Jana na leo magazeti yamekuwa ya kitangaza kuanza mpango wa kuuza viwanja vya Tabata Kinyerezi!
Kwa sio amini bei tajwa watafute gazeti la Mtanzania au Mwananchi la jana au wafike office za manispaa ya Ilala, mabango kila mahali! Hakuna typing errors! That are the price! Na hii ni Kinyerezi Kifulu! Mpo hapo wana janvi?
nania alikuambia kuna maisha bora??? na nani alisema serikali itapanga bei hata kwa ardhi binafsi??? wameshindwa sukari wataweza ardhi?Jana na leo magazeti yamekuwa ya kitangaza kuanza mpango wa kuuza viwanja vya Tabata Kinyerezi!
Lakini cha kushgangaza ni hizo bei! Hakika mtanzania wa kawaida kiwanja kilicho pimwa atakisikia kwenye bomba maana bei ya kiwanja cha makazi ni shs 10,000 kwa sqm moja, makazi na biashara shs 15,000, Biashara shs 20,000, Ibada shs 8,000 na waliokuwa na nyumba kabla ya mradi ni shs 5,000!
Yako wapi maisha bora kwa kila Mtanzania? Niwazi viwanja hivi vitachukuliwa na Mafisadi wenye pesa ndefu.
Kibaya zaidi watu waliochukuliwa maeneo yao hawajalipwa! Lakini viwanja sasa vinauzwa!
Habari za uhakika kutoka Manispaa ya Ilala, nikwamba Selikari haina pesa za kulipa fidia hivyo Basi wanauza viwanja ili waweze kulipa fidia, kama si unyonyaji ni nini sasa!
Wapi wanasiasa akina Nape na wenzake walioko madarakani? Je haya mnayaona? Au mnakalia ufisadi wa Slaa? Hima hima wana Kinyerezi haki yenu inapotea, na hakuna wa kuwasaidia, serikali imefilisika!
Huwezi kusema gharama za viwanja zinafidia gharama za upima na miundo mbinu wakati miundo mbinu yenyewe hatuioni.
Nguvu ya Umma Iko wapi!
Mungu Ibariki Tanzani
ukisusa wenzako twala ati'Kaka mimi nimesoma gazeti la Mtanzania jana sikuamini. Nikapiga simu mahala nikaambiwa habari ndiyo hiyo. Yaani ukitaka kiwanja cha 25mx22m = 550m2 (high density) unatakiwa utoe Tshs. 5,500,000.00 tena within 2 weeks. Jamani nani anaweza kupata hizo pesa na kulipa. Mfanyakazi gani atapata kiwanja cha bei hizi? Serikali naona sasa inachezea maisha ya watu. Kama hali ni hiyo kwa nini watu wasijenge mabondeni na kwenye hifadhi za barabara?
Wanasema unatakiwa urudishe gharama za miundombinu wakati hakuna miundombinu ni vichaka vitupu kule kinyerezi - Kifuru. Jamani jamani serikali hii naona imetuchoka sasa.
Bei hiyo ni kubwa mno na lengo lao nadhani ni kuwauzia mafisadi wenzao. Ni raia gani wa kawaida au mfanyakazi mwaminifu anayeweza kununua kiwanja kwa 9000000 ndani ya siku saba???.