Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,745
- 25,677
Dah! Soukouss Stars walitubariki sana vijana wa miaka ya 90! Ile bendi yao, wanamuziki wote walikuwa ni Mastaa kweli! Enzi hizo tunaenda kuangalia video; kabla mkanda wenyewe wa siku hiyo haujaanza, tulikuwa tunaoneshwa kwanza trela!WanaJf wote wenye Miaka 40+ na walilelewa na Wazee wapenda Soukous lazima wamjue huyu Mzee, aliipa Gittaa mdomo na kuiiimbisha kadri alivyopenda yeye. Apumzike kwa Amani