Mradi wa maji chalinze umekamilika asilimia 98

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
CHALINZE

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amekagua na kuridhika kuruhusu maji yaanze kutumiwa na wananchi katika maeneo ya Chalinze ambapo miundombinu imekamilika.

Hizi ni habari njema kwa wananchi wa Chalinze ambao kwa muda mrefu wanahangaika na shida ya maji.

Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Chalinze amemshukuru Hayati Rais John Magufuli kwa kuridhia kuanzisha mradi na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anaukamilisha mradi huu.

Mbunge alieleza kutambua mchango wa wote kwa kusema kuwa "...kiungwana Usipomshukuru Binadamu mwenzio kwa kidogo , hauwezi mshukuru Mwenyezi Mungu kwa kikubwa.

Mhe Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani.

FB_IMG_1636228982345.jpg

FB_IMG_1636228968142.jpg

FB_IMG_1636228960191.jpg

FB_IMG_1636228977996.jpg
 
Halafu anatokea mtu asiye na uelewa anapiga mayowe "ooo Awesso hatoshi ,oooh Mh.Rais Samia hatoshi" 😳🤣🤣

#Siempre JMT
#Kazi Iendelee Kwa Kasi & Weledi Zaidi 💪
 
HILI ZEE INALOTANGAZA CHANJO HAPO CHINI LIMESIMAMA KAMA LINAFOKA HIV???
 
Halafu anatokea mtu asiye na uelewa anapiga mayowe "ooo Awesso hatoshi ,oooh Mh.Rais Samia hatoshi"

#Siempre JMT
#Kazi Iendelee Kwa Kasi & Weledi Zaidi
Unadhani mradi umeanza jana huo? Si unaona ridhwani mwenyewe nafsi imemsuta kamtaja Jiwe. Anajua bila yeye huo mradi ungekuwa historia. Mpaka anakufa mradi ulikuwa umefikia 70%. Ingekuwa ajabu wangeshindwa kuukamilisha wakati pesa ilishatolewa.
 
Halafu anatokea mtu asiye na uelewa anapiga mayowe "ooo Awesso hatoshi ,oooh Mh.Rais Samia hatoshi" 😳🤣🤣

#Siempre JMT
#Kazi Iendelee Kwa Kasi & Weledi Zaidi 💪
Sio wao ndugu yangu.. ni njaa za matumbo yao ndio zinazofanya wauze mpaka utu wao. Japo ni wa kuwaonea huruma lkn ndio hivyo huo ni uhalisia wa maisha yao.
 
Unadhani mradi umeanza jana huo? Si unaona ridhwani mwenyewe nafsi imemsuta kamtaja Jiwe. Anajua bila yeye huo mradi ungekuwa historia. Mpaka anakufa mradi ulikuwa umefikia 70%. Ingekuwa ajabu wangeshindwa kuukamilisha wakati pesa ilishatolewa.
Hayati Magufuli na mama Samia ni ndugu wa familia moja. Na wote wanatumia jina la ukoo ambalo ni CCM. Kwahiyo tunaupongeza ukoo wa mzee CCM kwa kutuletea watoto bora na wenye upendo wa kweli kwa Taifa lao.
 
Unadhani mradi umeanza jana huo? Si unaona ridhwani mwenyewe nafsi imemsuta kamtaja Jiwe. Anajua bila yeye huo mradi ungekuwa historia. Mpaka anakufa mradi ulikuwa umefikia 70%. Ingekuwa ajabu wangeshindwa kuukamilisha wakati pesa ilishatolewa.
Kuna miradi ya kikwete ilifikia 80+% na haikumalizwa (kwa makusudi), km huyu ssh anaimalizia kwa upendo tu ya mwenzie basi anaxtahili sana pongezi
 
Mradi wa Chalinze ulianza tangu enzi za Kikwete na ulijengwa na Wachina. Pump house pale Wami na matenki pande zote mbili kwenda Himo na kuja Chalinze karibu yote yalikuwa yamekamilika.
 
Mradi wa Chalinze ulianza tangu enzi za Kikwete na ulijengwa na Wachina. Pump house pale Wami na matenki pande zote mbili kwenda Himo na kuja Chalinze karibu yote yalikuwa yamekamilika.
Ni tofauti,huu sasa unatoa maji ruvu sio wami,ulianza majuzi wakati wa mwendazake ,Rais wa miundombinu mbinu Yule,kwa apo anastaili pongezi
 
Dah aisee umenikumbusha mbali sana bingwa wangu.. By the way Mungu wetu hajawahi kukosea ktk maamuzi yake. Kamchukua kiumbe wake ili akampumzishe kwa kazi kubwa aliyotufanyia ktk nchi yetu na katuachia huyu ili amalize yale mazuri yalioachwa na mtangulizi wake.
Hakika mkuu wangu 👍
 
Back
Top Bottom