoma. Pole Sana ndugu na Mungu aendeleee kuwaimarisha afya zenu.
 
Pole sana mkuu Mungu azid kuwaponya.. Ila hii ajili ni uzembe wa dereva 100% kama yuko hai anatakiwa afungwe maisha! Sijui wanawahigi nini washenz hawa.. Pumbaf zake!
 
pole sana
hakika wote kwenye hiyo siti mlitembelea nyota ya mtoto
israel alivoona mtoto akaahilisha kuchukua roho zenu
ndio maana napenda sana kubeba watoto wa watu kwenye basi nikisafiri maana najua kwa imani ikitokea ajari ntapona tu
 
Daah polesana mkuu MUNGU awaponye haraka wote mlio patwa na hiyo ajali.

R.I.P marehemu wote.
 
Back
Top Bottom