Mramba anasafishwa?


Ukipanda bangi utavuna njugu teh teh teh hiiiii hiiii haaaa
 
Hao waheshimiwa hawakai kwenye majimbo yao, wanashinda Dar. Si ajabu hata Mramba mwenyewe hajui kuna mradi kama huo. Mramba kama msomi alitakiwa awe chachu ya kusimia hiyo miradi na kusaidia kuongeza capacity kwenye hizo halmashauri. Badala yake yeye anashinda Dar.

Hilo ndilo tatizo kubwa hata kwa wilaya zingine. Wanawaachia hizo shughuli watu ambao hawana uwezo kabisa.
 
Source:Mwananchi
 
Hapa kuna unafiki kwa walio wengi ili wasionekane wabaya! Hapo ndo tutakapokwamia! Kama mtu ana kesi ya wizi unampa pole ya nini? Kama hatuwezi kumwua nyani bila kumwangalia usoni nadhani safari yetu bado ni ndefu sana.
 
Hapa kuna unafiki kwa walio wengi ili wasionekane wabaya! Hapo ndo tutakapokwamia! Kama mtu ana kesi ya wizi unampa pole ya nini? Kama hatuwezi kumwua nyani bila kumwangalia usoni nadhani safari yetu bado ni ndefu sana.

SIKUJUA KAMA KUNA WATANZANIA WAKATILI KIASI HIKI.

Kama Mramba angekuwa ni Baba yako, Mjomba wako au Rafiki yako ungefanyaje?

Hapo nimeongea kwa ubinadamu tu wachilia mbali sheria inasemaje juu ya mtuhumiwa ni wakati gani anatakiwa aonekane ana hatia.
 

Mkuu mwizi ni mwizi,
Akiwa mjomba ako jambazi au mwizi utaendelea kumkumbatia?Labda kama uwa mnashare vitu anavyo piga sehem sehem.Huyu inafaa atengwe kabisa katika jamii kajinufaisha mwenyewe.
 

Ungekuwa hakimu anayesikiliza kesi yake ungemwachia? Ungekuwa mkuu wa gereza alikopelekwa rupango ungemweka wapi?

Kwani vibaka tunaowachoma moto kwa uiba mkufu wa 15000 hawana mama na baba au watoto? Au wezi ni watu masikini wasio na vyeo, ambao si binamu na hawastahili huruma? Kwa hiyo una maana akina Mramba wako juu katika hadhi za kibinadamu kwa hiyo wanatakiwa kuonewa huruma hata wakiiba au kuua? Kwa mtaji huo Mkapa atafikishwa kwenye mkono wa sheria kweli?
 

Huu ubinadamu wa aina hii ndio unatulemaza sisi Watanzania.

Hao wabunge wangemwachia mkewe hiyo kazi ya kumfariji.
 
Hapa kuna unafiki kwa walio wengi ili wasionekane wabaya! Hapo ndo tutakapokwamia! Kama mtu ana kesi ya wizi unampa pole ya nini? Kama hatuwezi kumwua nyani bila kumwangalia usoni nadhani safari yetu bado ni ndefu sana.

Huyu bado ni mtuhumiwa, hivyo hatakiwi kutengwa, ana kesi ya wizi (kutumia vibaya ofisi), lakini bado haijathibitishwa ni mwizi mpaka kesi itakapotolewa maamuzi.
 
Hapa kuna unafiki kwa walio wengi ili wasionekane wabaya! Hapo ndo tutakapokwamia! Kama mtu ana kesi ya wizi unampa pole ya nini? Kama hatuwezi kumwua nyani bila kumwangalia usoni nadhani safari yetu bado ni ndefu sana.

Mkuu nadhani tutakuwa tunakwenda mbali sana iwapo tutaanza kumuona Mramba kama ana hatia. Kilichopo mbele yetu ni ksi tu ambayo hakuna mwenye uhakika na matokeo yake. mwisho wa siku Mramba anaweza kuonkana kuwa hana hatia.
Lakini pia katika utamaduni wa kiafrika, kupeana pole, hata kwa adui yako, ni jambo la kistaarabu
 
Huyu bado ni mtuhumiwa, hivyo hatakiwi kutengwa, ana kesi ya wizi (kutumia vibaya ofisi), lakini bado haijathibitishwa ni mwizi mpaka kesi itakapotolewa maamuzi.

Mbona hata mimi sijasema atengwe na wala sijapinga yeye kuruhusiwa kuingia bungeni? Natambua kuwa ni mtuhumiwa kwa hiyo bado hana hatia mpaka mahakama ikisema. Ila kama tunamwonea huruma kiasi hicho tunatuma ujumbe gani kwa hakimu? Nadhani tunamwambia kuwa ukimtia hatiani wewe ndiye mbaya wake au?

Wabunge wangemsalimia kama kawaida na si kujaribu kuleta hisia za public sympathy kwamba anaonewa! Kwa maoni yangu, hii ina mdhara makubwa sana kwa watu wanaohusika na kesi hii (na nyingine za namna hii) na ni jambo la hatari. DPP atajisikiaje asikia wabunge wengi wa CCM wana-sympathise na Mramba?
 
Mimi nataka nyie wote mnaopinga.

KAMA ANGEKUWA NI BABA YENU AU REFIKI YAKO WA KARIBU UNGEFANYAJE?

SEMA UKWELI.

Kama na mimi ni mwizi kama yeye nitaumia sana na pia nitajitahidi kumsaidia. Na kama anaonewa nitakufa na mtu! Ila kama mimi si mshabiki wa mambo yake nitakaa upande mwingine. Sidhani kama kuna sheria au mila inayomlazimisha mtu kuwa upande wa ndugu yake ambaye ni mhalifu au anatuhumiwa kwa uhalifu. Kwa hiyo wewe mwenzetu utakufa na baba yako hata kama kaiba mkufu na tayari anachomwa moto pale mtaa wa Kongo?
 


Pole kwa ku kamatwa????

Maybe it went something like this:

Mheshimiwa I'm sorry you were caught stealing, if you need tips on how to steal without being caught we can talk later. I am experienced at stealing money meant for hospitals, schools, roads, medicine, food etc. All the things that could have saved the lives of thousands of Tanzanians, developed our country, improved the lives of many people.

But come on now i had to get that new Land Rover even if it means Tanzanians will have to eat grass i must have that new Landrover. I know i can count on you my friends, family and those stupid grass eating Tanzanians that i am robbing to support me through thick and thin, as i continue to plunder the resources of this country for my own personal benefit.

By the way remember you are innocent until proven guilty. Unlike those thieves that are caught stealing a chicken at the market and immediately lynched by an angry mob. You are a special thief, you wear a suit and tie so you will undoubtedly get the support of a lot of ignorant Tanzanians even though you stole millions and could have indirectly contributed to the death, illness and ignorance of thousands of Tanzanians....


GET THE **** OUT OF HERE!!!! these people are nothing but common thieves of the variety you find at Kariakoo. Throw them in Jail and throw away the key (actually if i had it my way i would go the chinese way and execute them). When he decided to stael he knew exactly what he was doing and now he wants sympathy. How about sympathy for all those people that have been affected by his theiving...

Tanzanians wake up. There should be zero tolerance for mafisadi.
 

YAANI NAONA CONTRADICTION TUPU.

unataka kunieleza ndugu wa watuhumiwa wakienda kuwasindikiza ndugu zao huku wakitoa machozi inainfluence maamuzi ya mahakimu?

sidhani kumpa mtu sumpath kwa kumkumbatia unatoa ujumbe kuwa anaonewa.
 
Siamini kuwa Hakimu yeyote anafanya maamuzi kutokana na hisia za watu wa nje (na hata public). Mahakimu wanaongozwa na sheria za nchi katika kutimiza wajibu wao na hasa kutoa maamuzi.

Vile vile itambulike kuwa kila mtu anae tuhumiwa kwa kosa lolote, hawi mkosefu mpaka Mahakama ithibitishe hivyo. Mramba, Yona na Mgonja sio wakosefu (ni watuhumiwa tu). Kesi yao itakapokwisha, ndipo tutakapojua nani mkosefu (au kama yupo mkosefu yeyote).

Wakuu, Wabunge wanayo haki kama walivyonayo watu wengine wowote kumpa pole na hata kumtakia mema Mbunge mwenzao, hasa wakati huu ambapo kesi inaendelea na haja hukumiwa. Hakuna hata mmoja kati yetu mwenye mamlaka ya kupinga uamuzi wao wa binafsi kufanya hivyo. Haina madhara yoyote, na ni hulka ya kibinadamu (hasa binadamu mstaarabu).
 
YAANI NAONA CONTRADICTION TUPU.

unataka kunieleza ndugu wa watuhumiwa wakienda kuwasindikiza ndugu zao huku wakitoa machozi inainfluence maamuzi ya mahakimu?

sidhani kumpa mtu sumpath kwa kumkumbatia unatoa ujumbe kuwa anaonewa.

Kwa hiyo wabunge wote wa CCM walioenda kumpa pole Mramba (na kumkumbatia!) ni ndugu zake? Tueleze basi kama na wewe ni ndugu yake. Hebu basi soma post ya Alpha hapo juu halafu utupe majibu. Naona unataka kupotosha mjadala kwa kutetea vitu ambavyo viko wazi tu!
 
Mkuu mwizi ni mwizi,
Akiwa mjomba ako jambazi au mwizi utaendelea kumkumbatia?Labda kama uwa mnashare vitu anavyo piga sehem sehem.Huyu inafaa atengwe kabisa katika jamii kajinufaisha mwenyewe.

Fidel80,
Hajathibitishwa kuwa mwizi bado jamani.Au hatujali tena utawala wa sheria?
Tukumbuke kwa sasa ni mtuhumiwa tu.. mpaka itakapothibitika pasipo shaka yoyote kuwa alitenda kosa.Hapo ndio tumhukumu kwamba ni mwizi.Naelewa Umma wa Watanzania wenye uchungu na nchi yao hawatanielewa lakini kama tunataka kufuata utawala wa sheria inabidi tukubali misingi hii.
 
Ikifika hapo huwa nachoka kabisa
 

Alpha,
Thanks for making me laugh out so loud even though this in not a laughing matter.....
The way you made a U-Turn in ur presentation is what really made my day.
WoS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…