Mpiga filimbi wa Hamelin! Deliver every promise

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,443
Reaction score
860,269
Hadithi yenye funzo kubwa! Nani anaikumbuka? 1427570781403.jpg filimbi ya kwanza ilikuwa kuwafukuza panya 1427570800278.jpg filimbi ya pili ilikuwa ya kulipa kisasi kwakuwapoteza watoto

timiza ahadi yako na kamwe usidhulumu cha mtu
 
Naikumbuka sana hiyo hadithi. Mwisho wa siku watoto wa kijiji kizima wakatoeshwa?
 
Nakumbuka nikiwa darasa la nne nilinunuliwa Kitabu chenye hadithi 50 mbalimbali na hii ilikuwa moja wapo; The Pied Piper of Hamelin.
 
Sikuwahi kusoma hiki kitabu ila baba aliwahi kunihadithia hii hadithi!
 
sijui kama naikumbuka vizur watoto walichukuliwa wakaenda mlima ......aaarrgghh nimesahau tena

naisubiri kwa haaaamu
Ni simulizi ya mwaka 1300 kwenye mji wa Hamelin huko Ujerumani
Huo mji ulikuwa ni sugu kwa ugonjwa wa tauni unaosababishwa na panya ambao walikuwa wengi kupitiliza kwenye huo mji...wakazi wa hamelin walishajaribu kila namna kuwadhibiti wale panya lakini ilishindikana kabisa

Siku moja alikuja mgeni mwenye mavazi makuukuu akiwa kabeba filimbi na kuwaambia wenyeji wa hamelin kuwa angeweza kuwaondolea baa lile la panya
Kwa muonekano wake wa kifukara hawakuamini kuwa angeweza kufanya hiyo kazi hivyo wakampa sharti la kumlipa baada ya kazi kukamilika
Jamaa hakubisha akaanza kazi mara moja kwa kupuliza filimbi yake ambapo mapanya yote yalitoka kwenye kila tundu kila ficho na kila nyumba na kumfuata
Aliendelea kupuliza filimbi yake huku akielekea upande wa mji kulikokuwa na mto mkubwa huku maelfu ya panya yakimfuata nyuma . ...kufika pale mtoni alisimama na kila panya aliyefika pale alirukia majini na kupotea...baada ya panya wote kupotelea majini alirudi mjini kudai ujira wake
Watu wa hamelin kwa ujuha wao wakamzingua na kugoma kumlipa ujira wa kazi yake, Jamaa akaondoka na kinyongo chake
Siku tatu baadae Jamaa alirejea Hamelin nyakati za jioni hivi na kuanza kupiga filimbi yake huku akielekea upande mwingine wa mji kulikokuwa na mlima mrefu...filimbi ya kipindi hiki haikutoa panya bali watoto wote wa mji wa hamelin
Wazazi walijaribu kuwakataza watoto wao wasimfuate bwana yule lakini haikuwezekana...alipofika pale mlimani, mlima ulifunguka naye akazama na kupotelea huko na wale watoto wote
Aliyesalimika ni mtoto mmoja mlemavu wa miguu ambaye aliachwa nyuma na mpaka anafika pale mlima ulikuwa umeshajifunga
Huyu ndie aliyerudi mjini na kusimulia kilichotokea (left to tell)
 
ndio hiyo hiyo sema Mimi niliyoisoma ilibadilishwa kidogo hapo kwenye miji lakini kwingine kote kupo sawa ila kitambo sana ilikuwa ni primary
 
Back
Top Bottom