Mr President Magufuli: Ipo siku watakuja kujua hekima uliyoitumia katika kutatua janga hili

XASKEYGY

Senior Member
Mar 29, 2020
124
225
Habari wana JF.

Naomba na Mimi nitoe yangu ya moyoni kidogo maana kila nikipita huku ndani nakuta watu wakimuongelea tu rais wetu kwa hatua anazochukua kuhusu hili janga la Corona.

Wengine wakimpongeza na wengine wakiponda lakini inaonekana wanaoponda ni wengi kukiko wanao support.

Ila wacha niwaambie kitu kimoja Watanzania wenzangu ambacho huwenda wengi wakabeza na kukejeli.

Ipo siku tutakuja kujua Hekima aliyotumia Rais wetu mpendwa katika kupambana na hili janga.

Na naamini watu wote walio na uadilifu na kupenda kuondea ukweli.

Watajitokeza na kumpa pongezi na kupewa tuzo.

Naomba kuwasilisha.
 

google helper

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
8,676
2,000
nyuzi ni nyingi kwa kweli hata ya kwako inaongeza idadi tu sioni hasa dawa ya unachosema zaidi ya kuongea na pande zote kuvutana ili kupata muafaka
 

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,499
2,000
Nyie ndo wachawi kabisa watu wanapukutika eti tutakua kukumbuka ujinga huo citaki kuniaminisha kwamba JPM ni ginius duniani hi hata kuliko Papa putini wana science wa WHO kaupata wapi u ginius wa kuona vitu vya mbali kuliko na Raisi wote wa dunia......
 

mysterio

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
5,611
2,000
XASKEYGY,
Nonsense, hujauona mziki wenyewe, pamoja na kwamba taarifa zinafichwa lakini subiri kidogo utarudi tena kuukana upuuzi wako ulioandika.The truth will shortly be on billboards
 

XASKEYGY

Senior Member
Mar 29, 2020
124
225
Nonsense, hujauona mziki wenyewe, pamoja na kwamba taarifa zinafichwa lakini subiri kidogo utarudi tena kuukana upuuzi wako ulioandika.The truth will shortly be on billboards
Zunguka Tanzania nzima kama unaweza Dar Es salaam pekee kuuliza kila family kam kuna mwana family Kati yao amekufa na Corona ?

Alafu hesabu

Ndo utakapojua hizi ni propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mwananchi

JF-Expert Member
Oct 4, 2012
2,932
2,000
Mpaka ijumaa ilikuwa hivi
Cases: 16,467
Deaths: 1,293
Recover: 118
Sasa unataka tumkumbuke kwa mauaji ya kimbali?
 

MICHAEL SON

JF-Expert Member
Apr 17, 2020
458
1,000
Zunguka Tanzania nzima kama unaweza Dar Es salaam pekee kuuliza kila family kam kuna mwana family Kati yao amekufa na Corona ?

Alafu hesabu

Ndo utakapojua hizi ni propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
200+ death na tunaendelea,,,,actual watu wanakufa hata KABLA ya corona,, ila mm sijapenda tu jinsi alivyo amua kuupuza kama hajpo
 

stella1975

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
873
1,000
Unajua mnashangaza Sana, yani hiyo njia aliyotumia kupambana na corona ni ipi? yani kuacha bar ziendelee, kuacha makanisa yaendelee, kutumia waganga wa kienyeji na wachungaji wa kilokole ndio njia Sahihi katika kudhibiti corona? Unajua umeongea hata ufafanuzi hujatoa kwa sababu huna Point nani kakuambia kuwa kulala kitandani pasipo kutumia chandarua ndio kudhibiti marelia? Maaana kitu pekee alichofanya cha kipekeee ni kuacha mikusanyiko iendelee tu ndicho cha kipekee au kuna njia tofauti iliyotumika?maaana kupima hapimi Watu au wewe huo mwenzetu umepimwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

stella1975

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
873
1,000
Zunguka Tanzania nzima kama unaweza Dar Es salaam pekee kuuliza kila family kam kuna mwana family Kati yao amekufa na Corona ?

Alafu hesabu

Ndo utakapojua hizi ni propaganda

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Jamaaa atakuwa ni lusekelo Au gwajima, eti zunguka uone Kama utapata aliekufa, hivi Wakati wizara inatoa maelekezo kuwa sasa watu watazikwa mchana wasizikwe usiku na kukiri kuwa walikuwa wanawazika usiku na kuwakataza waganga wa serikali kuwazika usiku yeye alikuwa Mombasa anashughulikiwa Nyuma? Au alikuwepo hapa Tanzania? Hivi huyu anasema eti zunguka Kama utawaona waliokufa kwa corona, na Wakati akienda kwenye taarifa ya wizara inasema kuna idadi ya watanzania waliokufa kwa corona, sasa yeye na serikali nani anajua zaid? Hawa watu Aisee wanaimba mapambio Lakini tuwasamehe hawajui waimbacho

Sent using Jamii Forums mobile app
 

gongolamboto

JF-Expert Member
Feb 21, 2011
1,125
2,000
Unajua mnashangaza Sana, yani hiyo njia aliyotumia kupambana na corona ni ipi?yani kuacha baar ziendelee, kuacha makanisa yaendelee, kutumia waganga wa kienyeji na wachungaji wa kilokole ndio njia Sahihi katika kudhibiti corona? Unajua umeongea hata ufafanuzi hujatoa kwa sababu huna Point nani kakuambia kuwa kulala kitandani pasipo kutumia chandarua ndio kudhibiti marelia? Maaana kitu pekee alichofanya cha kipekeee ni kuacha mikusanyiko iendelee tu ndicho cha kipekee au kuna njia tofauti iliyotumika?maaana kupima hapimi Watu au wewe huo mwenzetu umepimwa?

Sent using Jamii Forums mobile app

Hizo sehemu ulizotaja zote hakuna anayelazimishwa kwenda. Kila mtu anaenda kwa hiari yake. Kama unaona ukienda huko utapata corona ucha kwenda. Waziri mkuu alishatangaza bila chenga, kama huna jambo la muhimu la kufanya mtaani usitembee. Mlitaka kauli gani tena?
 

mushairizi

JF-Expert Member
Nov 27, 2011
255
250
Unajua mnashangaza Sana, yani hiyo njia aliyotumia kupambana na corona ni ipi?yani kuacha baar ziendelee, kuacha makanisa yaendelee, kutumia waganga wa kienyeji na wachungaji wa kilokole ndio njia Sahihi katika kudhibiti corona? Unajua umeongea hata ufafanuzi hujatoa kwa sababu huna Point nani kakuambia kuwa kulala kitandani pasipo kutumia chandarua ndio kudhibiti marelia? Maaana kitu pekee alichofanya cha kipekeee ni kuacha mikusanyiko iendelee tu ndicho cha kipekee au kuna njia tofauti iliyotumika?maaana kupima hapimi Watu au wewe huo mwenzetu umepimwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo kama hakuna kupima unajua je watu wanakufa kwa corona. Tusiwe wepesi wa kuamua. La msingi hapa umeambiwa ya kufanya tunalaumu bila kutumia busara tulizopewa na mwenyezi Mungu ushauri unaotilewa dunia nzima ndio huo uliotilewa kwa Watanzania tofauti ni moja tu ya kutofunga mipaka na kuruhusu watu kutoka. Mbona hamuilaumu Sweden ambako hakuna lockdown na bado kuna vifo na vingi tu. Wewe tumia busara yako kufuata maelekezo yaliyotolewa epuka mikusanyiko, ukiona huna sababu ya kutoka kaa ndani hujazuiliwa, ukitoka vaa barakoa, kaa umbali wa mita moja nazaidi na mwenzako mnayeingea, jihadhari na vitu unavyovishika na hakikisha unanawa mikono uone kama utaambukizwa au kuambukiza wengine. Kingine fuata ushauri wa kunywa limau na tangawizi kwa ajili ya kuimarisha kinga. Sasa mnataka Tanzania itufanyie nini zaidi ya maelekezo hayo. Ila kwa kuwa baadhi yetu haturimizi ndio maana maambukizi yanaongezeka sio Rais tusimsingizie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
6,561
2,000
Wengine wakimpongeza na wengine wakiponda lakini inaonekana wanaoponda ni wengi kukiko wanao support
"NI UPEPO, UTAPITA" A quote from the 4th President of the United Republic of Tanzania, His Excellence JM Kikwete
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom