18 wajeruhiwa ajali ya Coaster Same

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,833
21,466
Watu 18 wamejeruhiwa wilayani Same mkoani Kilimanjaro baada ya basi aina ya Coaster walilokuwa wamepanda kutoka Dar es salaam kuja Kilimanjaro kutumbukia kwenye korongo katika eneo la Mabilioni mpakani mwa wilaya za Korogwe na Same huku dereva wa gari hilo akidaiwa kuwa alisinzia.

Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema imetokea jana Julai 14, 2023 saa 10 alfajiri ambapo dereva pamoja na abiria waliokuwepo kwenye gari hilo walikuwa wamesinzia.

Kasilda amesema baadhi ya majeruhi hao wamevunjika mikono, wamejeruhiwa kichwani na sehemu za mbavu ma kati ya majeruhi hao, 10 wamekimbizwa katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC) baada ya hali zao kuwa mbaya huku wengine walipatiwa huduma katika kituo cha afya cha Hedaru na hospitali ya wilaya ya Same.
“Ni kweli kumetokea ajali alfajiri ya leo kati ya majira ya saa 9 au 10 usiku katika eneo la Mabilioni karibu na mpaka wa Korogwe na Same, inavyoonekana ni kama dereva alisinzia,” amesema.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, abiria wote walikuwa wamelala na hadi ajali inatokea, walikuwa hawajui kilichotokea mpaka hapo walipookolewa kwenye korongo hilo ambalo ni mkondo wa maji.

“Idadi ya abiria waliokuwa kwenye Coaster ni 25 lakini waliojeruhiwa ni 18, wawili ambao hawakujeruhiwa sana walikimbizwa kituo cha afya cha Hedaru wanaendelea na matibabu pale, lakini 16 walipelekwa hospitali ya wilaya ya Same kwa sababu walikuwa wamejeruhiwa sana na kati ya hawa, 10 walikimbizwa hospitali ya KCMC kwa ajili ya matibabu zaidi.

“Majeruhi wengi walipata majeraha kichwani, kwenye mbavu, wengine wamevunjika mikono, bahati mbaya walikaa muda mrefu pale kwa sababu ni eneo ambalo halina nyumba za kuishi ni mashamba tuu,” amesema.

Hata hivyo, Kasilda amesema baada ya kutokea ajali hiyo dereva wa gari hilo alitoroka kusikojulikana.

MCL
 
LATRA wasipoamka na kuondoa vicoaster route ndefu na za usiku kuna siku zitamaliza watu
 
Hii tena ni ya jana barabara hiyo hiyo
716638B8-75D0-4456-A416-DFFD9E649763.jpeg
 
LATRA wasipoamka na kuondoa vicoaster route ndefu na za usiku kuna siku zitamaliza watu
Wala wasiviondoe Sema wakomae na madereva tu

Ajali ni ajali tu, kwani new force zinazochinja watu mchana napo waondoe mabasi ya mchana?

Coaster nyingi tu zinatoka salama na zinarudi Salama kila usiku upitao
 
SPECIAL HIRE hizo, nakumbuka kuna siku tunatoka Moshi dereva alikua analala kabisa anajisahau, tukafika pale kwenye round about ya bagamoyo baada ya kukunja aje town jamaa anataka afakamie kile kibao cha Maryan University, kushikwa bega akashtuka ghafla, halafu anajitetea , nyie waoga sana, nina uzoefu na hii kazi.
 
Vinaendeshwa na vinyoka ukumbuke!!!
Na vyenyewe kabla ya kuondoka Dar vinapiga kwanza K vant
 
SPECIAL HIRE hizo, nakumbuka kuna siku tunatoka Moshi dereva alikua analala kabisa anajisahau, tukafika pale kwenye round about ya bagamoyo baada ya kukunja aje town jamaa anataka afakamie kile kibao cha Maryan University, kushikwa bega akashtuka ghafla, halafu anajitetea , nyie waoga sana, nina uzoefu na hii kazi.
Hahahaaa.... Alijaribu kuleta masihara na kifo!
 
Usafiri wa abiria kwa kutumia Coaster Dar - Kilimanjaro muda wa USIKU kuna siku mtaniambia.
Mkuu Ukipata dharura Ndiyo utaona umuhimu wa hizo coaster za usiku.

Kuna siku nilikuwa Kahama, nikapata dharura iliyonilazimu kuwepo Morogoro kesho asubuhi na mabasi yote yameondoka. Nikaja kubahatisha Coaster, nilitoka Kahama saa tisa alasiri nikafika Morogoro saa kumi na mbili alfajiri, nianywa kahawa nikaenda ofisini 😅
 
Kahama ni kahama mkuu.
Hakuna madereva walevi huko.
Hii Dar -Kilimanjaro , dereva wa coaster ana miaka 23 anapata Kvant ndio anaanza safari usiku.
 
SPECIAL HIRE hizo, nakumbuka kuna siku tunatoka Moshi dereva alikua analala kabisa anajisahau, tukafika pale kwenye round about ya bagamoyo baada ya kukunja aje town jamaa anataka afakamie kile kibao cha Maryan University, kushikwa bega akashtuka ghafla, halafu anajitetea , nyie waoga sana, nina uzoefu na hii kazi.

Aisee,mpuuzi kweli
 
Mkuu Ukipata dharura Ndiyo utaona umuhimu wa hizo coaster za usiku.

Kuna siku nilikuwa Kahama, nikapata dharura iliyonilazimu kuwepo Morogoro kesho asubuhi na mabasi yote yameondoka. Nikaja kubahatisha Coaster, nilitoka Kahama saa tisa alasiri nikafika Morogoro saa kumi na mbili alfajiri, nianywa kahawa nikaenda ofisini
Ni kweli kunakuwa na dharura sana ambayo inalazimu mtu uchomoke.dunia ya sasa huwez kuwa unasafir mchana tu.ajali imetokea polen sana. Kuna hizi za magazet.jamaa wanakamua fresh tu na halali.tumetoka dom asbuhi tupo dar
 
  • Thanks
Reactions: apk
PITIA HAPA NA HAKIKISHA UNAPIGA KURA,HIZI AJALI ZIMESHATUCHOSHA SANA WATANZANIA NI WAKATI WA KUAMKA NA KUITAKA SERIKALI IHAKIKISHE INAFANYA YAFUATAYO👇👇
 
Back
Top Bottom