Mradi wa Ufugaji wa ng'ombe

Wadau ninampango wa kufuga ngombe wa maziwa wa kizungu, kwa ajili ya biashara ya maziwa ila sijui changamotom zake, mwenye elimu na hii biashara anipe mwongozo jamani.

Natarajia kuanza na ngombe mmoja mwenye mimba.
 
Ndugu wasomaji, natafuta ng'ombe wa maziwa mwenye uwezo wa kutoa lita kuanzia 21 na zaidi kwa siku, awe wa uzao wa pili na na ana mimba ya 8months au zaidi. sema na bei. sihitaji dalali. Samahani kama kuna mtu anafahamu wapi naweza pata, naomba anisadie.
 
Sema wewe sasa hivi uko wapi na huyo ng`ombe utamfugia wapi. Hii itakusaidia kupunguza gharama za kumsafirisha. Kwa mfano ng`ombe hao wapo ASAS Iringa na ww uko Musoma, kwa vyo vyote inakuwa hailipi.
 
Sema wewe sasa hivi uko wapi na huyo ng`ombe utamfugia wapi. Hii itakusaidia kupunguza gharama za kumsafirisha. Kwa mfano ng`ombe hao wapo ASAS Iringa na ww uko Musoma, kwa vyo vyote inakuwa hailipi.

Mkuu Malila kuna ng'ombe wanaoweza kutoa zaidi ya lita 20 kwa siku kwa mazingira ya joto kama Dar na Pwani?
 
Mkuu Malila kuna ng'ombe wanaoweza kutoa zaidi ya lita 20 kwa siku kwa mazingira ya joto kama Dar na Pwani?

Jibu la haraka ni kwamba, ni kazi sana kumpata ng`ombe wa hivyo ktk mazingira ya Dar na Pwani. Japo chini ya jua mambo mengi yanawezekana.
 
Nashukurru sana kwa majibu na ushauri wanajamvini, mimi nipo morogoro-ifakara.nategemea kufuga huko ifakara.
 
Wape ng’ombe wako lishe kamili, yenye nguvu, protini, na vitamin pamoja na maji ya kutosha.
Kulisha ng’ombe kwa kutumia aina yoyote ya malisho haitoshi kukuhakikishia ng’ombe anakuwa na afya nzuri na kutoa maziwa ya kutosha. Kama ilivyo kwa binadamu, ng’ombe anahitaji mlo kamili. Malisho ni lazima yawe na uwiano sahihi wa viungo.
Mifugo inahitaji chakula kitakachowapa nguvu, protini, madini, na vitamin ili kujenga miili yao, kuzalisha maziwa, na kuzaliana. Wanyama wadogo wanahitaji virutubisho vya kutosha, ili wakuwe na kuongeza uzito. Ng’ombe wa maziwa wanahitaji virutubisho zaidi ili kuweza kuzalisha maziwa kwa wingi hasa katika kipindi cha miezi 3-4 ya mwanzo baada ya kuzaa, wakati ambao uzalishaji wa maziwa unakuwa juu.
ENDELEA KUSOMA ZAIDI HAPA SEKTA YA MIFUGO TANZANIA
 
ni aina gani ya ng'ombe ni nzuri kwa ajili ya maziwa na wanauzwa wapi na wanatoa lita ngapi kwa siku kama wakilishwa na wakihudumiwa vizuri?
 
hivi bei ya ng'ombe mwanamke mwenye umri wa mwaka na nusu hadi mitatu ni sh ngapi jamani?
 
Wakuu nawasalimu sana. Napenda kabla ya yote niappreciate michango yenu hasa katika forum hii, imekuwa ikinisaidia sana. Sasa turudi kwenye uzi huo hapo juu:
Naomba mwenye ushauri juu ya jambo hilo anisaidie please, nipo dar natamani kuanza mradi huo januari mwakani. Mpango ni kuwa na ng'ombe bora kama 10 hivi (wenye uwezo wa kutoa minimum of 10 liters/ng,ombe per day), shamba kwa ajili ya kufugia na kuotesha malisho ya mifugo hiyo (about 6 acres). Naomba ushauri kuhusu yafuatayo:

Mbegu bora ya ng'ombe wa maziwa

Eneo lililopo nje kidogo ya mji ambalo naweza kulitumia( kwa kulinunua)

Ushauri wa namna bora ya kufanya mradi huo.

Please kwa anaejua possible costs za eneo na ng'ombe wazuri nitashukuru.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom