Mr President Magufuli: Ipo siku watakuja kujua hekima uliyoitumia katika kutatua janga hili

Wenzio wamesubiri toka januari, sasa sijui hiyo kidogo ni muda gani

Sent using Jamii Forums mobile app

Toka January walikuwa wanasubiri nini wakati ugonjwa umeingia March 16?

Au walikuwa wanaahidiwa kuwa huu ugonjwa wa weupe, au ugonjwa wa nchi za baridi, au usio wa watu weusi huku kwetu hautafika wakati tukigoma kuwazuia wale wachina watalii marafiki zetu kuingia nchini?

Au siyo kile kipindi cha Profesa Kabudi kutuhabarisha ya Wuhan kabla hajaingia mitini mazima?
 
Zunguka Tanzania nzima kama unaweza Dar Es salaam pekee kuuliza kila family kam kuna mwana family Kati yao amekufa na Corona ?

Alafu hesabu

Ndo utakapojua hizi ni propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
.
tapatalk_1589327108185.jpg
tapatalk_1589327124601.jpg
tapatalk_1589327171588.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • tapatalk_1589327171588.jpg
    tapatalk_1589327171588.jpg
    106.5 KB · Views: 1
  • tapatalk_1589327124601.jpg
    tapatalk_1589327124601.jpg
    101.6 KB · Views: 1
Kwa hilo neno nakupa pongezi. Hakika hata mimi huwa najiuliza wanaomponda, kumpinga, kumbeza na kumtukana Rais Magufuli, pasipo kuwa na hoja, lengo lao ni nini, na ni akina nani?

Angalau baadhi wanajulikana km Mangi Kimambi au Fatuma Karume aka Shangazi, kuwa wana matatizo yao binafsi. Lakini mtu kama Kigogo@kigogo2014 (twitter) anashabikia viongozi wa upinzani kiasi cha kuamini ni mmoja wa viongozi wao ngazi za juu.

Yote kumi, tisa ni ukweli kwamba hajatokea Rais makini na mwenye maono kama Dr Magufuli. Baadhi ya mifano, ukiacha jinsi anavyowaasa Watanzania kukabiliana na janga la COVID-19, ni Sera yake ya uchumi wa viwanda. Sera hii ni kama Rais Magufuli alitabiri ujio wa gonjwa hilo ambalo limelazimisha nchi zenye viwanda kusimamisha uzalishaji kwa sababu ya "lockdown". Tungeendelea kutegemea bidhaa za nje, hali kwa sasa hivi ingekuwa ni balaa kwa ukosefu wa bidhaa hizo. Hali ya upatikanaji wa bidhaa kutoka nje, kwa sasa, haijawa mbaya sana kwa sababu maduka bado yana akiba.

Changamoto ya kukosekana kwa bidhaa kutoka nje ni fursa ya viwanda vyetu kuongeza uzalishaji wa bidhaa hizo na kwa ubora zaidi, kukidhi mahitaji ya ndani na nje, hasa nchi majirani zilizoamua " lockdown" na SADC, pale watakapofungua mipaka yao. Isitoshe kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa ndani ya nchi ni fursa ya kiuchumi kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wachimbaji, kwani nao pia wataongeza uzalishaji kukidhi mahitaji ya viwanda.

Tuachane na hao viongozi wanaoamua kujifungia ndani badaala ya kushiriki na wapiga kura kupambana na janga la korona. Baada ya kutoka kwenye "self-isolation" yao tunategemea wataendeleza madai yao ya Tume Huru, Demokrasia, Haki na Uhuru, pasi kuonesha nia ya dhati ya kuwaondolea wapiga kura kero zao za maendeleo. Kwa maana madai hayo kimsingi ni ya ubinfasi wa uchu wa madaraka.

Nani Kiongozi kama Rais Magufuli ambaye anaamini kuwa Tanzania bila korona inawezekana iwapo kila mtu atazingatia ushauri wa kitaalamu wa kujikinga dhidi ya maambukizi ya COVID-19, utolewao na kuhimizwa na mamlaka husika. Hapa ndipo viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa msitari wa mbele kuhamasisha wanachama wao.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE UWAPENDAO
 
Nyie ndo wachawi kabisa watu wanapukutika eti tutakua kukumbuka ujinga huo citaki kuniaminisha kwamba JPM ni ginius duniani hi hata kuliko Papa putini wana science wa WHO kaupata wapi u ginius wa kuona vitu vya mbali kuliko na Raisi wote wa dunia......
Pole sana iwapo familia na ndugu zako wamepukutika! Kama ni hivyo mjinga atakuwa wewe unayejua jinsi ya kupambana na gonjwa hili la hatari, kuliko JPM, na bado familia/ndugu zako wakapukutika. Bado zamu yako.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE WAPENDWA WAKO
 
Nonsense, hujauona mziki wenyewe, pamoja na kwamba taarifa zinafichwa lakini subiri kidogo utarudi tena kuukana upuuzi wako ulioandika.The truth will shortly be on billboards

Nawe pia umepoteza ndugu, au vipi unaombea mabaya wasio ndugu zako ili unachotarajia kitokee, kwambs The truth will shortly be on billboards? Roho mbaya hiyo.

JIKINGE UMKINGE JIRANI

JILINDE UWALINDE WAPENDWA WAKO
 
Unawasilisha nini sasa wakati hizo hekima hujazitaja?

Yani hata hatujui kama una point au huna, kwa sababu uneonesha uvivu wa kufikiri kwa kutotaja hekima hizo ni zipi na tunajuaje ni hekima kweli na si ndoto zako tu?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unawasilisha nini sasa wakati hizo hekima hujazitaja?

Yani hata hatujui kama una point au huna, kwa sababu uneonesha uvivu wa kufikiri kwa kutotaja hekima hizo ni zipi na tunajuaje ni hekima kweli na si ndoto zako tu?



Sent using Jamii Forums mobile app
Kiukweli katika tanzania kujadili mambo imekua ni kelele tu... watu hawaji na majibu kinachobaki ni shutuma, lawama ama kuunga mkono mawazo ya mtu fulani ili mradi tu mtu kaongea.... yaani ni kelele tu... kila kitu kinajadiliwa juu juu tu.... dah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiukweli katika tanzania kujadili mambo imekua ni kelele tu... watu hawaji na majibu kinachobaki ni shutuma, lawama ama kuunga mkono mawazo ya mtu fulani ili mradi tu mtu kaongea.... yaani ni kelele tu... kila kitu kinajadiliwa juu juu tu.... dah

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni ukosefu wa lishe na madini fulani ubongoni?

Au ni uvivu wa kiutamaduni tu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Jamaaa atakuwa ni lusekelo Au gwajima, eti zunguka uone Kama utapata aliekufa, hivi Wakati wizara inatoa maelekezo kuwa sasa watu watazikwa mchana wasizikwe usiku na kukiri kuwa walikuwa wanawazika usiku na kuwakataza waganga wa serikali kuwazika usiku yeye alikuwa Mombasa anashughulikiwa Nyuma? Au alikuwepo hapa Tanzania? Hivi huyu anasema eti zunguka Kama utawaona waliokufa kwa corona, na Wakati akienda kwenye taarifa ya wizara inasema kuna idadi ya watanzania waliokufa kwa corona, sasa yeye na serikali nani anajua zaid? Hawa watu Aisee wanaimba mapambio Lakini tuwasamehe hawajui waimbacho

Sent using Jamii Forums mobile app
Nashani huyu @xaskegy ndiyo haya marobot ya Lumumba Buk 7. Hayana uwezo kutumia akili zao, yamesetiwa kubisha tu
 
Kwa hiyo kama hakuna kupima unajua je watu wanakufa kwa corona. Tusiwe wepesi wa kuamua. La msingi hapa umeambiwa ya kufanya tunalaumu bila kutumia busara tulizopewa na mwenyezi Mungu ushauri unaotilewa dunia nzima ndio huo uliotilewa kwa Watanzania tofauti ni moja tu ya kutofunga mipaka na kuruhusu watu kutoka. Mbona hamuilaumu Sweden ambako hakuna lockdown na bado kuna vifo na vingi tu. Wewe tumia busara yako kufuata maelekezo yaliyotolewa epuka mikusanyiko, ukiona huna sababu ya kutoka kaa ndani hujazuiliwa, ukitoka vaa barakoa, kaa umbali wa mita moja nazaidi na mwenzako mnayeingea, jihadhari na vitu unavyovishika na hakikisha unanawa mikono uone kama utaambukizwa au kuambukiza wengine. Kingine fuata ushauri wa kunywa limau na tangawizi kwa ajili ya kuimarisha kinga. Sasa mnataka Tanzania itufanyie nini zaidi ya maelekezo hayo. Ila kwa kuwa baadhi yetu haturimizi ndio maana maambukizi yanaongezeka sio Rais tusimsingizie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo uwelewa kwenu unakuwa Mdogo, huuu ugonjwa ni mtambuka Mkuu, wewe utajilinda Lakini kumbuka kuna nafasi ya mtu mwingne kuweza kukuambukiza akiwa nao, unapoenda buchani yapo mazingira ambayo ni hatarishi na wewe huwezi kuyakwepa, ugonjwa huu unapaswa kujilinda wewe na kumlinda na mwenzako, ukisambaaa kwa watu wengi Sana hata wewe ulieepuka mikusanyiko kuna nafasi kubwa ya wewe pia kunasa, utaenda Dukani utakutana nao pale ambapo muuzaji atashika bidhaa na kukupatia, utanunua mboga za majani zilizoshikwa na watu wengi utanasa, utaenda Kusaga utashika kitu, utapita mahali kwa Bahati mbaya utashika sehemu, huuu ugonjwa ili uudhibiti ni kuzuia watu wengi wasiupate Mkuu, ndio maaana unaona nchi zinaomba kupigana pamoja.
Unaowaona wanalalamika juuu ya kutoudhibiti wako Sahihi Mkuu, hiii ni vita Ya pamoja sio ukimwi huuu, tatizo nyie mnakuwa wabishi mno, halafu unaposema kuwa mtu Kama naona vipi si akae yeye home Au ajitenge, unasahau kuwa kuenea kwa ugonjwa hata ukijetenga kuna madhara mengne ya kiuchumi na kijamiii mfano una baar iliyokuwa inalisha familia yako utaifunga utakosa hela, shule zitaendelea kufungwa watoto wako wataadhirika kimasomo, wengne ni wafanyakazi wa kampuni hizo kampuni zitafungwa je utawalisha hao wafanyakazi? Mnatetea ujinga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lini tena? Tayari wengi tumeshajua......Nchi nyingi zilizoweka lockdown tayari zimeondoa licha ya kuwepo na ongezeko la maambukizi...Russia ni mfano pamoja na Nchi kadhaa za ulaya...Uingereza nayo imo...waliobaki ni wapiga kelele tu mitandaoni wengi hapa kwetu wakiwa ni wafuasi wa chama Fulani Cha siasa...
 
Jambo kubwa atakalo kumbuka ni yeye kujiokoa na wanafamilia wake kwa kujifungia Chato na kuwaacha wananchi peke yao na kuwahimiza watu wachape kazi.
 
Back
Top Bottom