Si unajua tena shem nikikutiaga machoni mwenzio ninakuwa "distracted"....
Naona twisheni ya Kisukuma inafanya kazi. Hongera sana kwa jibu lako murua
yeye issue kwake bwana Ruge nikusaka mahale, hata kwa kunyonya jasho la wasanii hawa duni....Mimi ninafanya biashara na wasanii huwezi ukaniambia niache kutafuta wasanii wakati nahitaji hela, matatizo yake amalizane nao huko huko" Ruge alisema
mzee.. wakati mwingine hawa wenzetu huwa wanaweza kufanya lolote lile. Ungeona mawasiliano yetu na dada yule wa Vodacom ungejua jinsi gani tumemdharau. Sasa nikiyaona haya naombea isiwe kweli..
Usicheze na Ruge , kiboko ya wasanii, peleka dili then una achwa kwenye mataa , hii nikawaida kwa Tanzania lakini , pole sana SUGU nend amahakamani!
Tutanzisha kampeni ya RUGe asipewe usimamizi wa hiyo Mastering Studio ndio tumeshaanza maandalizi tuna anza na maandamano, no voting mbaka RUge awe pembeni..JK hatutaki RUge
............Na hii tunayoiona hapa Tanzania ni cha mchezo tu na wenzentu walishapitia huko zamani sana na walishauwana sana tu na hadi leo hii kuna wengine wanaogopa kabisa kushika Mic kwani mabwana zao watakuja hapohapo na kudai kipato chao chote. Kama hii isipotulizwa mapema, basi tusishangae tukafika huko very soon kwenye kutishiana maisha au kuuwana.
Si unaona sugu nae, kwenda hivyo je kama ndiyo angelikuwa na pass kama akina Ruge si ingekuwa balaa, jamaa kalimwa swali, wewe hauna tatizo lolote na Sugu na Sugu na wewe, nini kilichofanya aandikiwe barua ya kuitwa mahakamani na kuombwa sijui mpaka Jumatatu?
Nchi hii bana, yani mtu anakuja ofisini, eti jamani naomba mumuandikie barua Sugu ya kumtaka asitishe madai yake mpaka Jumatatu, na mahakama nayo inafanya kama ilivyoombwa damn, eti nimeitikia wito wa taifa ndiyo maana nikawalipa wasanii wiki moja kabla, kwani hao wasanii wakiombwa watumbuize bure watakataa?
Lakini nchi ilipofikia panatisha, yani baadhi ya watu wanaamua fanya lolote lile. Kichefu chefu yani, eti jana nimeongea na Sugu usiku nikamwambia sijui yeye hizo hela adai yeye ni mwanaume, lakini asiende kwenye press, sasa kwanini umemkataza asiende kwenye press kama hakuna kinachofichwa, watu wengine bana!
Halafu hizi ngono ninazosikia mnadai ili dada zetu ndiyo watoke, hivi mnataka mlale na wanawake wangapi ndiyo mjisikie nyie ndiyo wanaume? Watu wengine bana achaa tu...
Hivi wakati wa kuanzisha kampeni ya kuhamasisha kupima Virusi na JK alikuwepo kulikuwa na kiingilio chochote kile?
Oooh kumbe ndo maana wasanii wote (kasoro prof J) walioperform siku ile wako chini ya management ya Ruge!!
Haya bwana....naona na mkuu anamnunulia Ruge Mastering Studio kwa pesa zetu za kodi!!
mie naona kama mchezo mzima ulipata baraka za mkulu.ni maoni tu kutokana na matendo yote yalivyokwenda.Inamaana kule kumvesha T shirt Mkulu ya Zinduka na kumwita usiku ule pale Leaders yote ilikuwa kumwingiza mjini watu wale mishiko? ama kweli sasa Mkulu umeruhusu watu wakufanye mtaji kama alivyosema Makamba kuwa wewe ni Mtaji.
Nakumbuka walivyo mwita kule Arusha afungue Hoteli kwa mbwembwe na kesho yake Tanroad wanaibomoa. Naona sasa nchi inaendeshwa kama kikundi cha Mdumange, maana kama Mkulu anafanywa mtaji naye anatabasamu tuu, ANATUDHALILISHA WOTE
hili dili la zinduka jamaa wameingia kichwa kichwa na misaada yao wajanja wenye njaa zao,sijui tamaa zao,sijui tabia zao wakaona hapa hapa mgeni njoo mwenyeji hapone.Hivi wakati wa kuanzisha kampeni ya kuhamasisha kupima Virusi na JK alikuwepo kulikuwa na kiingilio chochote kile?
ha ha ha gharama za ulinzi wa raisi wakati watu wanamwaga hela zao kutaka kusaidia kupambana na malaria inamana serikali wao hawana ulinzi wa kumpa raisi kuhudhuria jambo ambalo linasaidia wananchi wake? kweli jamaa huwa wanakuja na majibu ya kitoto kwenye mambo muhimu.Na hilo jambo Ruge analifahamu vizuri sana..................
Hayo ni maswali ya msingi amabyo Ruge anatakiwa ajibu
Mkuu Mwanakijiji.....
........yaani nami nilishangaa sana kumsikiliza Ruge anasema eti........."pale kutakuwepo na Rais.........gharama za ulinzi........" and then blah blah blah.......gimmee a break..........Ulinzi wa Rais?..............
Kwanini uwa-charge watu kiingilio ?.........hii bado haijakaa sawa.............tukio ambalo udhamini wake uko nje nje........tena hao wakubwa ndio walitakiwa walipe zaidi ili Raia wa kawaida apate kushiriki kisawasawa............
ukiambiwa ikulu nako kuna fungu la maana lilitengwa kwa ajili ya rais kwenda zinduka utakataa?jaribu kuulizia pale utaambiwa mamilioni mangapi yalitumika,hiyo ndio bongo dalisalama,watu wanapiga dili kushoto,kulia,nyuma,mbele,hadi wadanganyika tunapata kizunguzungu.ha ha ha gharama za ulinzi wa raisi wakati watu wanamwaga hela zao kutaka kusaidia kupambana na malaria inamana serikali wao hawana ulinzi wa kumpa raisi kuhudhuria jambo ambalo linasaidia wananchi wake? kweli jamaa huwa wanakuja na majibu ya kitoto kwenye mambo muhimu.
zile harusi za marafiki na ndugu anazokwenda raisi huwa gharama za ulinzi analipia nani?
Sugu alihojiwa jana live na station moja ya radio ya hapa Bongo,amezungumza maneno yaliyonisikitisha sana kama mtanzania mpambanaji. Jamaa anapigana sana na maisha kama kijana lakini wayu wenye connections wanakuja kumnyang'anya tonge mdomoni. Anasema alisikitika sana katika waliotajwa kufanikisha tamasha hilo,jina lake halikutajwa kabisa wakati amefanya kazi kubwa sana na katumia pesa nyingi sana. Jamaa alistahili hata appreciation tu.
Anasema proposal yote kaindaa yeye kasoro mambo machache tu ambayo yameongezewa na akina RUGEMALILA MUTAHABA kama viingilio,kufanyika usiku nk. Jamaa ameongelea jinsi urafiki uliopo kati ya January Makamba na Rugemalila pamoja na clouds jinsi ulivyosababisha Sugu na Deiwaka Productions wapokonywe kazi ya kuandaa tamasha hilo.
BALOZI MARK GREEN
Sugu akiwa anafanya michakato ya tamasha hili alikuwa akiwasiliana na aliyekuwa balozi wa Marekani hapa kwetu Mark Green ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa shirika la Malaria No More mpaka inafikia mahali Green anamwambia itabidi washirikiane na akina Ruge kwani yeye Sugu ndiye mwanzilishi wa idea.
MLAWA WA IKULU
Sugu pia alielezea jinsi alivyokutana na msaidizi wa Rais anayeitwa Mlawa kwa maelezo yake alimpa ukweli wote na kumuomba amkutanishe na Rais kabla ya tamasha. Lakini huyo bwana Mlawa akamkatisha tamaa kwa kumshauri kuwa kwa issue ilipofikia imekuwa complicated na aachane nayo.
RUSHWA KWA WANAHABARI
Baada ya kuongea na vyombo vya habari, Sugu anasema kuna ushahidi kuwa counterparts wake walitembeza mlungula wa waandishi wa habari ili habari isitoke,lakini waandishi wngine ambao wanaheshimu kazi yao na weledi walitoa habari kama kawaida.
Maoni yangu
MAGONJWA KUGEUZWA DEALS
Kuna mtindo umezoeleka sana hapa kwetu kugeuza magonjwa kama deal. Mara ya kwanza hii naona uzinduzi wa kampeni kupinga ugonjwa watu wanatoa kiingilio.UKIMWI na MALARIA ni magonjwa yaliyosumbua taifa letu kwa muda mrefu sasa. Inatakiwa nia ya kweli iwepo katika kupambana nayo. Clouds FM, Ruge na wote mlioandaa hii kitu in atakiwa muwaombe radhi watanzania kwa kuwaibia pesa zao. Mnatakiwa kumuomba radhi Mh Rais kwa kumuaibisha kiasi hiki.