Mpenzi wangu kanipa ultimatum kuwa nisipomuoa mwaka huu, atachukua maamuzi magumu

Hata walio oa/kuolewa hawana majibu ya kuridhisha kwanini wameoa

1. Wapo waliooa kwasababu ya shinikizo la wazazi, wapo wazazi wamekua wakiwalalamikia watoto zao kuwa umri unaenda wanataka wajukuu

2. Lipo kundi ambalo wameoa/kuolewa kwasababu wamekua wakiona watu wa rika zao wote wameoa hivyo wana inferior kuwa jamii inawaona kwa jicho baya

3. Wapo walio oa kwasababu ya mkumbo wamekuta jamii ikiishi katika utamaduni huo kua umri fulani ni lazima mtu awe ameoa/kuolewa

4. Na saizi wapo wanao oa kwasababu kesho ni mfungo, kundi hili la watu wamejiwekea udhaifu kwamba ni ngumu kuishi katika hicho kipindi bila kufanya ngono, na kufanya ngono ya bila ndoa katika kipindi hicho ni dhambi hivyo inamlazimu aoe ili kuhalalisha ngono

5. Wapo walio oa kwasababu ya uvivu wa kazi ndogo ndogo za nyumbani, hili ni kundi lenye watu wengi sana mpaka sasa. Hii inamaana kwamba watu hawa hawakuingia kwa nia madhubuti ya kifamilia/kindoa changamoto za kufua, kuisha vyombo, usafi kiujumla zimepelekea kufunga ndoa. Hapo utaona nafasi ya mke ni kama beki tatu

6. Lipo kundi la watu walioingia kwenye ndoa kutokana na "HOFU". Hili ni kundi ambalo ukiwauliza kwanini umeoa watakuambia "maisha bila mke ni risk sana kwasababu unaweza ukaumwa usiku ukakosa nguvu hata kushika simu ukashindwa hivyo bila mke waweza kufa"

7. Hawa ni wale walio oa baada ya kukutwa na hatia ya kuzini eidha alimpa mimba mwanamke kwa bahati mbaya hivyo ikamlazimu amuoe. Wapo pia wanawake watukutu waliogomea kwenye mageto ya masela kwa kuforce kuolewa

Siku ambayo watu watajua sababu ya msingi kwanini wanaoa kuna uwezekano tukadhibiti kwa kiasi fulani hii migogoro ya ndoa na idadi ya talaka
umegusa mzizi mkubwa saana wa ndoa tulizonazo kwasasa nanyingi zinasua sua saana!! Vijana tujichekeche saana , Ndoa zinakuwa ngumu kutokana na sababu kuu Kama hizi zilizopelekea kufunga Ndoa!!!!

#Umetoa points hizi kama ulikua kwenye brain yangu
 
Habari za leo watanzania wenzangu?

Nimeshangaa tu jana usiku mpenzi wangu from nowhere kanitumia ujumbe kwenye simu kuwa, mwaka huu ukiisha kama sijamuoa, basi yeye atafanya maamuzi magumu na nisimlaumu kwa lolote.

Hapa nawaza, huyu ni kwamba sasa hivi ana mtu mwingine ndio maana ananipa hii ultimatum au tatizo nini?
Achana nae, anakuletea kauli za ajabu ajabu. Soko bado liko vizuri, tafuta mwingine songesha mpaka ukiwa tayari kuoa
 
Inabidi iwekwe sheria kabisa mwisho miaka mitatu usipomuoa mmojawapo alipwe pesa
 
Nadhani kati ya watu walotoa ushauri basi ushauri wako nimuhimu sana,umeandika maneno machache yenye ujumbe mzito,binafsi simshauri aoe kwa sababu ya pressure kutoka upande mmoja kwenye kuoa kila mtu anamipango yake na wengine wanakuwa na malengo ya kutimiza ndo wakaoe,unaoa et kwa sababu wadogo zako wote wameoa??ni ujinga,unaoa et kwa sababu classmates wako wote wameoa ni ujinga,unaoa et kisa una miaka 30 ni ujinga?kikubwa ishi kwa malengo
Mkuu malengo gan huwez jua huenda malengo yakatima akiwepo yy kina mwanamke na nyota yake hata mm Nina mpango wa kuoa labda maisha yatabadilika nimegundua ukiwa hujaoa matumiz ni makubwa bata mpaka saa nane usiku kwa sabab nan atakuliza ngoja nioe labda tabia itabadilika maana kurud saa mbili home nimeshindwa kabisa
 
Mkuu nakushauri uanze kubadili hiyo mienendo yako kwanza kisha ndio ufunge ndoa.
 
Habari za leo watanzania wenzangu?

Nimeshangaa tu jana usiku mpenzi wangu from nowhere kanitumia ujumbe kwenye simu kuwa, mwaka huu ukiisha kama sijamuoa, basi yeye atafanya maamuzi magumu na nisimlaumu kwa lolote.

Hapa nawaza, huyu ni kwamba sasa hivi ana mtu mwingine ndio maana ananipa hii ultimatum au tatizo nini?
Ana haki ya kukuacha miaka mitatu unataka kugundua nini kutoka kwake?
 
Kama umeridhika na yeye na unaona kabisa she will be a good mother rto your kids muoe tu.

Ndoa raha sana ndugu yangu. Usiangalie ndoa zilizofeli, mbona zipo nyingi tu ambazo watu wamefanikiwa?
 
Mimi nagonga mwaka wa 13 sijaoa bado....
namuahidi nitamuoa 'mke' wangu kwa ndoa ya kidini but tuna watoto watatu
ila mwaka huu lazima nioe
 
Mkuu malengo gan huwez jua huenda malengo yakatima akiwepo yy kina mwanamke na nyota yake hata mm Nina mpango wa kuoa labda maisha yatabadilika nimegundua ukiwa hujaoa matumiz ni makubwa bata mpaka saa nane usiku kwa sabab nan atakuliza ngoja nioe labda tabia itabadilika maana kurud saa mbili home nimeshindwa kabisa
Mkuu huo nao ni mtazamo wako siwezi kupinga lakini nizungumzie kdogo swala lako kwamba ukioa utabadilika(umeshindwa kubadilika unasubiri et uoe ndo utabadilika sidhani kama ni sahihi kiivo)ila ni mtazamo wako na naomba mrejesho ukishaoa
 
Ili tuweze kuchangia vizuli tuu Uzi na mleta mada upewe ushauli sahihi mleta mada unatakiwa ufunguke mambo yafuatayo

1.malengo yako na huyu binti ni nini katika mahusiano yenu.

2.je ulishawahi kumuahidi utamuoa ktk mahusiano yenu au

3.kama ndio ulimuahidi utamuoa ni wapi unapokwama hebu tueleze ili tukusaidie jinsi ya kujipanga

4.kama hapana hujawahi kumuahidi kumuoa na huna mipango nae ya kumuoa unataka kukaa na huyo binti ktk hayo mahusiano nae ili iweje mwisho wa siku

5.katika mahusiano yenu ya miaka mitatu nyumbani kwao binti unatambulika

6.Huyu binti ni kweli unampenda au eat and run
 
Back
Top Bottom