Mpenzi wangu wa zamani anaolewa kesho..

Mpenzi wangu wa zamani anaolewa kesho..

kwanini mkuu... ???

Mdada ni mzuri sana na anaongea politely. Kama sio mchunguzi huwezi kujua mienendo yake kabisa. Ila mtu kama mimi lazima nikufahamu tu kama si leo kesho:

1.Ana tabia ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja tena haonyeshi kumwachi mmoja

2. Mvivu sana na bahati mbaya anapenda kuonyesha anatoka familia ya matawi ya juu

3. Mwongo sana na hili ndilo gumu sana kuligundua toka kwake. Nilipogundua hii tabia akatokea kuniogopa sana sana. Na naamini itamchukua muda mrefu kwa huyo mtarajiwa wake kugundua hiyo tabia.

4. Tegemezi kupita maelezo

Tena hata leo alitaka kuja kwangu. Can you imagine mchumba wa mtu tena umebakisha siku kadhaa kufunga ndoa unataka kuja kwa B/F............tena si mara moja.

Honestly namuonea jamaa huruma, ingawa nina imani pengine atabadilika.
 
Ngoja nijipe moyo nitapata anayenifaa..

Chichunguze vizuri isije kuwa kati ya hao wannne hakuna aliyeona ungemfaa! tehe tehe!!!!!
 
Pole sana ilo sasa ni fundisho.. angalia no one is perfect under the sun so ukichagua sana
really utaumia mwenyewe
 
Malizia tenzi yako siku ile mnaaachana alikwmabia nini mpaka sasa anaolewa na kukuletea card ya mualiko

Wewe nenda na siku ukimpata wa kumuoa nawe mpelekee mualiko (kuachana sio kujengeana chuki na hasama)
 
he he he he, pole weye

ukisusa wenzio wala yakheee

Jamaa ni mzee wa ku-identify vipaji kama Arsene Wenger alafu anaviachia kiurahisi wakati amedumu navyo muda mrefu, ndio hivyo tena GANDA LA MUWA LA JANA CHUNGU KAONA KIVUNO na MWENYE CHONGO NI MFALME KWA VIPOFU. Inabidi tumpongeze kwa kuwatunza vizuri mpaka wanaolewa
 
Alafu mkiachana na mtu katika mazingira ya utata huku wewe ndio mwenye makosa mara nyingi mkija kukutana unamkuta mtu wako yupo more than bomba na unatamani urudiane lakini inakuwa haiwezekani, nenda kanisani kwani anaweza asikubali kuolewa na huyo jamaa si unajua tena huwa wanauliza mara tatu
 
sikte moyo ndugu.wako atakupata ulipo siku zikifika,jipanguze machozi,nenda harusi kama ulivyo alikwa uonyeshe heshima,mpenzi wa zamani amekualikaa maanake anakuheshimu
just my opinion
 
ha ha ha, hii ni movie ama tamthilia?

Au ule wimbo wa 'do you believe in love' Jodeci?

Alafu mkiachana na mtu katika mazingira ya utata huku wewe ndio mwenye makosa mara nyingi mkija kukutana unamkuta mtu wako yupo more than bomba na unatamani urudiane lakini inakuwa haiwezekani, nenda kanisani kwani anaweza asikubali kuolewa na huyo jamaa si unajua tena huwa wanauliza mara tatu
 
Mdada ni mzuri sana na anaongea politely. Kama sio mchunguzi huwezi kujua mienendo yake kabisa. Ila mtu kama mimi lazima nikufahamu tu kama si leo kesho:

1.Ana tabia ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja tena haonyeshi kumwachi mmoja

2. Mvivu sana na bahati mbaya anapenda kuonyesha anatoka familia ya matawi ya juu

3. Mwongo sana na hili ndilo gumu sana kuligundua toka kwake. Nilipogundua hii tabia akatokea kuniogopa sana sana. Na naamini itamchukua muda mrefu kwa huyo mtarajiwa wake kugundua hiyo tabia.

4. Tegemezi kupita maelezo

Tena hata leo alitaka kuja kwangu. Can you imagine mchumba wa mtu tena umebakisha siku kadhaa kufunga ndoa unataka kuja kwa B/F............tena si mara moja.

Honestly namuonea jamaa huruma, ingawa nina imani pengine atabadilika.

dah kumbe... lakini huenda akaja kubadilika....
 
Ukishaachana na mpenzi mfute kabisa akilini, nenda mbele kwa mbele usirudi nyuma. Kuna wimbo wa Remy Ongala unaitwa mbelekwa mbele, ungekufaa sana mkuu!
 
pole sana kijana ukiona hivyo huwaga unapenda kuonja ipi sukari ipi chumvi ndo maana unaacha 2 watoto wa wa2 na huwaga wanaumia sana na ndo maana naye akaamua kukupa card ukaumie kama wewe ulivyo muumiza ndo ujifunze sio vzr kulamba alafu unatema
 
Pole sana, nahisi wewe una matatizo au muda wa kuoa hujafika, kwa sababu inaaminika kuwa wakati wa kuoa ukifika kwa mwanaume ataoa hata bila kuchagua, na kwa wadada wakati wa kuolewa ukifika atatamani sana aingie ktk ndoa na ikishindikana anafanya mpango wa kuzaa bila ndoa.

Hatuwezi kuibadili kweli isipokuwa kuifumbaza.
 
Back
Top Bottom