Mpenzi wangu kaniacha kisa sina pesa

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Mwaka jana kama mwezi wa 8 nikiwa katika mazingira ya senta yetu nilikutana na mdada miaka 21 kwa jina Anita(si jina halisi). Nikaanza mchakato wa kumuaproach niwe nawe katika mahusiano ambayo hatima yake itakuwa ni ndoa. Katika harakati zile za kumtaka pamoja na ugumu lakini baadae alinielewa na akakubali kuwa na mimi katika shida na raha

Siku zikaenda, siku moja tukiwa faragha tukawa tunapiga stories za hapa na pale nikamgusia kabla yangu ni nani alikuwa naye kwenye mahusiano, akasema alikuwa na mwalimu mmoja wa sehemu fulani lakini baadae waliachana, na ni mwaka umepita tangu kuachana

Pia, akaeleza kwa siku za karibuni kuna mwanaume mtu mzima miaka 38 mwenye familia yake anamtaka ila hamtaki kwa sababu ana familia,ni mzee ingawa ana kazi nzuri ambayo inampa pesa ,kwa hiyo mapenzi si pesa. Aliposema mapenzi si pesa nikasema kwa sauti"Yeeeees asant,nashukuru kumpata mwanamke ambaye anajua maana ya kupenda (mapenzi) maana pesa si lolote katika mapenzi ya dhati

Kwa kuwa na mimi ndo nipo mtaani,nafanya kazi zisizo rasmi kupata kipato sikuwa vizuri kiuchumi ila Anita alionyesha kunipenda kwa hali niliyokuwa nayo akinipa matumaini siku moja tutapata pesa na tutaishi maisha mazuri

Mambo yalianza kubadilika baada ya siku moja kuniaomba elfu 30 anunue nguo,kiukweli sikuwa nayo nikamwambia avumilie nitafute

Kila siku jioni akawa ananitext anaulizia hiyo hela ,nikawa namwambia sijapata bado,sasa na mimi kwa sababu ya hiyo hela sikutaka kumuomba mchezo maana niliona aibu

Siku moja nilihisi kuzidiwa na ugwadu nikamwambia bila aibu akaja gheto nikamaliza,ila baada ya mchezo akaeleza mapungufu anayopungukiwa hadi nikahisi kuchanganyikiwa ,basi akaondoka

Baada ya siku 2 akanitext anaomba elfu 15 anunue mafuta ya kupaka na pedi,nikamwambia sina. Kuanzia hapo akaanza kupunguza mawasiliano,ikawa mimi ndo nimtafute,nikajua hela ndo tatizo ila namna ya kuipata sipati njia halali. Nikajikaza kuwa naye karibu lakini bila hela sioni mafanikio

Siku zinaenda ila nahisi kama mahusiano yanazorota, siku moja rafiki yangu akanipigia simu akanambia amemuona Anita mjini maeneo ya hotel ila kama wapo na mwanaume mtu mzima kidogo

Nikajihisi kuchanganyikiwa,hisia zikanipeleka kwa yule jamaa ambaye aliniambia kuwa anamtongoza. Basi baada ya hiyo simu nikampigia Anita simu hakupokea, kama mara 20 hapokei, nikatuma sms hakujibu

Nikazidi kuumia zaidi,jioni nikamuona online WhatsApp ,nikamtumia sms seen hakujibu,nikapiga simu hakupokea,nikatext tena whasap akajibu" Staki kuwa na mwanaume mzigo ,asiyejali ,achana na mimi " ghafla akaniblock ,nikazidi kuumia

Nikamtumia sms za kawaida" pamoja na yote yale uliokuwa unaniambia hujali pesa ,na hutaki mwanaume mzee leo unakula matapishi yako? Akanijibu"ukafungiwa kwenye chumba bila chakula kwa siku 5 lazima utakula kinyes na mkojo wako utakunywa usishangae na matapishi ,maisha mema"

Wadau siko vizuri, nahisi kuchanganyikiwa kabisa.

IMG_20210609_063205_528.jpg
 

sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
4,237
2,000
Pole, tafuta pesa sasa, nadhani Anita kakufunza, mapenzi ya sasa hivi bila pesa hayapo na mwanaume bila kuwa na pesa unaonekana mzigo.

Ongeza juhudi kwenye kutafuta pesa ili uwe na maisha bora, pesa ni sabuni ya roho aisee.
 

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Pole , tafuta pesa sasa , nadhani Anita kakufunza , mapenzi ya sasa hivi bila pesa hayapo na mwanaume bila kua na pesa unaonekana mzigo .

Ongeza juhudi kwenye kutafuta pesa ili uwe na maisha bora , pesa ni sabuni ya roho aisee
Hakika mkuu
 

Brigadier Isaac

JF-Expert Member
Jan 2, 2021
258
1,000
Mtoa mada ningekuwa mimi ningeenda kutoa sadaka ya shukrani jinsi Mungu alivyoniepusha na fedhuri kama huyo

Maana kama ungebahatika kumuoa siku kwenye ndoa mambo yakikuendea ovyo au angetokea mwenye pesa zaidi yako tambua angebadilika kama sasa

Halafu huyo demu wako alikuwa anakucheat tangu muda sema ulikuwa kipofu wa mapenzi ulishidwa kuchambua mambo kwa kina (kiufupi huyo demu anapenda watu wazima)

Mkuu hapo kuondoka kwake kakuepusha magojwa,mateso,pressure,amani ya moyo,kulea watoto wasio wako,kifo cha mapema pia na umaskini maana kama ungekua unamuhudumia na hali yako hiyo ya uchumi sidhani kama ungeendelea,yani mpaka hapo mshukuru Mungu wako ulikuwa unaishi golden diggers moja mkubwa ndio maana hata ukidadisi historia yake ya kudate ni watu wazima wenye mishahara yao halafu akakudanganya hapendi pesa na wewe ukaitikia yes baby
Mimi ushauri wangu kwa sasa achana na mapenzi kabisa jiweke stable kiuchumi kwanza utakuja kunishukuru
 

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
376
1,000
Mtoa mada ningekua mimi ningenda kutoa sadaka ya shukrani jinsi Mungu alivyoniepusha na fedhuri kama huyo

maana kama ungebahatika kumuoa siku kwenye ndoa mambo yakikuendea ovyo au angetokea mwenye pesa zaidi yako tambua angebadilika kama sasa

Halafu huyo demu wako alikuwa anakucheat tangu muda sema ulikuwa kipofu wa mapenzi ulishidwa kuchambua mambo kwa kina (kiufupi huyo demu anapenda watu wazima)

Mkuu hapo kuondoka kwake kakuepusha magojwa,mateso,pressure,amani ya moyo,kulea watoto wasio wako,kifo cha mapema pia na umaskini maana kama ungekua unamuhudumia na hali yako hiyo ya uchumi sidhani kama ungeendelea,yani mpaka hapo mshukuru Mungu wako ulikuwa unaishi golden diggers moja mkubwa ndio maana hata ukidadisi historia yake ya kudate ni watu wazima wenye mishahara yao halafu akakudanganya hapendi pesa na wewe ukaitikia yes baby
Mimi ushauri wangu kwa sasa achana na mapenzi kabisa jiweke stable kiuchumi kwanza utakuja kunishukuru
Dah! Asante mkuu
 

Kambaku

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
4,060
2,000
Mkuu we mtu wa miaka 38 kwanini mnamuita mzee? Ana uzee gani huyo mwalimu?

Pili, ulitaka huyo Anita akae tu hata kumpa 15 ya mafuta humpi? Ujue saa ingine hawa viumbe tunawaonea bure kabisa, wewe ni mpenzi wake tena mchumba unasema kabisa unataka mafuta na pedi nani amnunulie?

Narudia tena kusema, ukizaliwa mwanaume fanya yote pambana uwezavyo ila kaa ujue watoto wako na mpenzi wako ni jukumu lako kuwalea! Hii haijalishi huyo dada ana hela au hana! Sasa wewe kabinti ka miaka 21 unataka kasikuombe matumizi kweli? Na bila haya unakapanda kila ukisikia ugwadu

Endelea kuwaza kuwa mapenzi sio pesa alafu utaona mwisho wake. Kwanza sio ishu ya mapenzi ni pesa ila ni ishu ya mwanaume kumuhudumia mpenzi wake fullstop
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom