Kijana pole sana kwa hayo yaliyokukuta natambua utakuwa umeumia sana Psychologically ila naomba nikueleze hivi;
Kwanza inavyoonekana huyo unayetembea naye bado ni mtoto mdogo na ni mwanafunzi ndo maana alipopata ujauzito mliamua mtoe mimba kitu ambacho ni kosa la jinai kisheria lakini pia ni dhambi kwa Mungu.
Pili, kwa uelewa wangu, mnatawaliwa na matamanio ya kimwili (emotions) na siyo mapenzi ya kweli (true/real love) na ndo maana alipopata mimba haukuwa tayari kumuoa au kumpa matunzo ili aweze kulea mimba na yeye kwa sababu tu ya kutokuwa na mawasiliano mazuri kwa miezi minne aliweza kuwa na mwanamme mwingine kwa kisingizio cha kupata msaada wa mahitaji ya shule. Je kama leo hana maitaji ya shule anaamua kutembea na wanaume wengine sasa swali, je kwa mfano, mkija kuoana na ukashindwa kuja kutunza familia kutokana na sababu ambazo zitakuwa nje ya uwezo wenu na majukumu yakambakia yeye huoni kuna uwezekano wa kuja kutoka nje ya ndoa ilimradi aweze kulea familia ukiwemo na wewe?
Tatu, kwa kawaida mapenzi ya awali yakipotea, ni vigumu sana kuyarudisha labda mpaka kila mmoja adhamirie kwa dhati kabisa toka moyoni mwake vinginevyo kila siku mtakuwa wa kugombana na kukosana make kwa mfano nyie kule kuaminiana kumeshapotea
Mwisho, USIRUHUSU HISIA ZA MAPENZI ZIKAKUTAWALA, UUTAWALE MOYO WAKO. Jiulize swali hili, Ni kweli unampenda huyo dada kwa dhati kabisa au kwa kuwa umemzoea? Au kuna mambo flani ambayo amewahi kukufanyia yanayokufanya uchanganyikiwe na badala ya kuona ni tamaa tu we unaona kama ni upendo?
POLE SANA ILA KUWA MAKINI.