Mrejesho ajali ya coaster Tanga

Mrejesho ajali ya coaster Tanga

Pole sana mkuu na mtoto wetu, mungu awape uponyaji na awalaze mahali pema peponi waliofariki katika ajali hiyo.

Katika ajali hii dreva wa coaster ni mzembe sana, kwa nini akimbize gari lenye abiria na ku overtake Lori bovu sehemu ya mlimani ambayo haoni mbele vizuri? ?

Serikali, msikae kimya ajali za barabarani hv sasa ni janga zito na kubwa hivi kweli imeshindikana kabisa kuzizidhibiti? ?
Mfano haya malori kuharibika barabarani ambapo ni nyembamba, hv serikali mmeshindwa kabisa kujenga diversions mfano wa vituo vya mabasi ila viwe virefu kila baada ya kilomita 10, kwa ajili ya kuegesha malori mabovu, yaliyopata hitilafu, madereva kupumzika nk hii ingekupunguza kwa kiasi kikubwa ajali hizi.
Pia traffic police rudisheni road patrol, kuna madreva wazembe wengi ambao mngeweza kuwabaini mara moja kuliko kukaa sehemu moja na kupima speed tu, viongozi wetu acheni kukariri mambo hayo hayo kila siku, jaribuni kuwa wabunifu, watu wengi wanapoteza maisha huko barabarani ni lazima sasa kitu kikubwa kifanyike.
Sijui hata kama ushauri wangu huu utamfikia yoyote na kuleta badiliko Kwny janga hili.
 
Pole sana! Mwenye Enzi Mungu aendelee kuwabariki! RIP kwa hao watu wa4 jamani!
 
View attachment 506991 Tarehe 7/ May nilikuwa miongoni mwa abiria,nikiwa na mtoto wangu 3yrs old tukitoka kumsalimia Babu yake Tanga mjini.
Ajali ilipotokea ni umbali wa dakika 3 mpaka kituo tulichokuwa tushuke. Dereva akiwa speed kwenye kujaribu kuovertake,akaona mbele gari inakuja kasi na pembeni kuna koronga na Scania lilipark,tukasikia break kali na mayowe yakatamaaki.

Dalili ya ajali ilijia,nikamkumbatia mwanangu mapajani huku kalala,dereva akachomeka upande kwenye roli,mshindo mkubwa,mtoto akaanguka chini,nikarushwa mbele kidogo. Mtoto akaanza kulia,nimebanwa na siti kwenye mguu,ikavuta na watu,mtoto akaokotwa,hali ya kuchanganyikiwa ikanijaa,nikajikaza nabubuj8ka damu kichwa kizima,nikatoka na dirishani nikipiga yowe namtaka mwanangu!

Nilijibiwa kashapelekwa hospital,watu wakizidi kujaa kushangaa bila ya wengi kutoa msaada,vijana wakijazana kwenye basi huku nikiugulia chini baada ya nguvu za kysimama kuniisha huku nikipaza sauti "naomba mnipeleke hospital"

Dada mmoja akaja akanifunga na kanga yake kichwani kwani damu zilizidi,akaenda ndani ya bus,hatimae msamaria mwema mmoja akanibeba na mwenzie kwenye pikipiki na kuniwahisha hospital. Nikampa simu yangu awap8gie wazazi na ndugu,simu nyingine ziliibwa,hata saa ya mkononi dikumbuki nilivuliwa saa nggapi japo sikuzimia,Mungu mkubwa!

Nikamkuta mwanangu akishonwa huku akimlilia baba,nikalazwa pembeni yake,akaniona,akapunguza kulia,akapelekwa ward ya watoto.

Nikashonwa kichwani kwa zaidi ya masaa mawili na kibatari pia umeme ulipikatika,bila ganzi,wakahamia na mkononi ila baadhi nikagoma waniache,maumivu ya nyama za mkono yalizidi,hiyo ni hospital ya teule.

Kesho hadi saa 8 mchana sijafanyiwa dressing ya vidonda,kisa umeme hamna na vyombo havijachemshwa,tukapambana nikahamia hospital ya mkoa baada ya wazazi na ndugu kuja juu.

Nashukuru Mungu,naimarika,nafarijika.

Well,wanasema watoto ni malaika,I reserve my comment ila wakati tunapanda mtoto alichagua siti ya mwisho kabisa,nikamwambia njoo huku,akasema hapa,huku,hapa,hatimae akanitii akaja,akakaa dirishani. Nilimchagulia siti karibu na mbinuko wa tyre ili aweze kukanyaga vizuri pia watu wawili,he is 3yrs old.

Siti aliyochagua hakuna aliyekufa,siti yetu tumejeruhiwa,wa mbele yetu wanne walifariki palepale. Mungu awarehemu.

Naendelea kyjiuguza,Ahsanteni,mbarikiwe!
Pole sana
 
Wanajamii. ... sikusudiii kuanzisha hoja ya kisiasa tafadhali nieleweni. Ila inafaa sana kujua. Mapesa yote yanayo kusanywa kweli tunashindwa kua na fungu ambalo linaweza kuwa tayari kukabiliana na mambo kama haya. Mtu anafika hospital anashonwa bila sindano ya ganzi? Hata gari la wagonjwa hakuna? Tanzania ndio inayoongoza kwa kukusanya kodi za bara bara Africa kwa nini kusiwe na fungu la kukabiliana na mambo kama haya?
 
Dah, hii thread imenisikitisha sana, pole sana mkuu, Msijali mtapona tu.
Na vipi kuhusu dripu? Walikuwekea? Manake umepoteza damu na maji mengi
 
Ooh jamani poleni sana, Mola awaondolee maumivu na mpone haraka.

Hiyo habari ni ya kusikitisha sana juu ya hospitali zetu nchini hapa.
Waeleze wanaokutuma kutukana wenzio basi wafanye na yanayowahusu siyo pole wakati wewe ni kati ya tatizo.
 
Back
Top Bottom