Mpenzio akikushushia heshima, wewe utafanyaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpenzio akikushushia heshima, wewe utafanyaje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Papa Mopao, Jul 31, 2011.

1. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#1
Jul 31, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180
Mpenzio/ Mumeo au Mkeo....
Akikushushia heshima kwa namna hii:

"Kenge wewe!" au " Kima mkubwa wewe kampe mamako!"

Wewe utamchukuliaje au utachukua hatua gani? Vipondo vya kufa mtu au talaka au kumpiga chini!

Kujua kutukana nako kunadhihirisha picha nzima ya malezi!

Ni hayo tu...

2. The Boss

The Boss JF-Expert Member

#2
Jul 31, 2011
Joined: Aug 18, 2009
Messages: 37,826
Likes Received: 22,463
Trophy Points: 280
Hayo ni matokeo
kuna kitu kilishavunjika siku nyingi hapo..

3. Mwendabure

Mwendabure JF-Expert Member

#3
Jul 31, 2011
Joined: Mar 10, 2011
Messages: 2,051
Likes Received: 277
Trophy Points: 180
Mkuu mbona hujafafanua ni kwa mazingira gani mpenzio anakushushia heshima yako? Uchumi umeshuka ghafla? Umepata ugonjwa au ulemavu uliokusababishia kushindwa kumridhisha ktk unyumba? Amekuzidi kwa kipato, umri, elimu au kitu gani? Binafsi nashindwa kuchangia kwa hakika.

4. Likwanda

Likwanda JF-Expert Member

#4
Jul 31, 2011
Joined: Jun 16, 2011
Messages: 3,854
Likes Received: 45
Trophy Points: 145
Ni vizuri kuepuka malumbano ya moja kwa moja (Dialogue), kwa maana sio kwamba itawashushieni wote heshima bali itaochoche ugomvi kuwa mkubwa zaidi. Wakati mwingine hutokea labda mtu aliyetoa maneno machafu kwa mwenzie amepata mghafiriko au amelewa hivyo ni kumsubiri hadi hasira zake au pombe iishe kwanza ndipo kuuliza ilikuaje mpaka akatoa maneno kama hayo. Kama mtu anaendelea na tabia kama hizo ni vizuri kumuepuka kabisa kuliko kuwa mnatukanana maana ukifanya hivyo utajikuta na wewe unakuwa na tabia zile zile za matusi.

5. s

shosti JF-Expert Member

#5
Jul 31, 2011
Joined: Dec 21, 2010
Messages: 4,949
Likes Received: 28
Trophy Points: 145
kwenye malumbano chochote kinweza kutokea,ila mpaka kufikia hapo hadhi yako ishashuka kwa kweli!

6. Meritta

Meritta JF-Expert Member

#6
Jul 31, 2011
Joined: Apr 26, 2011
Messages: 1,304
Likes Received: 7
Trophy Points: 0
mi sijaolewa sa sijui itakuwaje, ila nikiolewa nitajua

7. Rose1980

Rose1980 JF-Expert Member

#7
Jul 31, 2011
Joined: May 10, 2010
Messages: 5,701
Likes Received: 28
Trophy Points: 0

sasa mbona ushatoa jibu?

kukutukana,dharau na mizaha isiyokuwa na adabu vnatokana na malez/makuzi ya mtu

kumdunda si suluhisho...kaa naye kwa upendo na amani na umwelekeze kwa utaratibu m sure HATARUDIA tena kudharau au kukutukana.....

ukkimpiga haisadii..itakuwa ni sawasa na nikikutukana unanipiga then basi maisha yanaendelea...

kwa mfano;

umemkanyaga mtu kwa bahat mbaya afu ukashtuka dahh kumbe nimemkanyaga mtu ...ahhh wakat unataka tu kusema samahan ndugu yule jamaa akaanza ahh we ***** nini unankanyaga union...? we pumbavu nini?....NAMBIE VP APO APETITE YA KUSEMA SAMAHANI SIKUKUONA ITAKWEPO?..AS HUMAN BEING HALI ITAJISWCH AHH ASI USHANITUKANA SASA NKUOMBE MSAMAHA WA NIN...na apo pia km wew pia matusi yamejaa mtaendelea kutukanana...lakin km umemkanyaga na ukageuka ukaona anatabasamu/au anakwambia haina shda ..usijali...LAZIMA UTASEMA AHH POLE BWNA SIKUKUONA NDG YANGU...

usilipize ubaya kwa ubaya..iwe makusudi au umetendewa kwa bahat mbaya....

8. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#8
Jul 31, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Utajuaje kwamba kitu kilishavunjika siku nyingi? Na kama mtu tayari yuko kwenye ndoa hapo atavumilia katika mvunjiko mkuu?

9. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#9
Jul 31, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Labda kifupi niseme hivi:
Mtu anakushushia heshima kwa njia ya kukusema vibaya au kukutolea lugha chafu mpaka wewe unashindwa kuvumilia mitusi, sasa katika mazingira kama hayo huyo ni mumeo au mkeo! Hilo ni la kutokea katika mazingira yoyote kama ulivoainisha katika post yako na pia ni la mara kwa mara! Sijui kama umenipata vema?

10. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#10
Jul 31, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Tumekupata vizuri sana mkuu, kuepuka kweli ni njia nzuri lkn unakuta mwenzio anakupa mitusi mibaya kiasi kwamba ukimvumilia kwa muda mrefu mpaka inafika mahali hasira inakufika shingoni, sasa kwa mtu wa dizaini hiyo si ataleta vurugu pale?

11. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#11
Jul 31, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Shosti! Kama hadhi ishashuka ukiwa kama mume au mke, kwa maisha yaliyobakia utamchukulia kama vile hadhi yake ni ndogo?

12. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#12
Jul 31, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Siyo mbaya, omba Mungu akujalie neema ya kumpata mwenzi bora dada yangu! Usihofu!

13. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#13
Aug 1, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Rose! Mchango ni mzuri sana, ila kuna kitu kimoja, mtu amelelewa katika mazingira hayo,kumkalisha chini kwakweza kutokea mambo mawili, moja atabadilika lingine hatabadilika. Sasa kama mtu habadiliki baada ya kumwelewesha kwa upendo kwamba analofanya si nzuri, na bado anarudia kosa lile lile kila mara na kila siku, huyo kama mumeo au mkeo, utachukua hatua gani ingawa malezi aliyolelewa tuseme amepitia katika walakini mkubwa?

14. Elia

Elia JF-Expert Member

#14
Aug 1, 2011
Joined: Dec 30, 2009
Messages: 3,442
Likes Received: 3
Trophy Points: 135
Akikwambia kenge wewe, mwambie heh kumbe unalala na kenge. unachotakiwa ni kuboresha tusi lake tu usianzishe lingine...

15. Tulizo

Tulizo JF-Expert Member

#15
Aug 1, 2011
Joined: Jun 13, 2011
Messages: 849
Likes Received: 21
Trophy Points: 35
Papa Mopao..Lugha ni makubaliano..hata kule kwa wazungu wanaitana "Nigga, dawg.etc." ni makubaliano... unaweza kwenda nyumba ya mtu ukasikia mtu anamwita mume wake "kalume kenge" ukataka kukimbia ..halafu kidogo ukasikia mme anajibu kwa upendo..na pozi la mahaba .."sema malaya wangu"..

Mabadiliko ya makubaliano ya lugha ndani ya nyumba ni mazao (result/outcome) ya vitu vingine ambavyo vilitakiwa kurekebishwa wakati huo.. cha kurekebisha sio lugha ila ni masuguano ambayo inavunja amani.... Kama mtarekebisha hayo mapungufu mengine basi hata lugha nayo kama ni mazao (outcome) nayo itabadilika.. Inaweza isiwe kama lugha ambayo jamii inavyotaka lakini..ni ile lugha ambayo inayokubaliwa ndani ya mipaka ya nyumba au mahusiano yenu..

16. Mwanamayu

Mwanamayu JF-Expert Member

#16
Aug 1, 2011
Joined: May 7, 2010
Messages: 7,936
Likes Received: 2,085
Trophy Points: 280
Kama ni mchumba au mpenzi wako tu basi ni kupiga chini instantly! Kama ni mkeo au mumeo; mimi hapa taongelea kama ni mkeo basi wewe mtazame tu, tena ikiwezekana kuwa na furaha kwani hiyo ni nafasi nzuri ya kumtambua zaidi mkeo kwani alikuwa ameficha makucha yake na sasa anayatoa basi wewe unakuwa mtulivu na kutafuta nail cutter ya size yake kwa taratibu.

Pia unamwuliza behaviour ya kenge na kima halafu una-behave kwake kama hao kenge na kima mpaka atakapo withdraw hizo statements zake!!!

17. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#17
Aug 1, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Duh sasa hapo rafiki yangu, jino kwa jino haipendezi! Kwa kufanya hivyo utaalamu wa kutukana utakuwa hali ya juu mno.

18. Papa Mopao

Papa Mopao JF-Expert Member

#18
Aug 1, 2011
Joined: Oct 7, 2009
Messages: 3,353
Likes Received: 387
Trophy Points: 180

Hahaha! hiyo staili ya kupeana lugha mbofu kweli kali. Kama ni makubaliano sawa nakubaliana wewe, twende zile ambazo hazina makubaliano!

19. Smile

Smile JF-Expert Member

#19
Aug 1, 2011
Joined: Jul 18, 2011
Messages: 15,431
Likes Received: 194
Trophy Points: 160
yaani iyo ni stage mbaya sana katika mapenzi hapo kuna ugonjwa siku miingi sasa ndo umechipuka.yaani amekuchoka so heshima kushnei.cha kufanya kama ni mkeo/mumeo mvumilie muonye tu kwa upendo maana sio jambo zuri kabisa kama ni mpenzi mmmmmmmmmmh hana adabu mpenzi tu na matusi chagua kilicho jema

Loading...