Serikali Yatakiwa Kutumia Ziwa Tanganyika Kusambaza Maji Mkoa wa Rukwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE BUPE MWAKANG'ATA AITAKA SERIKALI KUTUMIA ZIWA TANGANYIKA KUSAMBAZA MAJI MKOA WA RUKWA

"Je, lini Mradi wa Maji Kata za Kaengesa na Sumbawanga Vijijini utakamilika?" - Mhe. Bupe Nelson Mwakang'ata, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa

"Kata ya Kaengesa ina Vijiji 4 ambapo katika mwaka wa fedha 2022-2023 Serikali imeendelea kutekeleza mradi wa Maji Mkunda group unaohudumia Vijiji vya Mkunda, Kaengesa A&B. Mradi unategemea kukamilika Septemba 2023. Wananchi wa Kijiji cha Mkunda wameanza kupata Maji. Kijiji cha Itera Serikali itafanya usanifu na kujenga mradi wa Maji katika mwaka wa fedha 2023-2024. Kata ya Kanda yenye Vijiji 4 katika mwaka wa fedha 2022-2023 Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa Maji utakaohudumia Vijiji vya Rula na Chitete. Vijiji vya Lapola A&B usanifu unafanyika katika mwaka wa fedha 2023-2024 na miradi hiyo itajengwa" - Mhe. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri Maji

"Ni lini Serikali itapeleka fedha kwenye mradi uliochukua muda mrefu, Nkana - Isare ulioko Nkasi Kusini? Ni lini Serikali itakamilisha mradi wa kutoa Maji katika Ziwa Tanganyika na kusambaza Mkoa wa Rukwa? - Mhe. Bupe Nelson Mwakang'ata, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa

"Malipo ya mradi uliochukua muda mrefu ni vipaumbele vya Wizara kuhakikisha miradi yote inakamilika, lengo la kupata Maji bombani linatimia Kusambaza Maji Ziwa Tanganyika ni moja ya vipaumbele vya Wizara. Tutahakikisha maeneo yote ya Nkasi Kusini & Kaskazini tuweze kuyafikia na miradi iweze kukamilika" - Mhe. Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-06-14 at 15.55.08.jpeg
    WhatsApp Image 2023-06-14 at 15.55.08.jpeg
    155.6 KB · Views: 5
Back
Top Bottom